Luteni
JF-Expert Member
- Jan 9, 2010
- 2,274
- 302
CHUO Kikuu cha Fatih cha nchini Uturuki kinatarajiwa kumtunuku Rais Jakaya Kikwete, Shahada ya Uzamivu (PhD) ya heshima, imefahamika.
Ikulu, Dar es Salaam imesema, Rais Kikwete anaondoka leo nchini kwenda Uturuki na pia atakwenda Jordan, kwa ziara rasmi za kiserikali kwa mwaliko wa viongozi wa nchi hizo.
Rais Kikwete anafuatana na mkewe, Mama Salma, pamoja na wafanyabiashara wa Tanzania.
Atafanya ziara ya siku tatu nchini Uturuki kwa mwaliko wa Rais Abdallah Gul.
Alipokea na kukubali mwaliko wa kuitembelea Uturuki Februari mwaka jana wakati Rais Gul alipotembelea nchini kwa mwaliko wa Rais Kikwete.
Atakapokuwa Uturuki, Rais Kikwete atazungumza na mwenyeji wake na pia kukutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan.
Rais Kikwete pia anatarajiwa kuzungumza na viongozi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Uturuki na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini humo.
Tanzania na Uturuki zinatarajiwa kusaini mikataba sita ya ushirikiano.
Rais anatarajiwa kuondoka Uturuki Jumapili, kwenda Jordan kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Mfalme Abdullah II.
UPDATE:
The Rector of Fatih University in Instabul, Turkey, Professor Shariff Ali confer upon President Jakaya Mrisho Kikwete a honorary Doctorate Degree (Honoris Causa) in International Relations during a colourful ceremony held at Fatih Univesity in Instabul Turkey Friday evening
President Jakaya Mrisho Kikwete prepares to deliver his acceptance speech shortly after he was conferred with Honorary Doctorate Degree in International Relations yesterday at Fatih University, in Instabul, Turkey Friday evening. Photo by Freddy Maro.