JK apangua makatibu wakuu

JK hana washauri wazuri, wakati huu kama angekuwa serious ndio angeutumia kuwaondoa mafisadi wote kwenye safu ya maps!! Lakini wapi bado yupo Patrick Rutabanzibwa na huyo mama Mapunjo ambae amefanya madudu mengi alipokuwa hazina na Mgonja leo nasoma amepandishwa cheo kuwa PS viwanda; tutafika kweli??
 
Kwa Rutabanzibwa kumwita fisadi nadhani ni mapema mno na twaeza mwonea.The man is a fearless fighter wa ufisadi.Alipigana kufa na kupona kupinga mikataba mibovu ya IPTL lakini akazidiwa nguvu na mafisadi.

Binafsi namheshimu kama mtu mwenye msimamo asiyependa rushwa kabisa na wala hana mpango nayo,mchapa kazi na asiyeyumba akiamua kusimamia kitu.labda awe alibadilika hapo katikati maana binadamu aweza geuka awapo safarini akaacha kuangalia mbele aendako akageuka nyuma kukumbatia kusalimiana na kula na mafisadi.

Kwenye kundi la mafisadi walioko sasa Rutabanzibwa nawaza kumtoa.Sina uhakika sana kama niko sahihi au siko sahihi lakini nafikiria nimtoe kichwani mwangu kwenye kundi la mafisadi ninaowawazia.

Huyu ni kati ya watu waliotetea kufa na kupona kampuni ya NETGROUP. Kumwita ni fighter au mtu wa maadili ni kumwonea, kwa sababu siyo! Kwa vigezo pana vya ufisadi, huyu hawezi kukwepa.

By the way, how is this news "breaking"?
 
Inawezekana kweli aliitetea Net Group lakini kwa undani zaidi, ndiye aliyechangia kuwabana hao Net Group na ndiye aliyesaidia hata Watanzania wahafahamu udhaifu wao hata kabla hawajaanza kazi.

Naamini utaelewa (kwa undani zaidi), maana kabla hata kina Huysen wa Net Group hawajatua Dar es Salaam, gazeti la Mtanzania la wakati huo liliandika majina yao na hata wakaweza kupata picha zao pale Airport waliposhuka, usidhani ilikuwa ni bahati mbaya tu waliwaona pale Airport. Kwa ufupi huyu bwana ni mpambanaji.

Kuna wakati alilalamikia serikali kwa kumuuzia nyumba ambayo serikali iliikarabati kwa gharama kubwa zaidi kabla ya kuiuza.
 
Halisi

Jamani mi namempenda Pat alipambana sana kwenye kashfa ya IPTL, alikataa rushwa wazi wazi. Lakini naona CHADEMA wamemtaja kwenye orodha ya mafisadi. Je, ni kutokana na kuwa mkurugenzi wa TANGOLD iliyoiba fedha za umma? Sasa kwa nini hakupambana kupinga huo ufisadi? Kwa nini alikaa kimya na mpaka leo anaficha ufisadi huo?

Baada ya kutajwa kwenye list of shame alisema atakwenda mahakamani, mbona hajaenda?

Asha
 
Kufuatana na barua ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu, Gavana Balali aliruhusu na/au kuidhinisha na/au kunyamazia malipo ya Dola za Marekani 13,736,628.73 kwa kampuni ya Tangold Ltd. Katika hotuba yake Bungeni ya tarehe 27 Juni 2007, Waziri wa Madini na Nishati Mheshimiwa Nazir Karamagi alidai kwamba “… mali na madeni ya MEREMETA yamehamishiwa kwenye kampuni mpya ya TANGOLD ambayo inamilikiwa na Serikali kwa asilimia mia moja.” Hata hivyo, barua ya BRELA ya tarehe 4 Julai 2007 inatamka wazi kwamba “Tangold Limited ni kampuni ya kigeni iliyosajiliwa kwa mara ya kwanza nchini Jamhuri ya Mauritius, na baadae kuandikishwa nchini Tanzania kama tawi la kampuni ya kigeni.” Barua hiyo inaongeza kwamba kampuni hiyo ilipewa hati ya kutimiza masharti ya Tanzania mnamo tarehe 20 Februari 2006 na kwamba Katiba ya kampuni hiyo haikuonyesha “majina ya wanahisa wa kampuni na mgawanyo wa hisa.” Barua hiyo ya BRELA inaonyesha kwamba wakurugenzi wa Tangold Limited ni pamoja na Gavana Balali, Gray S. Mgonja ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Andrew J. Chenge ambaye ni Waziri wa sasa wa Miundo Mbinu, Patrick W.R. Rutabanzibwa ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Vincent F. Mrisho ambaye ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu. Aidha fomu Na. 1F inayohusu usajili wa kampuni za kigeni iliyowasilishwa BRELA na mawakili wa Tangold Limited na kusainiwa na Gavana Balali tarehe 20 Mei 2005 inaonyesha kwamba kampuni hii imetokea “Jamhuri ya Mauritius” na anwani yake iko Suite 520, Barkly Wharf, Le Caudan, Waterfront, Port Louis, Mauritius. Hivyo ndivyo kinavyoonyesha cheti cha usajili kilichotolewa na Msajili wa Makampuni wa Jamhuri ya Mauritius mnamo tarehe 5 Aprili 2005 na pia leseni ya biashara iliyotolewa kwa Tangold Ltd. Port Louis nchini Mauritius tarehe 8 Aprili 2005. nyaraka hizi pia zinaonyesha kwamba Tangold Limited ni kampuni binafsi (private company limited by shares). Kuna utata zaidi kwani kifungu cha 7(e) cha Katiba ya Tangold Ltd. kinaruhusu hisa za wanaomiliki kampuni hiyo binafsi kuhamisha hisa zao kwa wanandoa, baba, mama, watoto, wajukuu au wakwe zao wa kike au wa kiume! Sasa kama ni kweli kwamba Tangold Ltd. inamilikiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia mia moja, je nani ni mke au mume au baba au mama au motto au mjukuu au mkwe wa kike au wa kiume wa Serikali ya Tanzania ambaye anaweza kuhamishiwa hisa za kampuni hiyo? Katika barua yake ya ukaguzi, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu alidai kwamba Ofisi yake ilishindwa kuelewa uhalali wa malipo ya dola za Marekani 13,340,168.37 yaliyofanywa na Benki Kuu kwa Tangold Limited;
 
Kumuweka Dr. Turuka pale Utamaduni na michezo ni matusi kwa elimu ya huyu mtu.......similar to what happened to Mh Sarungi........hivi hawa washauri wa JK wanaangalia kweli CV za watu au basi tu ili kumpandisha mtu cheo.........!!
 
- Wananchi angalieni another scenario inayotembea mjini leo sina uhakika na ukweli wake, inasema hivi:-
kulikuwa na vikao vya siri vya kamati za el kugombea urais vilivyokuwa vikifanyika katika hotel ya mzee mmoja mjini anayeitwa Msiba. vikao hivyo vilikuwa vikiongozwa na mramba. na leo mtoto wa mramba ameolewa na mtoto wa huyo msiba. kwamba harakati zimewaka moto za 2010 kwa sababu makubaliano ya mtandao yalikua muungwana atawale term moja tu amuachie el lakini sasa anaonekana kukiuka makubaliano.

Hivi kuna ajabu gani watu ambao watoto wao wanataka kuooana kufanya vikao? Wote tunajua toka kutuma posa hadi harusi ni lazima vikao kibao vipite. Hata kabla ya hivyo kuna vikao vya kutambulishana ndugu, kujadili mahari na gharama nyingine. Mimi, hii habari naitilia shaka.
 
Inawezekana kweli aliitetea Net Group lakini kwa undani zaidi, ndiye aliyechangia kuwabana hao Net Group na ndiye aliyesaidia hata Watanzania wahafahamu udhaifu wao hata kabla hawajaanza kazi.

Naamini utaelewa (kwa undani zaidi), maana kabla hata kina Huysen wa Net Group hawajatua Dar es Salaam, gazeti la Mtanzania la wakati huo liliandika majina yao na hata wakaweza kupata picha zao pale Airport waliposhuka, usidhani ilikuwa ni bahati mbaya tu waliwaona pale Airport. Kwa ufupi huyu bwana ni mpambanaji.

Kuna wakati alilalamikia serikali kwa kumuuzia nyumba ambayo serikali iliikarabati kwa gharama kubwa zaidi kabla ya kuiuza.

Angeaminika zaidi kama angekataa kununua hiyo nyumba badala ya kulalamika tu. Hiyo nyumba hata hivyo isingeweza kufanyiwa ukarabati huo bila yeye mwenyewe kujua maana yaye ndie accounting officer wa wizara. Utetezi huu una walakin!
 
Hivi kuna ajabu gani watu ambao watoto wao wanataka kuooana kufanya vikao? Wote tunajua toka kutuma posa hadi harusi ni lazima vikao kibao vipite. Hata kabla ya hivyo kuna vikao vya kutambulishana ndugu, kujadili mahari na gharama nyingine. Mimi, hii habari naitilia shaka.

Quote:- FMES

- Wananchi angalieni another scenario inayotembea mjini leo sina uhakika na ukweli wake, inasema hivi:-

- Na besides vikao vilikuwa ni vya urais wa EL sio harusi, sio tatizo kujitilia shaka kama hujaielewa habari ambayo tayari imesemwa kuwa sio ya uhakika.
 
Quote:- FMES

- Wananchi angalieni another scenario inayotembea mjini leo sina uhakika na ukweli wake, inasema hivi:-

1. Mimi, hii habari naitilia shaka.

2. Sasa tatizo liko wapi? Si uliishasema kuwa habari hauna hakika nayo? Au kosa ni Fundi Mchundo ku-comment?

Lol!
 
FMeS. Mbona unataka kuharibu jamvi tena? Kwenye post yangu ya mwanzo si nili-bold uliposema kuwa una shaka na habari yenyewe?

- Wananchi angalieni another scenario inayotembea mjini leo sina uhakika na ukweli wake, inasema hivi:-

Sikusema kuwa hii habari umeileta kama dataz. Ila nilichomaanisha ni kuwa hata mimi nina shaka na habari yenyewe.

Sasa tatizo liko wapi? Hivi unafurahi kila kukicha tuwe tunatoa sinema ya bure kwa malumbano yasiyo na kichwa wala miguu?
 
Katika mchuano na mpambano huu wa hoja hapa JF naona kati ya kina Mchundo na FMES bado umo...Ila naona FMES amebadili tactics kwa ghafla na hivyo kumchanganya Fundi Mchundo kiaina..At least kwa wakati huu...Kwasababu FMES alishasema habari isiyokuwa na uhakika, na FM akaikosoa habari hiyo bila kutilia maanani kauli ya mwanzo ya habari hiyo kutokuwa na uhakika.
All in all hapa JF tuna uwezo wa kusoma katikati ya mistari na kwahiyo mambo hayawezi kuharibika provided tunaeleweshana pasi na matusi.
 
Lakini kaka kuna watu humu ndani wamezidii, utadhani mtu anakaa siku nzima kuangalia kama fulani kaandika kitu ili apinge, yaani badala ya kupinga na hoja anachambua maneno, kwamba hili neno au hili hayajakaa vizuri yaani utadhani mwanasheria ambaye anataka kushinda kesi kwa kupindisha maneno, na mara nyingine huwa hawaangalii maneno yaliyoandikwa na kuanza kubisha upuuzi, kama hapo mtu kashasema na yeye hana uhakika lakini bado wanataka kumhukumu na maneno yake (utadhani sio watu wenye akili zao na kuweza kuchambua kilichoandikwa). Wanakuwa kama watoto sasa.
 
...

- Muungwana alikuwa foreign huyu sister alikua Hazina, kwa kawaida foreign huwa wanaamini wanajua sana kuliko sekta zote za serikali bongo, kwa hiyo huwa hawakubali ushauri wa mtu yoyote, ndio maana huyu sister aliamua kumtolea uvivu bosi wao huko huko majuu.
...

mkuu naona hapa huwatendei haki foreign. naamini mara nyingi nasisitiza "mara nyingi" watu wa sekta nyingine za serikali ndio wanapenda kuwaona wizara ya mambo ya nje "wanaamini wanajua sana". lakini hili linaweza kujadiliwa kwenye thread ya peke yake.

pamoja na yote kuna mdau hapo juu ameuliza huyu mama mapunjo si wa longi hapo hazina? hivi madudu yote yaliyokuwa yanafanyika hapo hakuwahi kuyaona na kuwatolea uvivu akina mgonja kama alivyomtolea uvivu jk?
 
1.

- Kwenye hilo ninaongea na authority kubwa sana kwa sababu nimeshwahi kutoa mifano mingi sana, kwamba ni foreign ndio wenye problem, ukitafuta michngo yangu nyuma utaona jinsi kivumbi kilichotokea kuhusu houtba ya Mama Salma recently pale UN.

2.

- Bosi wa hazina alikuwa another friend of mine sister Blandina you know that, Joyce alikuwa ni mtu mdogo sana, ndio maana hata muungwana alishangazwa na ujasiri aliokuwa nao kumjibu vile na mpaka leo anamheshimu kuliko na hakuna kiongozi mkuu wa serikali asiyejua umakini wa huyu sisiter inapokuja ishus muhimu za uchumi na taifa letu, na huwa haogopi, lakini hakuwahi kuwa kwenye position yoyote ya kumuhusisha na unayoyasema, au?
 
japokuwa nami siwezi kusema naongea kwa authority kubwa sana naamini nayafahamu mengi yanayotokea foreign ingawa mara nyingi sichangii hususan pale ninapoona wengine wamekwisha changia yale niliyotaka yachangia. pia kunawakati wawakilishi wa sekta nyingine wamekwama kwenye shughuli nyingine hususan pale walipoona mchango wa foreign sio muhimu.

ninachotaka kusema hapa ni kwamba foreign watakosea sana watakapojiona wao ni muhimu kuliko wizara mama inayohusika na issue na hali kadhalika wizara mama zitakosea zitakapoona foreing wanajidai wanajua hivyo kuwakwepa. muhimu ni ushirikiano.

2.

- Bosi wa hazina alikuwa another friend of mine sister Blandina you know that, Joyce alikuwa ni mtu mdogo sana, ndio maana hata muungwana alishangazwa na ujasiri aliokuwa nao kumjibu vile na mpaka leo anamheshimu kuliko na hakuna kiongozi mkuu wa serikali asiyejua umakini wa huyu sisiter inapokuja ishus muhimu za uchumi na taifa letu, na huwa haogopi, lakini hakuwahi kuwa kwenye position yoyote ya kumuhusisha na unayoyasema, au?

sijamhusisha huyo dada na mabaya yoyote isipokuwa nilikuwa nauliza kama alikuwa anaubavu wa kumpa ukweli jk (jambo ambalo ni zuri na anastahili pongezi), je aliwahi kuwapa ukweli wakuu wake wa kazi? kama sikosei dada huyo alishawahi kuwa idara inayohusika pia na pesa za nje pale hazina na hakuwa mtu mdogo sana je huko alikokuwa mambo yalikuwa shwari? au aliwahi kupiga kelele lakini kwa vile alikuwa mtu "mdogo" sauti yake haikusikika.
 
Back
Top Bottom