JK na wabunge wa CCM Dodoma kimenuka

JK na wabunge wa CCM Dodoma kimenuka

mswada gani ulikuwa wa chadema wewe,au bado hujapona kale ka ugonjwa kako.
 
Kwa umri wangu huu mdogo wa angalau miaka kama thelathini, sijawahi kuona na kushuhudia wabunge wanaosahau wajibu wao wakiwa bungeni.Sijui hiki kizazi cha wabunge wa CCM (walio wengi), japo wachache kusahau kuwa wakiwa bungeni wanawakilisha wananchi wa majimbo walikotoka.Nilitegemea watasimamia kidete yale ambayo wananchi wanayataka lakini cha ajabu na mbaya zaidi, wanasema yale waliyo nayo wenyewe na sina imani kama huwa wanazunguka kusikia kilio cha masikini Watanzania.

Lakini kinachonikera ni kuona Raisi mwenye rungu la kila aina analea ujinga usio na sababu, wabunge wamemdanganya si mara moja,mswada unapitishwa kwa asilimia 100,wananchi wanaupinga, anaalika mabalozi na wageni wengi ikulu eti anasign mswaada kuwa sheria,mara unasikia kuna marekebisho,hivi nani ambaye ameshawahi kujiuliza ule mda waliotumia kubishana bungeni na wakakubali kupitisha ujinga na huku wakijua ni ujinga, si heri wangeenda vijijini wakalime?

Kama kweli Mheshimiwa Raisi ana mamchungu na wananchi wake, vunja bunge, wabunge wako wanakuaibisha na mwisho wa siku wewe ndo unaonekana KILAZA(hujui kitu),na nasikitika kusema nami nachelea kusema labda ni serikali kwa ujumla yote ni VILAZA au hamshauriki.

Serikali gani inaacha wagonjwa wakifa huku wakitanua,hata Raisi,mimi natamani ningekuwa na Uwezo ningewachapa viboko!!Ila sisi wakristo tunaambiwa tuwaombee wabaya wetu na adhabu kutoka kwa Mungu ni kali sawasawa!!Eee Mungu inusuru Tanzania na ufisadi na ujinga wa serikali yetu, ili tuweze kujua tunakoenda.

Kikwetu ukishindwa kuchukua maamuzi magumu,afadhali ujiuzulu,utaheshimiwa duniani kote na wananchi watakupokea kwa nderemo kubwa. Lakini uking'ang'ania madarakani kwa kucheka na wanafiki wako, sipati picha mwaka 2015, chama mbadala kikichukua hatamu, sijui mtakimbilia wapi? Jenga heshima mapema
Nawasilisha!!!
 
Kama una maana JK kawaambia wabunge wampigie kura ya kutokuwa na imani nae, hap namuunga mkono JK, kwani hizo kura hazitatosha na wabunge watajifunza kwa viboko sasa, kwani pamoja na mapungufu aliyonayo Rais, kama alivyo binadamu mwingine, Rais katika hili kasimamia upande sahhihi, na ni upande wa walio wengi nchi hii.

JK kafanya makosa mengi katika uongozi wake lakini katika jambo hili wengi tupo nyuma yake maana watu makini humwunga mkono au kutomwunga mkono mtu yeyote siyo kwa itikadi yake, sura yake, imani yake, kabila lake, n.k. bali ni katika fikra na matendo yake.
 
Kama baraza la mawaziri litavunjwa, naunga mkono hatua hiyo kwa asilimia mia moja kwa sababu baraza lote limeunder perform tangu liingie madarakani. Bora liteuliwe jingine ambalo litaendana na kasi ya mabadiliko.
 
Labda arudi Mwakyembe pekee, ila hawezithubutu kuvunja bunge.
A%20S%20embarassed.gif
 
Usually kabla ya kufanya maamuzi serikali yetu inaangalia garama husika. kama unakumbuka hata wakina Kafulila na Hamadi Rashidi kilichowaokoa ni garama ya uchaguzi. Tunasubiria tukiwa vizuri kifedha tunariadhia maamuzi ya vyama vyao. So kwa hili itakuwa ndoto
 
Spika atakuwa Mzee 6..tunarudisha standard and speed yetu ya kipindi killee...
 
Kama TISS wanaona upuuzi yeye mwenyewe haoni, sasa anafanya nini pale Ikulu?

a man passed past a hyner(spelling?),the man hand as always was hanging and swinging.the hyner was hungry so it began following the man hoping the man hands could fall so that it can eat them.because of hyner foolishness it walked a veeerry looong distance and no hands dropped.
SO YOU BETTER FIGURE IT OUT FOR YOURSELF body.
 
Kuna tetesi kuwa huenda yale yaliyotokea mwaka 2008 yakajirudia tena. Safari hii mtoto wa Mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda Waziri Mkuu anaachia ngazi ya Uwaziri Mkuu baada ya tuhuma nzito tatu(3)zinazomkabili katika ofisi hiyo nyeti.
  1. Mizengo Pinda anatuhumiwa kuwa kwa kushirikiana na spika wa Bunge Anne Makinda AMELIDANGANYA BUNGE KUHUSU POSHO ZA VIKAO ZA WABUNGE KUWA RAIS KIWETE ALIKUWA AMERIDHIA NYONGEZA HIYO YA POSHO KUTOKA SHS.70,000/= MPAKA SHS.200,000/=kitu ambacho siyo kweli.
  2. Mizengo Pinda akishirikiana na Waziri wa Afya na NAIBU wake anatuhumiwa kushindwa kusimamia ipasavyo ili kuepusha au kuzuia MGOMO WA MADAKTARI MUHIMBILI MGOMO AMBAO HATIMAYE ULIPELEKEA MGOMO WA MADAKTARI NCHI NZIMA.
  3. Mizengo Pinda kama Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni ameonyesha UDHAIFU mkubwa kwa kushindwa kuwasimamia Wabunge wa CCM ambao wametishia kupiga KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA RAIS WAO Kiwete na pia kutishia KUPINGA MSWADA WA KATIBA MPYA YA JMT.
naongeza hapa
4. Pinda ni waziri mkuu wa kwanza anayeongopea bunge na uongo wake kudhihirika haraka sana

5. Akishndwa kujibu maswali hukumbilia kulia hivyo kuonewa huruma na wabunge

6. amekuwa anatafutwa kupendwa na makundi yote yanasigana ndani ya bunge na chama chake hivyo kupelekea kukosa maamuzi ya kimaendeleo
 
Kuna tetesi kuwa huenda yale yaliyotokea mwaka 2008 yakajirudia tena. Safari hii mtoto wa Mkulima Mizengo Kayanza Peter Pinda Waziri Mkuu anaachia ngazi ya Uwaziri Mkuu baada ya tuhuma nzito tatu(3)zinazomkabili katika ofisi hiyo nyeti.
  1. Mizengo Pinda anatuhumiwa kuwa kwa kushirikiana na spika wa Bunge Anne Makinda AMELIDANGANYA BUNGE KUHUSU POSHO ZA VIKAO ZA WABUNGE KUWA RAIS KIWETE ALIKUWA AMERIDHIA NYONGEZA HIYO YA POSHO KUTOKA SHS.70,000/= MPAKA SHS.200,000/=kitu ambacho siyo kweli.
  2. Mizengo Pinda akishirikiana na Waziri wa Afya na NAIBU wake anatuhumiwa kushindwa kusimamia ipasavyo ili kuepusha au kuzuia MGOMO WA MADAKTARI MUHIMBILI MGOMO AMBAO HATIMAYE ULIPELEKEA MGOMO WA MADAKTARI NCHI NZIMA.
  3. Mizengo Pinda kama Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni ameonyesha UDHAIFU mkubwa kwa kushindwa kuwasimamia Wabunge wa CCM ambao wametishia kupiga KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NA RAIS WAO Kiwete na pia kutishia KUPINGA MSWADA WA KATIBA MPYA YA JMT.
Kwa mwenye habari za undani zaidi kuhusu hizi tetesi naomba aendelee kutupasha zaidi.

Nawasilisha

Wewe ndio unatupasha sisi habari,sasa hizo tetesi tuzitoe wapi?
 
JK, tangu achukue uongozi wa Taifa letu amefanya makosa mengi lakini tuna haki, na kwa kweli tuna wajibu wa kumwunga mkono, kumlinda, na kumpa moyo wa kusonga mbele anaposimamia jambo lenye maslahi kwa Taifa. Watu makini, siku zote humwunga mkono kiongozi siyo kwa itikadi yake, urafiki, sura yake, dini yake, kabila lake au jinsia yake, bali kwa kile anachokiamini na kukisimamia.
JK, katika suala la upatikananji wa katiba, japo halikuwepo katika ilani ya uchaguzi wa CCM, pamoja na upinzani kutoka kwenye chama chake na watendaji wa serikali yake, yeye kwa busara yake alitamka kuwa, 'Ni lazima tupate katiba mpya'. Hiyo kukubali tu kilio cha Watanzania cha miaka mingi, tuna haki ya kumpongeza iwe alifanya hivyo kwa dhamira yake au kwa kulazimishwa na mazingira ya kisiasa yaliyokuwepo.
Kuhusu mswada wa sheria ya upatikanaji wa katiba mpya, bila shaka mswada huo Rais aliuona kabla ya kupelekwa bungeni. Rais alifanya makosa kukubali mswada huo upelekwe bungeni kama ulivyokuwa lakini nina hakika Mwanasheria Mkuu na Waziri wa Sheria, hawa walifanya makosa makubwa kuandaa mswada wa ovyo namna ile. Na sitashangaa kama watu hawa walifanya kila jitihada kumshawishi Rais akubali kuwa mswada ule ulikuwa ni mzuri. Sina uhakika kama JK aliuelewa vizuri, na aliutafakari kwa makini. Kuruhusu mswada wa ovyo namna ile kwenda bungeni, JK pamoja na watendaji wake walifanya kosa kubwa, na kama Rais anaamini washauri wake hawakufanya kazi vizuri, alistahili kuwafukuza kazi Mwanasheria Mkuu na Waziri wa Sheria mara moja ili marekebisho ya sheria hii ya mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya yawasilishwe na Waziri na Mwanasheria mpya.
Pamoja na makosa ya serikali ya JK kupeleka mswada wa hovyo bungeni, na kisha kupitishwa na wabunge maslahi wa CCM bila ya kuangalia maslahi ya Taifa, tuna haki ya kumpongeza JK kuwasikiliza wadau wengine na kutambua umbumbu wa wabunge wa chama chake. Kwa JK kukubaliana na matakwa ya wadau mbalimbali, na kutupilia mbali matakwa ya mabunge wake mbumbu wa CCM, JK ameonesha uzalendo na ametimiza wajibu wake kama Raia na kama kiongozi wa nchi.
Sasa ni wakati mwingine muhimu kuliko wowote ule kwa JK kuweza kuonesha kwa vitendo kuwa ana uwezo na dhamira ya kusimamia mambo yenye maslahi kwa Taifa. JK ni lazima awatambue na awatangaze hadharani wabunge wa CCM ambao ni maadui wa Taifa letu. Hawa ni wale wabunge ambao hawataki kuwa na sheria yenye kuleta mwafaka wa kitaifa wa kupata katiba yenye maslahi kwa Taifa letu.
WATANZANIA TUNAKUAMBIA JK KUWA JUKUMU LAKO KUBWA NA AMBALO LINAWEZA KUFUTA MAKOSA YAKO YOTE KATIKA UONGOZI WAKO NI UIMARA WAKO WA KUSIMAMIA UPATIKANAJI WA KATIBA BORA, IKIWEZEKANA IWE KATIBA BORA KULIKO KATIBA YA TAIFA LOLOTE. TUKIPATA KATIBA YA HIVYO, HIYO NDIYO ITAKUWA NURU YA TAIFA LETU.
JK una machaguo mawili tu, au kusimama na mamilioni ya Watanzania au na kikundi kidogo cha wabunge wa CCM wenye uchu wa madaraka. Lakini sisi tunatamka wazi kuwa ni lazima tutapata katiba iliyo bora hata kama ukiamua kuwainamia wabunge maslahi wa CCM. Tunajua kuwa ukiwa upande wetu, tutapata katiba yetu mpya kwa njia iliyonyooka, bila ya mtanzania yeyote kutolewa jicho, au kuvunjwa mguu au mkono. Sisi Watanzania tunataka tupate katiba mpya iliyo bora huku tukiwa wamoja na tunaopendana, na uzinduzi wake usherehekewe na kila Mtanzania kwa kuamini ni katiba inayozingatia haki za kila mmoja wetu.
RAIS UWE NA NGUVU KATIKA HILI MAANA NYUMA YAKO KUNA MAMILIONI YA WATANZANIA WANAOKUUNGA MKONO.
 
Ndugu wapendwa kama una mgonjwa mpeleke TMJ, REagecy, Aghakan ukiulizwa malipo toa kadi ya ccm huduma itakuwa kama ya muhimbili chama chetu kitalipa tofaouti. Tunza risiti yako ukaikabidhi shinani kwako.

CCM oyeeeeeeeeeeeeeeee
 
Back
Top Bottom