JK apangua makatibu wakuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK apangua makatibu wakuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mpita Njia, Nov 29, 2008.

 1. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  RAIS Kikwete, amefanya mabadiliko ya makatibu wakuu na naibu katibu wakuu wa wizara 13 na Gray Mgonja wa fedha amekwenda likizo ya kustaafu.

  Makatibu kadhaa na manaibu wamehamishwa na wengine wapya wameteuliwa baada ya wengine kustaafu.

  Mabadiliko hayo yamegusa wizara kadhaa ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Ulinzi, Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki na nyingine tisa.

  Kikwete amewateua wasaidizi wake wawili wa Ikulu kuwa naibu makatibu wakuu wa wizara.

  Alhaj Ramadhan Kijja anakuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Uchumi, Dk Florens Turuka Katibu Mkuu wa Habari Utamaduni na Michezo, Joyce Mapunjo anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara na Andrew Nyumayo anakuwa Katibu Mkuu, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

  Kabla ya uteuzi Kijja alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Uchumi, Dk Turuka alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Joyce Mapunjo alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Miundo Mbinu na Andrew Nyumayo alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu.

  Makatibu wakuu waliohamishwa Wizara ya ni pamoja na Paniel Lyimo aliyekuwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Masoko sasa anakwenda Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk. Ladislaus Komba amehamishiwa Maliasili na Utalii, Kijakazi Mtengwa amepekewa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana na Mohamed Muya amehamishiwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika.

  Awali Dk Ladislaus Komba alikuwa Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Kijakazi Mtengwa alikuwa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ambapo Mohamed Muya alikuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  Makatibu wakuu wengine waliohamishwa ni Patrick Rutabanzibwa amepangiwa Wizara ya Mambo ya Ndani kutoka Maji na Umwagiliaji, Dk Sergomena Tax - Afrika Mashariki akitokea Viwanda, Biashara na Masoko, Wilson Mukama anakwenda Maji na Umwagiliaji kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, pamoja na Blandina Nyoni anayekwenda Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii akitokea Maliasili na Utalii.

  Naibu makatibu wakuu wapya walioteuliwa ni pamoja na Dk. Philip Mpango- Fedha na Uchumi, Celestine Gesimba - Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Seti Kamuhanda - mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

  Dk Mpango alikuwa msaidizi wa rais (Uchumi) Ikulu, Seti Kamuhanda pia alikuwa msaidizi wa rais (Hotuba) Ikulu na Gesimba alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

  Fanuel Mbonde aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI amehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu.

  Makatibu wakuu wengine waliostaafu pamoja na Mgonja ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Vincent Mrisho, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Abel Mwaisumo, Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bakari Mahiza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Charles Sanga.
  Naomba kuwasilisha
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  hivi hii nayo ni BREAKING NEWS?

  kwa nini wasimuunganishe huyo MGONJA kwenye kesi za ufisad au ana legal advisor mzuri?
   
 3. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Safi mkuu,
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  huyu Rutabanzibwa bado wanaye tuuu
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huyo Mgonja wamempunzisha ili ajipange kulala keko.
   
 6. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  This is worse than what that revered Roman poet by the name of Juvenal suggested (bread and circuses).This is just circuses, cheap ones at that, without the bread.
   
 7. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kuna mmoja sijamuona humu au yeye hajaguwa...Charles Nyamurunda
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  This President has a big problem. I can't imagine under the current situation he still entertains deputy ministers, deputy PS (sometimes 2 in a ministry) etc. The size of his inefficient cabinet is already big and thought he would be struggling to reduce it. But now see what he is doing. Still appointing deputy PS(s).
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Nov 29, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Hamna kipya humu
   
 10. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mgonja anaandaliwa kwenda Kisutu.
   
 11. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  It is very hard right now to tell BUT he is struggling to restore the trust we we had upon his Government. Cheers JK from JF
   
 12. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Rutabanzibwa fisadi bado yumo tu, na sasa anakwenda kuonana na Fisadi mwingine MASHA. Mmmh Kikwete una shughuli kaka.
   
 13. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Katibu Mkuu ni technocrat na si mwanasiasa, ni mtu ambaye ni mtaalamu na mahiri katika fani fulani na hivyo huwekwa pale kuwa gurudumu la kuendesha shughuli za wizara.

  Sasa kwenye hii panga pangua, jambo hilo lilifuatwa? je ina maana kuwa makatibu wakuuu wetu ni all weather kuwa anaweza kutoka wizara ya elimu akaenda kuwa katibu mkuu mambo ya ndani? au kutoka wizara ya kilimo na kwenda afya na kuwa fanisi na makini?
   
 14. M

  Mkora JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2008
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu Rev Yaan tupo ukurasa mmoja kabisa sasa PS anahamishwa kama waziri sasa pale wizarani gurudumu atakuwa nani katika fani ile
  Yaan kazi ipo kweli kweli
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Nov 29, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Rev.
  Mkuu muundo zmima wa Utawala wetu ndio kama hivyo... wasomi wetu kina Mwandosya ndio wanasiasa hizo nafasi za Ukatibu mkuu zinakwenda kwa wale waliobakia ambao pia lazima uwe Mwanasiasa!
  Sishani kama kuna katibu mkuu ambaye sii mwana CCM... kwa maana ya Kibongo mwanasiasa..Kwa sababu nafasi za Ubunge ni limited, nje ya hapo tungekuwa na wasomi wote wanasiasa..
  Siku hizi Gurudumu la gari linaweza kuwa Yokohama likachanganywa na mengine General Tyre, Firestone na kadhalika ili mradi yote saizi moja.. mwendo mdundo!
   
 16. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Ama kweli inaelekea kila mtendaji wa Tanzania ni mithili ya marehemu Method "Kiraka" Mogella! Mtoe Ulinzi mpeleke Kilimo atafanya kazi. Mtoe Michezo umpeleke Hazina, uchumi utapaa!
   
 17. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Huu ni uteuzi unaofaa sana kwa taifa, maana huyu sister hana mchezo ni kazi tu I can't wait siku atakapokuja kuwa waziri mkuu, maana mbingu zitashuka.

  Nakumbuka siku moja mkutanoni Paris alivyomshangaza muungwana akiwa waziri, kwa kuiita hoja yake kuhusu uchumi wa bongo kuwa ni nonsense na kwamba anahitaji kwenda kufanya homework, duh! mkulu hakuamini kuwa huyu dada ana huu ubavu!

  Na pia ninakumbuka wakati tunasubiri cabinet ya kwanza ya awamu ya nne kutangazwa, nilimuuliza vipi, akasema baada ya ile ya Paris haamini anaweza kupewa anything, huyu sasa anaondoka kumbe muungwana huheshimu wanaoweza kumpa facts usoni bila uoga.

  Saafi sana sister Joyce wembe ni ule ule kumkoma nyani usoni tu, najua upo hapa respect na nitakutwangia later!
   
 18. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #18
  Nov 29, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Sasa Mkuu FMES huoni kwamba mambo kama haya kama aliyajua kusubiri mpaka Paris ni kuchemsha? Na kwamba serikali ikiwa viwanja huko kunatakiwa collective responsibility?

  Alikuwa wapi wakati mipango hii inapitishwa na kuwa adopted kusubiri mpaka ughaibuni kusema hivi?
   
 19. UramboTabora

  UramboTabora Member

  #19
  Nov 29, 2008
  Joined: Sep 11, 2008
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mgonja wa Hazina aastafu
  Mwandishi Wetu
  Daily News; Saturday,November 29, 2008 @18:01

  Habari nyingine
  Mgonja wa Hazina aastafu
  Wasomi watakiwa kuzingatia utaalamu
  Watuhumiwa wa EPA waripoti Kisutu
  Tanzania yampongeza Balozi wa Japan
  Watatu mbaroni wakitaka kumteka albino
  Katibu Msaidizi CCM Tabora Mjini afariki
  Wahitimu SUA watoa vitanda hospitalini
  Ntimizi awania uenyekiti UWT Tabora
  Hospitali ya Mawenzi yakana kubagua wagonjwa
  Makamba ataka mazuri ya maendeleo yatangazwe

  Mmoja wa makatibu wakuu waliofanya kazi kwa muda mrefu, Gray Mgonja, ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, amestaafu kwa mujibu wa sheria baada ya kutumikia taifa kwa muda mrefu.

  Kutokana na kustaafu kwa Mgonja na wenzake watatu, Rais Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa makatibu wakuu wapya, kuhamisha wengine na kuteua manaibu katibu wakuu wapya. Kwa sasa, Mgonja ambaye yuko katika likizo ya kustaafu, amestaafu sambamba na makatibu wakuu wengine watatu na Naibu Katibu Mkuu mmoja kati ya Agosti na Novemba mwaka huu.

  Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo katika taarifa yake Dar es Salaam jana, aliwataja wastaafu wengine ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Vincent Mrisho, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Abel Mwaisumo, Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bakari Mahiza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Charles Sanga.

  Luhanjo alisema kutokana na kustaafu kwa makatibu wakuu na Naibu Katibu Mkuu huyo, Rais Kikwete amefanya uteuzi na uhamisho wa makatibu wakuu na baadhi ya manaibu makatibu wakuu. Aliwataja makatibu wakuu wapya ambao wote walikuwa ni manaibu katibu mkuu ni Ramadhani Khijjah anayemrithi Mgonja, awali akiwa Naibu Katibu Mkuu Hazina.

  Wengine ni Dk. Florens Turuka anayekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, akitokea Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko; Joyce Mapunjo anayekwenda Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, akitokea Maendeleo ya Miundombinu na Andrew Nyumayo kusimamia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, akitokea Ofisi ya Waziri Mkuu.

  Aliwataja Manaibu Katibu Wakuu wapya kuwa ni Dk. Phillip Mpango (Wizara ya Fedha na Uchumi) ambaye awali alikuwa Msaidizi wa Rais (Uchumi)-Ikulu, Selestine Gesimba (Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi), akitokea Mkurugenzi wa Sera na Mipango ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

  Mwingine ni Seti Kamuhanda anayekwenda Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Awali alikuwa Msaidizi wa Rais (Hotuba) Ikulu; na kabla ya hapo, alikuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), inayochapisha Daily News, Sunday News, HabariLeo na HabariLeo Jumapili.

  Katika uhamisho huo, Luhanjo aliwataja waliohamishwa na sehemu wanazotoka na wizara walizopangiwa katika mabano kuwa Peniel Lyimo (Ofisi ya Waziri Mkuu kutoka Kilimo, Chakula na Ushirika); Dk. Ladislaus Komba (Maliasili na Utalii kutoka Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana) na Kijazi Mtengwa (Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana kutoka Habari, Utamaduni na Michezo.

  Wengine ni Mohammed Muya (Kilimo, Chakula na Ushirika kutoka Mambo ya Ndani; Patrick Rutabanzibwa (Mambo ya Ndani kutoka Maji na Umwagiliaji); Dk. Stergomena Tax (Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka Viwanda, Biashara na Masoko); Wilson Mukama (Maji na Umwagiliaji kutoka Afya na Ustawi wa Jamii); na Blandina Nyoni (Afya na Ustawi wa Jamii kutoka Maliasili na Utalii).

  Aidha, Luhanjo alisema rais amemhamisha Naibu Katibu Mkuu Fanuel Mbonde kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi) kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu. Katibu Mkuu Kiongozi alisema uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu hao unaanza mara moja.
   
 20. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #20
  Nov 29, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  JK Apangua makatibu wakuu = This thread
   
Loading...