Inavyoelekea CHADEMA wakiingia madarakani kila mbunge atakopeshwa Helkopta yake ya kuzungukia jimbo.
hujitambui Nasary anakula kodi zetu wameru kukodisha helkopta.
Inavyoelekea CHADEMA wakiingia madarakani kila mbunge atakopeshwa Helkopta yake ya kuzungukia jimbo.
We hela yako uliyotumia kununua simu yako na kununua bando umeitoa wapi? Hujui kuna watu wanakosa hata mlo mmoja,kwanini hiyo hela usingewasaidia wagonjwa wasio na ndugu,watoto wa mtaani watu wenye njaa.Huoni kuwa una matumizi mabaya ya pesa.Nadhani una washauri wabaya
hujitambui Nasary anakula kodi zetu wameru kukodisha helkopta.
Mkuu mmaranguoriginal hivi unakumbuka swali langu la kitambo kuhusu ule mradi wa maji wa maji ya chai uliyoyeyushwa na team yako? Bado nasubiri majibu mkuu
mtoa mada umetudhalilisha sana waMARANGU.
Wewe sasa nimeamini lazima utakuwa "Ke" na ulikuwa mchepuko wa Nassary na mambo yalikuendea kombo baada ya yule kijana kuoa. Hapa JF huna hoja nyingine zaidi ya hoja zako za hovyo kama hizi juu ya Nassari tuu?
Hivi kodi gani Nasari anaweza kuIiza kwa kukodi chombo cha usafiri? Yeye ni Accounting Officer wa fedha gani za serikali ambazo anaweza kuzifuja?
Hizo tabia za kimichepuko usituletee hapa JF wenzako wakina Wema wanapeleka kwa Shigongo.
Kama unafikiri chopa ni ishu, njoo na wewe nikuazime kama nilivyo mwazima Nasari.wanabodi nawasalimu sana.
leo katika viwanja vya Seela Singisi mbunge Wa Meru ndugu Joshua Nasary anafanya mkutano Wa hadhara kusemea ilani ya chama chake aliyosimamia miaka takribani mitatu.
mosi karibu wiki mbili mbunge huyu amekuwa akifanya ziara zake kwa kutumia usafiri Wa helkopta katika kata 26 za hapa meru , napata mashaka na maswali kama mwananchi Wake kwamba gharama anayotumia kuzunguka na helkopta hii wakati wanameru wengi bado wanachangamoto kubwa sana kama ukosefu Wa Maji kama kata za Maroroni, kata ya Maji ya Chai , mathalani kijiji anachotoka hivi majuzi shule ya pale ilifungwa kwa ukosefu Wa vyoo.
aghalabu mbunge huyu kakodisha helkopta hii toka nchini Kenya sasa swali la logic inakuwaje gharama ya hizi helkopta asielekeze kutoa misaada kwenye maeneo yenye changamoto kama miundombinu ya barabara n.k
kaleta ambulance bado hajazikabidhi kwa Mkurugenzi Wa haashauri ya Meru ndugu Mallya, mganga Mkuu Wa Wilaya bado hana taarifa ya hizi ambulance , wananchi wanashangaa tu zinapiga ruti kama daladala.
naomba wanaomshauri Nasary wamshauri vizuri , na sisi tunaposema hatuna chuki Bali kukumbushana majukumu.
Nawasilisha.
Kwani mama yako alipata wapi za kukupeleka clinic
Kama kodi hata wewe unakula kodi zetu,mbona unanunua simu na bando badala ya kutumia hiyo hela kusaidia maskini.Umepata wapi hela ya kununulia hivyo vitu? Kasaidie maskini.Unajifanya unamuangalia Nassary kwa jicho la wivu kumbe we mwenyewe jizi.Kwanza una mawazo ya kiwiziwizi kama ulivyo wewe unafikiri kila mtu mwizi.Nassari analipwa mshahara unasema kodi yako kodi yako ipi,yaani jasho lake aanze kukugawia wewe unayeshinda kwenye simu? Kama ni hivyo anza wewe kuwagawia watu kipato chako maana hiyo simu tu ni anasa.
Nina wasiwasi na mtoa mada atakuwa nae anagombea jimbo mwaka huu, sio bure.
Nasary tumempa ubunge miaka mitatu tu kakodisha chopa, tukimuongezea mingine atakodisha ndege binafsi kabisa. hii ni hatari kwa jimbo letu kutopiga hatua
Huyu mmaranguoriginal hagombei ila alikuwa demu wa Nassary akamuacha akamuoa mwingine bifu likaanzia hapo.
Wewe utakuwa chizi.
Kama unafikiri chopa ni ishu, njoo na wewe nikuazime kama nilivyo mwazima Nasari.
Lete issues za maana za kujadili hapa and not this porridge.
Saa moja ni million moja, kwani mbunge atashindwa kukodisha masaa mawili ya kurusha helkopta, na unajua helkopta inafanya mikotano mingapi ndani ya saa moja? Uwe na taarifa za kutosha kabla ya kutoa tuhuma.