JK apata PhD ya International Relations

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
CHUO Kikuu cha Fatih cha nchini Uturuki kinatarajiwa kumtunuku Rais Jakaya Kikwete, Shahada ya Uzamivu (PhD) ya heshima, imefahamika.

Ikulu, Dar es Salaam imesema, Rais Kikwete anaondoka leo nchini kwenda Uturuki na pia atakwenda Jordan, kwa ziara rasmi za kiserikali kwa mwaliko wa viongozi wa nchi hizo.

Rais Kikwete anafuatana na mkewe, Mama Salma, pamoja na wafanyabiashara wa Tanzania.

Atafanya ziara ya siku tatu nchini Uturuki kwa mwaliko wa Rais Abdallah Gul.

Alipokea na kukubali mwaliko wa kuitembelea Uturuki Februari mwaka jana wakati Rais Gul alipotembelea nchini kwa mwaliko wa Rais Kikwete.

Atakapokuwa Uturuki, Rais Kikwete atazungumza na mwenyeji wake na pia kukutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan.

Rais Kikwete pia anatarajiwa kuzungumza na viongozi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Uturuki na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini humo.

Tanzania na Uturuki zinatarajiwa kusaini mikataba sita ya ushirikiano.

Rais anatarajiwa kuondoka Uturuki Jumapili, kwenda Jordan kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Mfalme Abdullah II.

UPDATE:

8e9u6204.jpg

The Rector of Fatih University in Instabul, Turkey, Professor Shariff Ali confer upon President Jakaya Mrisho Kikwete a honorary Doctorate Degree (Honoris Causa) in International Relations during a colourful ceremony held at Fatih Univesity in Instabul Turkey Friday evening

8e9u6205.jpg

President Jakaya Mrisho Kikwete prepares to deliver his acceptance speech shortly after he was conferred with Honorary Doctorate Degree in International Relations yesterday at Fatih University, in Instabul, Turkey Friday evening. Photo by Freddy Maro.

promo tupu siku hizi... wanaweza kumpa hata mwanawe PhD ya kuzaliwa na rais wa tanzania
 
Ndiyo yale yale ya kumpa Obama Nobel prize wakati anaescalate war! Nadhani wampe shahada hiyo na kumpongeza kwa kupambana na ufisadi, kusimamia matumizi ya serikali vizuri n.k
 
Ndiyo yale yale ya kumpa Obama Nobel prize wakati anaescalate war! Nadhani wampe shahada hiyo na kumpongeza kwa kupambana na ufisadi, kusimamia matumizi ya serikali vizuri n.k

Angalau hata Kikwete wanampa baada ya kukaa madarakani miaka zaidi ya minne. Obama alipewa wakati hata mwaka hajafikisha. Kumbuka aliteuliwa mwezi wa pili baada tu ya kula kiapo.....vichekesho mtupu
 
Angalau hata Kikwete wanampa baada ya kukaa madarakani miaka zaidi ya minne. Obama alipewa wakati hata mwaka hajafikisha. Kumbuka aliteuliwa mwezi wa pili baada tu ya kula kiapo.....vichekesho mtupu

acha wivu wa kiume!
 
Upuuzi mtupu... na safari zisizo na tija. Si wangemtumia hicho cheti kwa UPS
 
Angalau hata Kikwete wanampa baada ya kukaa madarakani miaka zaidi ya minne. Obama alipewa wakati hata mwaka hajafikisha. Kumbuka aliteuliwa mwezi wa pili baada tu ya kula kiapo.....vichekesho mtupu

Maelezo waliyotoa ni kwamba uchaguzi na kampeni ya Obama ilibadilisha sura ya Marekani toka dola iliyokuwa ikitishia kuanzisha vita na yeyote asiyekubaliana na mtazamo wake (beligerent state) hadi dola sikivu yenye kutambua na kuheshimu maoni ya wengine. Hivyo, kampeni na kuchaguliwa kwa Obama tu kulitazamwa kama mchango mkubwa sana wa Marekani katika kuimarisha amani ya dunia iliyotiwa hatihati wakati wa utawala wa Bush/Cheney (you are either with us or with our enemies!)
 
promo tupu siku hizi... wanaweza kumpa hata mwanawe PhD ya kuzaliwa na rais wa tanzania

Dr Halifani Kikwete kaazi kweli hizi degree za kupeana sijui kweli unaweza kuwa proud nazo
 
Maelezo waliyotoa ni kwamba uchaguzi na kampeni ya Obama ilibadilisha sura ya Marekani toka dola iliyokuwa ikitishia kuanzisha vita na yeyote asiyekubaliana na mtazamo wake (beligerent state) hadi dola sikivu yenye kutambua na kuheshimu maoni ya wengine. Hivyo, kampeni na kuchaguliwa kwa Obama tu kulitazamwa kama mchango mkubwa sana wa Marekani katika kuimarisha amani ya dunia iliyotiwa hatihati wakati wa utawala wa Bush/Cheney (you are either with us or with our enemies!)

Nonsense
 
Nahitaji elimu hapa. Nilifikiri Ph.D za heshima zinatolewa kwa aliyetoa mchango mkubwa katika utekelezaji wa falsafa fulani mhimu k.m. JKN alivyojitahidi kujenga taifa la kijamaa au Mandela alivyopigania usawa na heshima ya mtu mweusi huko A. Kusini. Sasa hawa Waturuki wanasema nini kuhusu mchango wa JK unaowapelekea kumtunuku shahada hiyo ya uzamivu? Ni muhimu hii iwekwe wazi ili nasi skeptics tumpe heshima yake.
 
Ni mtazamo tu mkuu. Mimi binafsi, kwa jinsi nilivyotahayari enzi za akina Cheney/Rumsfeld, nakiri hoja hii ya Kamati ya Nobel imenichukua kiasi. Ingawa natambua huwezi kuibadilisha marekani toka kwenye mlengo wake halisi.
 
Angalau hata Kikwete wanampa baada ya kukaa madarakani miaka zaidi ya minne. Obama alipewa wakati hata mwaka hajafikisha. Kumbuka aliteuliwa mwezi wa pili baada tu ya kula kiapo.....vichekesho mtupu

Kwani wanampa mtu kwa kukaa madarakani au kwa kufanya kitu cha ziada kama kiongozi?
 
Baada ya hiyo PHD watampa tena nini ? maana yeye na serikali yake yote wapenda vya kupewa tu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom