Joshua Nassary ametoa pesa wapi ya kukodisha Helkopta?

Joshua Nassary ametoa pesa wapi ya kukodisha Helkopta?

Huyu aliye ileta hii mada hapa katumwa na Zito ahache ujinga
 
hujitambui Nasary anakula kodi zetu wameru kukodisha helkopta.

mkuu wewe ni mkabila sana inaonyesha jimbo la nasary kuna wameru tu.Nyie nyerere angekuwepo angewachapa bakora ajabu.Mbunge ni mwakilishi wa wananchi na sio mfadhili hii ni kutokana na uelewa wangu mdogo na elimu yangu kama yule MKULIMA wa kigoma
 
We jamaa mbona huletagi mazuri anayofanyaga nassari au unalitaka jimbo nn ndo unakuja kiivyo
 
Well hata mimi sishabikii chopa kutumika kwa hali tuliyo nayo labda kwa jambo la dharura tu! Kama anazo ndururu za kutosha awasaidie wahitaji jimboni mwake najua wako wengi tu! Na huko ndiko kujitoa na kuitwa mtu wa watu.
 
Naona chopa imeruka hyooooooo.
Tengeru baiiiii,tutaiona tena octoba.
 
wanabodi nawasalimu sana.

leo katika viwanja vya Seela Singisi mbunge Wa Meru ndugu Joshua Nasary anafanya mkutano Wa hadhara kusemea ilani ya chama chake aliyosimamia miaka takribani mitatu.

mosi karibu wiki mbili mbunge huyu amekuwa akifanya ziara zake kwa kutumia usafiri Wa helkopta katika kata 26 za hapa meru , napata mashaka na maswali kama mwananchi Wake kwamba gharama anayotumia kuzunguka na helkopta hii wakati wanameru wengi bado wanachangamoto kubwa sana kama ukosefu Wa Maji kama kata za Maroroni, kata ya Maji ya Chai , mathalani kijiji anachotoka hivi majuzi shule ya pale ilifungwa kwa ukosefu Wa vyoo.

aghalabu mbunge huyu kakodisha helkopta hii toka nchini Kenya sasa swali la logic inakuwaje gharama ya hizi helkopta asielekeze kutoa misaada kwenye maeneo yenye changamoto kama miundombinu ya barabara n.k

kaleta ambulance bado hajazikabidhi kwa Mkurugenzi Wa haashauri ya Meru ndugu Mallya, mganga Mkuu Wa Wilaya bado hana taarifa ya hizi ambulance , wananchi wanashangaa tu zinapiga ruti kama daladala.

naomba wanaomshauri Nasary wamshauri vizuri , na sisi tunaposema hatuna chuki Bali kukumbushana majukumu.

Nawasilisha.

Nilimpatia kiasi cha kutosha.
 
Nina wasiwasi na mtoa mada atakuwa nae anagombea jimbo mwaka huu, sio bure.
 
hujitambui Nasary anakula kodi zetu wameru kukodisha helkopta.

Ni kweli anakula kodi zenu najua yeye peke yake hawezi kuzimaliza lakini huko kwenye chungu hakuna kilichobaki tafadhali tuambie na hao walaji wengi au ulkuwa unaitengeneza singo ya kodi zenu******
 
Acha kutetea wezi, bunge la katiba ukawa wamekaa muda gani au ndo CDM si wezi ila CCM na ACT??

wapi kwenye comment yangu nimeweka CCM, CDM, ACT au Ukawa....kama lengo lako lilikuwa kuwatusi CDM ungewatusi moja kwa moja lakini umeleta hoja ya nassari as an individual....jaribu kuwa unashirikisha akili yako na ufahamu wako.
 
.... Za Lowasa Na Watia Nia Wa Ccm Za Kuhonga Wazamini Zimetoka Wapi? Nyani Haoni Kundule.
 
Back
Top Bottom