Nimefatilia sana matamko ya Zitto na Mkumbo na nimeona niwashauri wafanye yafatayo ili kujiosha na shutuma hizi juu yao.
1. Zitto weka wazi kama kweli unafahamiana na yule mwanamke raia wa Ujeruman na imekuwaje wachafuzi wako waku connect naye?
2. Zitto hupokei posho na huli rushwa, tueleze unawezaje kumiliki nyumba kubwa ya gorofa na gari expensive aina ya Range Rover New Model?
3. Zitto hivi umewahi kuwatumia pesa washutumiwa wale wote kwa njia ya mitandao ya simu? Kitila, Shibuda, mwampambe, shonza nk.
4. Zitto unafahamu hizi shtuma hazijakilenga chama ila wewe na wenzio indidually; na wala chama hakijatoa shutuma hizo bali watu binafsi kama wao. Sasa inakuwaje unadai kumtaka katibu mkuu kutoa tamko? Kwani yeye atoe tamko kwa kukusemea wewe au kuwasemea wale wanaokushutumu ambao naye hawajui pia? Humtendei haki kiongozi yeyote wa chama kutaka akutetee. Kwanini usimtake na kumwomba mtuhumiwa mwenzio Ben Sanane anayeonekana mda wote JF akusaidie kueleza ukweli? Unaogopa anaweza kuharibu zaidi?
5. Zitto wewe ni kiongozi mkubwa Chadema lakini unadai umemwandikia barua katibu mkuu wa chama chako juu ya swala hili hajarespond; je hamna mazoea ya kuwasiliana kwa simu wakat mwingine hata na Mweyekiti wako? Twambie kabla hata ya wao kuja na thibitisho au kanusho unazotaka lakini wanakushaurije au wanakwambije juu ya kashifa hii? Au hamuwasiliani?
6. Zitto mikutano yako ya kichama na ziara zako zote mikoani kwa sasa zinaratibiwa kichama? Ziko kwenye ratiba ya ziara za viongozi wa chama? Huwa unarudisha mrejesho? Unwasilisha wapi mrejesho? (Feedback)
Dr Kitila ntakujia baadae jiandae kujibu tuhuma sio kupanic na kudai huongeki. Wewe bado sana kuridhika kifedha kaka nakufahamu. Jibu tu shutuma tene kwa busara na hekima ujikoshe!!