John Mnyika: CHADEMA haihusiki na 'Taarifa ya Siri'

John Mnyika: CHADEMA haihusiki na 'Taarifa ya Siri'

Kuhusu Huyu Kijana Kamwulize Lukuvi Na Makinda, Watapingana Na Kauli Yako

Labda leo kwa mara ya kwanza atakiri na atasema, wale Lukuvi na Makinda hamna kitu kichwani kwani MaCCM huwaga yanajitoa akili. Na akikosa hoja kabisa atakwambia, Wamemsifia eti kwasababu ni MKATORIKI mwenzao. Maana hili lijamaa Ritz, linapenda udini hilo!!
 
mjadala umeisha
Hili ni pigo lingine kwa CCM...
ngoma mlioanzisha imeshapasuka...katafuteni plan E
Mnyika keshafunga jalada
 
Jamani kweli mfa maji haachi kutapa kwanza huyu zitto aeleze kuwa amehamia chama gani mpaka leo aombe kuzibitishiwa na chama ambacho mimi natambua kuwa yeye ndiye katibu msaidizi sasa kama yeye tarifa hiyo hana anataka katibu wake apike tarifa za kumzibitishia? Na kama ni muungwana sehemu ya kupata ukweli ni ndani ya kamati husika na wala sio kwenye vyombo vya habari na natambua analijua hilo ila ameamua kutekeleza aliyokusudia kufanya
 
Kweli Mnyika ana kichwa kitupu na kuna kila sababu ya kushinikizwa arudi shule angalau apate hata cheti cha uandishi wa habari...maana hajui lolote kuhusu habari huyo Mnyika.

Kwahiyo Nape ana cheti cha uandishi wa habari?

Jinga kabisa wewe.
 
1.Mnyika ameikana taarifa ya siri juu ya ZZK mtandaoni kuwa si ya kutoka makao makuu.

2. Kwamba, amewataka wa trace chanzo cha taarifa na kwenda mahakamani kuwashtaki wahusika ukweli ujulikane.

hapo kwenye no. 2 mwananchi wameficha hiyo statement.
 
mjadala umeisha
Hili ni pigo lingine kwa CCM...
ngoma mlioanzisha imeshapasuka...katafuteni plan E
Mnyika keshafunga jalada

Kwa kweli Mnyika ameongea kwa hekima kubwa sana.

Mjadala umeshafungwa!
 
kwa kifupi ninavyowafahamu viongozi wa chadema hawawezi kufanya ujinga huo,hizo ni njama za magamba kutaka kuwachonganisha chadema, ninavyoamini chadema hawana muda wa kunuogopa mtu kama wanawasiwasi na mtu fulani umuambia wazi chadema sio kama ccm wanaoneana haya.pamoja na njama zote hizo za ccm mwisho wa ccm ni 2015
 
Wacheni mambo yasiyo na Tija, kajisajilinl kwanye misingi yenu. Zitto nenda Tabobora ukawashe moto wa ukombozi. msikubali kucheza ngoma za CCM.

Shutuma za mitandaoni hujibiwa mitandaoni, inakuwaje Zitto unakimbizia hoja za mitandaoni kwenye Chama? Utamuandikiaje Katibu Dr. Slaa akujibu mambo yaliyo ibuliwa mitandaoni? Hoja za huku zibaki huku huku mpaka hapo atyakaye ziropoka Uraiani huyu ashughulikiwe kwa mujibu wa Sheria.

TCRA imeelekeza, ukipata ujumbe usiofaa mtandaoni (sms, mail,...), "futa kabisa delete yote". Sasa wewe unamtaka Dr. Slaa athibitishe au akanushe! Yanamuhusu nini mambo yenu ya mitandaoni?

Dr. Kitila Mkumbo usifuate mkumbo wewe ni mtu unaeheshimika kuliko kijana Zitto umri bado ni changamoto kwake. Kama si kweli wala huna haja ya kupanic, yapuuzie kwani ni upepo utapita. Jiwe limerushwa kwenye kichaka kama mnapiga kelele za maumivu basi ni kweli kuna haja ya kuwachunguza kwa nini mmejificha kwenye chaka hilo!

Mambo ya mtandaoni msiyapeleke ofisini jibuni tuhuma humu humu na mahakimu wa humu watatoa hukumu humu humu mtandaoni.

NA KAMA MTALAZIMISHA DR. SLAA ATAMKE KITU BASI TUTAFAHAMU LENGO LENU LA KUVURUGA CHAMA MNATAKA LIKAMILIKE SASA KAMA "RIPORT YA SIRI" INAVYOSEMA. KWANI MNAOKOTA VITU MITANDAONI MNAVIFANYA VIWE OFFICIAL ISSUE. NAOMBA DR. ASIJIBISHANE NAO.
 
Kwahiyo Nape ana cheti cha uandishi wa habari?

Jinga kabisa wewe.

Unawezaje kumlinganisha mtu mwenye masters degree (Nape) na huyo form six leaver (Mnyika) katika nyanja ya kiupeo, tafakuri na uchambuzi wa mambo?

Nape ni mtu sahihi katika nafasi aliyonayo sasa hasa kwa uwezo wake wa kijibu hoja mbalimbali zinazoibuliwa na wapinzani na zenye kuathiri chama tawala. Ila huyo Mnyika unaweza kuona pumba alizoongea kuhusu sakata la Zitto. Mnyika arudi shule kwa kuwa ana kichwa kitupu mno.
 
Unawezaje kumlinganisha mtu mwenye masters degree (Nape) na huyo form six leaver (Mnyika) katika nyanja ya kiupeo, tafakuri na uchambuzi wa mambo?

Nape ni mtu sahihi katika nafasi aliyonayo sasa hasa kwa uwezo wake wa kijibu hoja mbalimbali zinazoibuliwa na wapinzani na zenye kuathiri chama tawala. Ila huyo Mnyika unaweza kuona pumba alizoongea kuhusu sakata la Zitto. Mnyika arudi shule kwa kuwa ana kichwa kitupu mno.

Imesemwa Ficha upumbavu wako lakini usifiche hekima yako!
 
Nami naunga mkono.Ni vyema chama kikatoa msimamo kwamba huu ni uzushi na kazi ya kujenga chama iendelee.

Kwa hiyo alichosema Mnyika siyo taarifa ya chama?

Hakika uelewa wa binadamu unatofautiana sana...
 
Mnyika unataka Dr Kitila Mkumbo akae kimya asijisafishe mbele ya jamii malalamiko yake ayapeleke Chadema.

...Hapa nimemdharau Mnyika,yawezeka nae yupo kwenye timu iliyo nyuma ya uchafuzi huu....
 
+255754787550 Mbona hio namba imesajiliwa kama John Majige?
 
CHADEMA ni mpango wa MUNGU ..hatuyumbishwi na maccm...
forward ever backward never
 
...Hapa nimemdharau Mnyika,yawezeka nae yupo kwenye timu iliyo nyuma ya uchafuzi huu....

Ulitaka usikie kipi kutoka kwa Mnyika?

Mnyika amejibu kwa hekima kubwa.
 
USHAURI WA BURE KWA ZITTO

Nenda makao makuu ya CDM kaongee na Katibu mkuu wako Dr Slaa,kumuandikia barua hujatumia busara hata kidogo.
lakini ukiwa m/kiti wa PAC ulitoa tuhuma nzito za ubadharifu wa ruzuku ya CDM na ukamtaka Slaa aje kwenye kikao cha PAC kujibu tuhuma leo hii umemwangukia Dr slaa ili akusafishe na tuhuma zako za kifisadi!
 
Uchaguzi ukikaribia ndipo vyama vya upinzani vinaanza upumbavu. Huyu Zito na Mkumbo wameamua kucheza ngoma za kuvuruga chama chao badala hata ya kuanza kujadili mambo hayo huko chamani kwao ambapo Zito ni mmoja wa viongozi wake. Wao wakakimbilia vyombo vya habari ili kuongeza nguvu kwenye ngoma ya kubomoana. Jambo la ajabu sana hilo. Zito akiwa naibu katibu mkuu siyo mtu wa kumwandikia barua Katibu mkuu na kutangaza hivyo; alishawahi kufanya hivyo tena huko nyuma. Kwa nini afanye hivyo kama hakuna sababu nyuma ya pazia?

Nina mashaka sana na kiini cha mgogor huo.
 
dr slaa na mbowe toeni tamko tuwe huru na haya majitu ya ccm mtandaoni

Haya ndiyo malipo ya viongozi wanaopenda sana kutoa matamko mitandaoni.Matamko wayatolee mitandaoni ,majibu waombe kutoka uongozi?
Kwanza mie hii taarifa naweza kuona pengine akina zitto wenyewe ndio walioitengeneza ili kuweza kujinufaisha kisiasa.
 
Back
Top Bottom