Joshua Nassary ametoa pesa wapi ya kukodisha Helkopta?

Joshua Nassary ametoa pesa wapi ya kukodisha Helkopta?

Nina mke tayari.

ungeuliza na hilo kapatikana wapi huyo binti? unamshambulia nasari mpaka unaonekana kituko, huwezi kuzuia mafuriko tulia tu, nyota yake kung'aa ni wakati huu, subiri itafika muda itazima kwa mipango ya Mungu, acha kutumbua nyongo yako.
 
Kinana anatoa wapi pesa za kufanya mikutano yake?
 
Mkuu majibu mepesi na hovyo kwa mada nyepesi na ya ovyo. Usiogope.
 
Kwan hela ya kampeni kabla hajawa MBUNGE aliitoa Wapi mbona haukuuliza wakati huo, jibu rahis ni katoa mfukon mwake
 
Yeye badala ya kununua/kupeshwa SHANGINGI kaamua anunue/akodishe CHOPA
 
Acha wivu wa kike ww utauliza hata mtu akioa mke wa pili kuwa uwezo wa kuzimudu anaupata wapi
 
We jamaa mbona huletagi mazuri anayofanyaga nassari au unalitaka jimbo nn ndo unakuja kiivyo
mkuu huyo dada ndo alivyo na ndo maana wanamdharau hata majibu serious hapewi coz ana atittude anaishia kupata matusi tu
 
wanabodi nawasalimu sana.

leo katika viwanja vya Seela Singisi mbunge Wa Meru ndugu Joshua Nasary anafanya mkutano Wa hadhara kusemea ilani ya chama chake aliyosimamia miaka takribani mitatu.

mosi karibu wiki mbili mbunge huyu amekuwa akifanya ziara zake kwa kutumia usafiri Wa helkopta katika kata 26 za hapa meru , napata mashaka na maswali kama mwananchi Wake kwamba gharama anayotumia kuzunguka na helkopta hii wakati wanameru wengi bado wanachangamoto kubwa sana kama ukosefu Wa Maji kama kata za Maroroni, kata ya Maji ya Chai , mathalani kijiji anachotoka hivi majuzi shule ya pale ilifungwa kwa ukosefu Wa vyoo.

aghalabu mbunge huyu kakodisha helkopta hii toka nchini Kenya sasa swali la logic inakuwaje gharama ya hizi helkopta asielekeze kutoa misaada kwenye maeneo yenye changamoto kama miundombinu ya barabara n.k

kaleta ambulance bado hajazikabidhi kwa Mkurugenzi Wa haashauri ya Meru ndugu Mallya, mganga Mkuu Wa Wilaya bado hana taarifa ya hizi ambulance , wananchi wanashangaa tu zinapiga ruti kama daladala.

naomba wanaomshauri Nasary wamshauri vizuri , na sisi tunaposema hatuna chuki Bali kukumbushana majukumu.

Nawasilisha.
Nimempa mimi baada ya kuona zimenizidi! Na mimi hizo hela nilihongwa na mama yako! Ina maana mama yako alizichukua hizo hela bila ya ninyi kuwa na taarifa?
 
Naona Nassary amekushikeni pabaya hawaachi mmpumue.Poleni basi
 
Back
Top Bottom