JK: mauaji ya mchungaji Geita ni fedheha!

JK: mauaji ya mchungaji Geita ni fedheha!

Katika hili watanzania wenzangu tusikubari kuburuzwa na mtu yeyote! Tusimame kama taifa moja, ndugu moja na familia moja . Watanzania tumechangamana sana, hakuna familia au ukoo usiokuwa na waislam au wakristo au kuoleana au ujirani na urafiki pia. Hili suala tusikubari hata siku moja litugawe, ndugu zangu wanaJF nmekuwa nikiangalia post mbali mbali hapa zikipostiwa cha ajabu watu wengine wanaangalia ubinafsi zaidi kuliko kuangalia utaifa. Kwa hili hebu ndugu zangu tujaribu kuangalia wadogo zetu, watoto wetu, baba zetu, mama zetu, babu zetu, bibi zetu nk nk. Si busara kushabikia mauwaji eti tu tunashabikia dini zetu, hebu suara la imani zetu libakie kwetu kama sisi na imani zetu tusikwazane kwa masuala ya imani ndugu zangu. Viongozi wa dini mbali mbali, viongozi wa kada mbali mbali tafadharini kama ni tunalipenda taifa letu kwa dhati tuhubiri kutokomeza mauaji haya na kwa umoja wetu bila kuangalia itikadi zetu tulaani kwa pamoja mauaji haya yasipate kurudia tena. Imani yangu ni kwamba hakua sehemu kwenye quran au biblia inaporuhusu kuchinjana! Narudia tena ndugu zangu hapa tulipofikia tuseme kwa pamoja kuwa inatosha na tusikubari kamwe kutumiwa na watu wanaotafuta umaarufu aidha kidini au kisiasa! Si utamaduni wetu watanzania huu.

Asanteni na samahani kwa kuchukua muda wenu.

kuna aliyesoma mwanzo-mwisho hapa?..... Mi nmeshindwa!
 
Sidhani kama kuna kiongozi wa CCM ambaye anaweza kuwa "Firm" kwa hili kwani ni wao wamelikuza.Mara nyingi viongozi wetu wamekuwa wepesi wakuwaambia wananchi chama fulani kuna mlengo wa dini fulani na chama hiki kinamlengo wa kabila fulani,sasa hawawezi kuja tena kuwagombeza hao wanaowatia hasira.

Mwanza kuna mtu kwa jina la Ustaadhi Ilunga huyu yuko busy kukashfu wakristu na kuhamasihsa waislamu waue wakristu,wakianzia na viongozi wa wakristu,na kwa namna yoyote ile na wakisha fanya uhalifu ruksa kukimbia ,Je,serikali mkoa wa Mwanza imehama?Kwa nini huyu asifunguliwe mashitaka ya kuhamasisha dini moja kuua watu wa dini nyingine?

Serikali ikianza kukemea ni sawa na kurudia matapishi yake.Viongozi wawe wakali kwenye jumuia za kidini hasa zile zinazohamasisha vurugu,pili viongozi waache sasa kusema uongo juu ya vyama vya upinzani na atakaye endelea basi achukuliwe hatua za kisheria na hii itakomesha haya yote.

Hata wale wanaofanya misikiti au makanisa mahali pao pa kufanyia siasa waonywe na wakiendelea sheria ichukue nafasi,tumechoka na haya ya udini.
 
Nina mashaka na ukristo wako

Wala usiwe na shaka na ukristo wangu, ungekuwa na shaka kama ningesema nikifa nitaenda mbiguni kwa imani hiyo niliyoieleza. Inawezekana hicho ndicho kikwazo changu. Ninakushauri utafakari zaidi na unisahihishe, mimi ni mwafunzi mtiifu.
 
Inabidi rais apunguziwe majukumu,mtwara wakiandamana rais,kuchinja ,,rais,,madaktari kuandamana ,,,rais,,maandamano ya wapinzani ,,rais,,,
mawaziri,wakuu wa mikoa,wakuu wa wilaya,wakuu wa polisi wana kazi gani kama kila kitu atupiwe rais,,
tushajua udhaifu wa rais wetu kuwa yupo slow kwa kuwa ni flagmatic,,basi tuwakomalie mawaziri wake,,mbona akina mwakyembe,maghufuli wanafanya vizuri na hakuna tatizo lolote.
 
Nimekuwa nikifuatilia mjadala huu kwa muda mrefu, lakini nimekuwa nikishangazwa na maoni ya watu wengi kuhusu suala la nani achinje. Mimi ni mkristu mtiifu na kusema kweli nimerithi kutoka kwa baba yangu miaka mingi iliyopita. Jirani zangu ni waislam watiifu kwa imani yao tumeishi kwa uwelewano mkubwa tangu enzi hizo hadi sasa. Wamekuwa wakila kwetu nasi tukila kwao bila mashaka. Kutokana na muungiliano huo, sisi kila tulipoamua kuchinja mbuzi au kuku tumekuwa tukitafuta huduma hii kwenye familia ya kiislam. Na ujira wa kuchinja unaeleweka kwa yule mchinjaji ni sehemu ya nyama ya shingo. Kuamua waislam wachinje kulitokana na ustaarabu wa kutaka kutowanyima kitoweo ndugu zetu kwa maana inamani zao zinaelekeza mashart fulani yafuatwe.

kwa mtu anaye fanya biashara ya kuuza nyama, kuchinjiwa na muisalam mnyama wake ni kupanua soko kuwa wanunuzi wawe wengi. Kwa mtu asiyefanya biashara ya nyama na anamchinja mnyama wake nani achinje ni hiari yake. lakini kama unamuingiliano na waisalam na wanaweza kuja kupata mlo kwako, kuchinja kinyume na matakwa yao ni ushenzi, au ni kinyume cha ustaarabu.

Wakristu lazima tukubali kuwa kama nyama ni kwa ajili ya biashara, mchinjaji lazima awe muislam na hilo lisiwe na mjadala. Lakini mkristu atakae chinja na kupeleka nyama hiyo kwenye bucha la jumla/umma ni mharifu. Adhabu yake sio kukata mapanga na kumuua. Atakaye ua binadamu mwenzie sio muislam bali ni mharifu achukuliwe hatua za kisheria.

Wakristu hatuna sababu ya kulitumia hili la kuchinja kama chanzo cha kutetea imani yetu, hata hivyo hakuna amri ya Mungu hata moja inayosema, muumini ataingia mbinguni kwa kuwa aliwahi kuchinja mnyama kwa mikono yake. Tuachane na ukorofi usio na tija.

Kwa hiyo una maana kila nyama inayochinjwa lazima muislamu ale? Kwani mi nikichinja na kuweka bango imechinjwa na wakristo au nikauzia kanisani wao inawakera nini! si waipotezee kwa sababu kwao ni haramu! Halafu hizi nyama tunazonunua kwenye mabucha nyingine zikiwa ni za ng'ombe wa wizi wanaochinjwa maporini usiku wa manane unaweza kujua kama zimechinjwa na muislamu au la? Na sidhani kama inshu ni kuchinjwa tu na muislamu,kwangu mimi nadhani ni kuchinja kiislamu. Unaweza kuta mchinjaji ni muislamu jina akachinja tu bila kufuata utaratibu wa kiislamu hapo hiyo nyama it is as good as ile iliyochinjwa na mtu mwingine yeyote!
 
  • Thanks
Reactions: JGG
labda hujamuelewa pitia upya maelezo sio kukurupuka na kuleta uzi.walitakiwa kukamatwa sio watu ni hewa.kwenye ukweli tuwe wakweli
 
Wewe ukristo wako ni wa kurithi kama ulivyo sema lkn hujauamini ukristo, maana kama ungekuwa umeuamini usingeandika hayo uliyoandika.
 
Hizi vurugu azikuanza jana! viongozi wa serikali ya leo awana maono kwani kila dalili zilikwisha onekana kuwa siku moja umwagaji damu utatokea,lakini kwa wendawazimu wao wakaliona si tishio.baada ya haya yote kutokea wanaanza kulalama kuwatafuta wauaji wakati wanawajua.mkuu wa mkoa wa mwanza alikuwa mtu wa kwanza kupuuzia dalili za vita ya udini,alikwenda sehemu ya tukio badala ya kutuliza wananchi na kuwaelimisha kwa lugha ya kueleweka yeyealianza kutumia mabavu na kejeri kwa cheo chake.AIWEZEKANI JAMBO ZITO KAMA HILO LINALOGUSA IMANI YA WATU MKALITATUA KISIASA.itawachukua muda sana kama mbinu za kukabiliana na mambo kama haya azitabadilishwa na viongozi kutenganisha siasa na mambo ya dini(imani),na mazoeha wanayo yaona ni msingi wa utatuzi.
 
Kwani yeye aliwatuma wakamuue!!Si wameamua wenyewe na akili zao zilivowatuma

Mimi nakubaliana na wewe kuwa hakuwatuma, ni wazimu wao tu. lkn Hebu kumbuka wkt wa vurugu za mabucha ya Nuguruwe pale Mwembechai Dar, Rais Mwinyi alitoa kauli ambayo ilitengua maamuzi yote na ushabiki wote uliosababisha vurugu zile, kwa kuwaambia watanzania kuwa kila mtu anaruhusiwa kula anachojisikia ili maradi havunji sheria yoyote ya nchi. Rais Kikwete a nashindwa nini kutoa msimamo wake na kuruhusu wananchi waishi kwa Imani zao bila kuvunjwa sheria? Nadhani hapo pana tatizo ambalo lonawafanya baadhi ya wananchi kudhani na kuamini kuwa hawatendewi haki. Kusema tu watu waishi Kama walivyokuwa wakiishi mwanzo hakutoshi kwa sababu tayari kuna maagizo ya viongozi wateule wake ambayo yanaagiza watu waishi kwa utaratibu usio wa mwanzo Kama anavyosema Rais
 
Hivi wale waliomuua Padri kule zanzibari walishakamatwa?
Na wale waliomtesa Docta Ulimboka vipi wamekamatwa?
Je waliochoma makanisa hivi walikamatwa!, na kama walikamatwa wamechukuliwa hatua gani?
Je waliochoma makanisa mbagala hivi walikamatwa! Na je walichukuliwa hatua gani?
Ukweli unabaki pale pale serikali iko nyuma ya waislamu wanafanya haya matuukio! Na tumeshazoea matamko yanayotolewa na Jk mara nyingi yanakosa mshiko ni yakawaida sana.
Hatuoni akichukizwa na hivi vitendo vinavyoshamira sana wakati huu wa serikali yake,
hatuoni kiongozi anaeweza kuongea wananchi wakamsikia!
Amekua akiogopapa upande mwingine watamfikiriaje!.
Nakumbuka mwalimu Nyerere alikuwa hang'ati na kupuliza ila jk anang'ata na kupuliza..
Amekuwa akimtumia waziri DHAIFU wasira kwenda kusuluhisha wa kristo na waislam kule geita! Matokeo yake tumeyaona.
Tusubiri tuendelee kusikia matamko thaifu yasiyo na mshiko ya huyu mr maendeleo.
Kweli raia anazungumza tu ili aonekane yupo lakini haaminiki kasababu hakuna hatua au utekelezaji wa anyoyasema. Polisi walipoua raia wasiokuwa na hatia kule Arusha alisema ilikuwa ni 'very unfortunate' na akasema hayatatokea tena. La ajbu polisi waliendelea kuua raia wasiokuwa na hatia kule Songea, Mororgoro, Iringa na sehemu nyingine na akawa kimya! Lakini ni ukweli kuwa mbegu ya udini imepandwa katika utawala wake naye ameitumia kama mtaji wa kisiasa. Sasa hivi chama chake kinahubiri ukabila na ukanda amenyamaza tu akiwaangalia kina Nape wakiipanda mbegu hiyo. Itakapoota na kutoa matunda atainuka na kulalama wakati anatakiwa kuwakemea na kuwachukulia hatua Nape na Kundi lake sasa.
 
Kwa hiyo una maana kila nyama inayochinjwa lazima muislamu ale? Kwani mi nikichinja na kuweka bango imechinjwa na wakristo au nikauzia kanisani wao inawakera nini! si waipotezee kwa sababu kwao ni haramu! Halafu hizi nyama tunazonunua kwenye mabucha nyingine zikiwa ni za ng'ombe wa wizi wanaochinjwa maporini usiku wa manane unaweza kujua kama zimechinjwa na muislamu au la? Na sidhani kama inshu ni kuchinjwa tu na muislamu,kwangu mimi nadhani ni kuchinja kiislamu. Unaweza kuta mchinjaji ni muislamu jina akachinja tu bila kufuata utaratibu wa kiislamu hapo hiyo nyama it is as good as ile iliyochinjwa na mtu mwingine yeyote!

Ninalosema hapa ni moja, kufanya jambo unaloamini kwamba halitamkwaza mtu. Inahitaji mtu kujiamini kuwa kwa vigezo vyovyote wewe haujahusika kufanya jambo kwa nia ya kutatiza imani ya mtu. Sitetei tabia ya watu kujichukulia hatua ya kuuwa wenzao, ndio maana nikasema hao ni wauaji wanastahili kuchukuliwa hatua bila ya kuhusisa madhehebu yao. Hayo ni mauaji na sheria ziko wazi.
 
Mimi nadhani kuwa na raisi kama Kikwete ndio fedheha kubwa kwa taifa letu.

Mhhmm! Kuliko kutoa roho ya mtu kwa sababu za kupuuzi? Ingekatwa Shingo ya mama, baba, mdogo au mwana ungesema hayo? Hivi wewe ni great thinker kweli?:confused2:
 
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete amesema mauaji ya mchungaji yaliyosababishwa na waislam wa buseresere mkoani Geita ni fedheha, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wapya wa CC JK alisema wale wote waliohusika na mauwaji hayo watasakwa hadi wapatikane.

Tatizo lilikuwa la kujadili baina ya wanandugu wawili - mkristu na muislam - lakini ukifuatilia kiini unaona udhaifu mkubwa wa viongozi walioteuliwa na JK - huenda walikuwa na ajenda ya siri. Wao badala ya kukaa na kulitafutia ufumbuzi wanakwenda na polisi kusweka watu ndani. Mbegu ya udini imepandikizwa wazi wazi katika awamu hii na JK asitafute mchawi nje ya serikali yake na chama chake. Huwezi kuotesha mahindi ukavuna mpunga
 
Mimi nakubaliana na wewe kuwa hakuwatuma, ni wazimu wao tu. lkn Hebu kumbuka wkt wa vurugu za mabucha ya Nuguruwe pale Mwembechai Dar, Rais Mwinyi alitoa kauli ambayo ilitengua maamuzi yote na ushabiki wote uliosababisha vurugu zile, kwa kuwaambia watanzania kuwa kila mtu anaruhusiwa kula anachojisikia ili maradi havunji sheria yoyote ya nchi. Rais Kikwete a nashindwa nini kutoa msimamo wake na kuruhusu wananchi waishi kwa Imani zao bila kuvunjwa sheria? Nadhani hapo pana tatizo ambalo lonawafanya baadhi ya wananchi kudhani na kuamini kuwa hawatendewi haki. Kusema tu watu waishi Kama walivyokuwa wakiishi mwanzo hakutoshi kwa sababu tayari kuna maagizo ya viongozi wateule wake ambayo yanaagiza watu waishi kwa utaratibu usio wa mwanzo Kama anavyosema Rais
Hapo kwenye red kama una uhakika hao viongozi wateule ndo wametoa maagizo yanayovunja amani basi hapo ndio kuna tatizo..Na raisi anawajibika kwa hilo kwa kuwa hao ni wateule wake.
 
Nimekuwa nikifuatilia mjadala huu kwa muda mrefu, lakini nimekuwa nikishangazwa na maoni ya watu wengi kuhusu suala la nani achinje. Mimi ni mkristu mtiifu na kusema kweli nimerithi kutoka kwa baba yangu miaka mingi iliyopita. Jirani zangu ni waislam watiifu kwa imani yao tumeishi kwa uwelewano mkubwa tangu enzi hizo hadi sasa. Wamekuwa wakila kwetu nasi tukila kwao bila mashaka. Kutokana na muungiliano huo, sisi kila tulipoamua kuchinja mbuzi au kuku tumekuwa tukitafuta huduma hii kwenye familia ya kiislam. Na ujira wa kuchinja unaeleweka kwa yule mchinjaji ni sehemu ya nyama ya shingo. Kuamua waislam wachinje kulitokana na ustaarabu wa kutaka kutowanyima kitoweo ndugu zetu kwa maana inamani zao zinaelekeza mashart fulani yafuatwe.

kwa mtu anaye fanya biashara ya kuuza nyama, kuchinjiwa na muisalam mnyama wake ni kupanua soko kuwa wanunuzi wawe wengi. Kwa mtu asiyefanya biashara ya nyama na anamchinja mnyama wake nani achinje ni hiari yake. lakini kama unamuingiliano na waisalam na wanaweza kuja kupata mlo kwako, kuchinja kinyume na matakwa yao ni ushenzi, au ni kinyume cha ustaarabu.

Wakristu lazima tukubali kuwa kama nyama ni kwa ajili ya biashara, mchinjaji lazima awe muislam na hilo lisiwe na mjadala. Lakini mkristu atakae chinja na kupeleka nyama hiyo kwenye bucha la jumla/umma ni mharifu. Adhabu yake sio kukata mapanga na kumuua. Atakaye ua binadamu mwenzie sio muislam bali ni mharifu achukuliwe hatua za kisheria.

Wakristu hatuna sababu ya kulitumia hili la kuchinja kama chanzo cha kutetea imani yetu, hata hivyo hakuna amri ya Mungu hata moja inayosema, muumini ataingia mbinguni kwa kuwa aliwahi kuchinja mnyama kwa mikono yake. Tuachane na ukorofi usio na tija.

Mkuu, nimeupenda sana mchango wako. Kweli, kwani zamani ilikuwaje? kwanini tugombee kuchinja wanyama? kama imani ya waislamu mnyama lazima achinjwe kwa taratibu zao hakuna tatizo, na iwapo mkristo anakula kitoweo kilichochinjwa na muislam na hadhuriki, tatizo ni nini sasa? Mkristo akijichinjia nyumbani kwake for his consumption hakuna tatizo pia, ila kwa undugu na ustaarabu tuliojijengea kati yetu si sawa labda kama wewe ni mchoyo, maana utawanyima jirani na ndg zako walio waislam kula nyumbani kwako.

Watanzania tupendane!
 
Raisi Jakaya Mrisho Kikwete amesema mauaji ya mchungaji yaliyosababishwa na waislam wa buseresere mkoani Geita ni fedheha, akizungumza wakati wa kuwatambulisha wajumbe wapya wa CC JK alisema wale wote waliohusika na mauwaji hayo watasakwa hadi wapatikane.
Hakika ni fedheha na imetia doa serikali na nchi kwa ujumla.
 
Ili tupate nini sasa? Do we understand well the christianity teachings in the holy bible? Kuacha kuchinja...is it something too much to allow? Kuacha malumbano kwenye issue kama hizo kunatugharimu nini? Hatuna mambo muhimu ya kufanya tuanze kugombania kuchinja wanyama?

Kila tatizo lazima lipatiwe ufumbuzi.Kuacha tatizo lijitatue lenyewe ni kutengeneza Bomu jingine.siku nyingine watakuja na jambo jingine utawaachia?Ukweli lazima ubaki kuwa ukweli.kama wana haki tujue ukweli, kama hawana haki tujue ukweli ,then tupige mstari wa suluhisho.Ili watakaopotosha wasulubiwe.Lisije kutokea tena mbeleni.
 
Wewe ukristo wako ni wa kurithi kama ulivyo sema lkn hujauamini ukristo, maana kama ungekuwa umeuamini usingeandika hayo uliyoandika.

Unalotaka kuaminisha watu sio sahihi, ukristo uko wazi kuwa " hatutahukumiwa kwa kundi", "kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe". Msalaba wako, uko katika amri kumi za Mungu. Na katika amri hizo hakuna ndogo na hakuna kubwa, zinatakiwa kutimizwa kwa ukamilifu wake na kwa ujumla wake. Katika amri hizo kumi hakuna ya "kuchinja au kutochinja mnyama". Jumuisho la amri hizo kumi ni "Upendo" na "uchaji Mungu wetu",usiokuwa na shaka na wala masharti. Kurithi au tafuta mwenyewe hakupo hapa.

Ukiamua kumkosoa mtu onesha eneo au neno au sentensi iliyokosewa au iliyotumiwa vibaya. Useme jumla jumla tu, hutamsaidia mtu.
 
Back
Top Bottom