Mchango wa madini kwenye Pato la Taifa wazidi kuongezeka

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Waziri wa Madini Dkt. Dotto Biteko amesema mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 6.8 hadi kufikia asilimia 9.11 kwa mwaka 2022/23.

Pia amewataka wafanyabiashara wa madini kuhakikisha wanarejesha mauzo kwa fedha za kigeni. Dk Biteko alisema hayo Dodoma jana wakati wa kikao cha wafanyabiashara wa madini kujadili mwenendo wa biashara ya madini yanayouzwa nje ya nchi.

Alisema kwa mwaka 2022/23, mauzo ya madini ya dhahabu, almasi na madini ya vito yaliyofanywa na wafanyabiashara yamefikia thamani ya dola za Marekani milioni 952.9.

Aidha, Biteko alisema kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wafanyabiashara wa madini kuuza madini nje ya nchi bila kurejesha fedha za mauzo katika benki za hapa nchini kwa mujibu wa sheria hali inayopelekea kupungua kwa fedha za kigeni.

Alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo aunde kamati ili kufanya tathmini ni kwanini fedha hizo hazirudi kwa kiwango kinachotakiwa nchini. Alisema sekta ya madini imekuwa na mchango mkubwa katika kuchangia upatikanaji wa fedha za kigeni kutokana na mauzo ya madini ya aina mbalimbali.

Dkt. Biteko alisema mchango wa sekta ya madini katika kuliingizia Taifa fedha za kigeni umekuwa ukiimarika ambapo mwaka 2022 madini yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 3,395.3 yaliuzwa nje ya nchi sawa na asilimia 56 ya mauzo yote ya bidhaa nje ya nchi.

"Mauzo hayo ni ongezeko la asilimia 9 ikilinganishwa na mauzo ya dola za Marekani milioni 3,116.40 mwaka
2021," alisema.

Dkt. Biteko alisema pamoja na mafanikio kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wafanyabiashara wa madini kuuza madini nje ya nchi bila kurejesha fedha za mauzo kwenye benki za hapa nchini.

"Mfano tunajua Katika mwaka 2022/23 wafanyabiashara wa madini kupitia kampuni zao walisafirisha nje ya nchi jumla ya madini yenye thamani ya dola za Marekani 952,926,784 sasa hebu tuiihoi ni kiasi gani cha fedha hizo kilirejeshwa katika akaunti zenu za benki za hapa nchini?" Alihoii DkBiteko.​
 
Ukitaka kuwa maskini hii nchi kuwa mkulima, ukitaka kuwa tajiri ingia kwenye hii sekta ila jipange.
 
Back
Top Bottom