Mnyika awajibu
Hata hivyo, Katibu Mwenezi wa Chadema, John Mnyika ameikana ripoti hiyo na kueleza kuwa haijaandikwa na makao makuu ya Chadema.
Mnyika alisema Zitto ameibua kitu ambacho anafahamu kuwa kimeshughulikiwa na uongozi wa chama hicho.
Zitto anajua kuwa Andrea Cordes aliniandikia baruapepe na nakala kwake nikawajibu kuwa ripoti hiyo haijaandikwa na Makao Makuu ya chama na tukipokea malalamiko rasmi tutachunguza kwa sasa chama kinaichukulia ripoti hiyo kama ripoti nyingine zinazosambazwa mitandaoni, alifafanua Mnyika.
Akizungumzia malalamiko ya Dk Mkumbo, Mnyika alisema alikuwa anapaswa kufuata taratibu za chama kama alikuwa na malalamiko.
Alisema baada ya taarifa hiyo ya siri kusambaa mtandaoni, Zitto alitoa kauli na kama Dk Mkumbo hakuridhika, alipaswa kuonana na watu wa Idara ya Uenezi ya Chadema.
Idara ingetoa ufafanuzi zaidi. Mjadala huu usikuzwe bila sababu za msingi na kufunika masuala mengine muhimu ya kitaifa, alisema Mnyika.
Well said Right answers at the right time...Mmejifunza nini kutoka kwa JJ @Nape na ZZK?