JK amteua Jaji Kiongozi mpya

Kwa nini JK ateue karibu kila mtu???

hakuna vyombo vingine vya kuteua?


Ndiyo maana Mahakama hutoa hukumu hata saa 8 za usiku iwapo Serikali ina manufaa! Si wakumbuka hukumu ya Mahakama ya KAzi dhidi ya mgomo wa Walimu? Kuna Mwanazuoni mmoja mashuhuri alishangazwa hukumu kutolewa baada ya saa za kazi tena usiku!
 
Bado mpo.. I'm so done. Mambo mengine ninawaachia muendelee. Next.

Mzee Mwanakijiji, sioni sababu ya watu kukushambulia kiasi hiki. Naamini wamekereka na ukweli uliowazi katika mada yako. Ikumbukwe kuwa ulichosema ni kuhusu uteuzi wa Jundu na ukweli kuwa hakukulia mahakamani na kwamba tangu ameteuliwa kuwa Jaji hana muda mrefu. Masuala ya dini yake hukuyaanzisha wewe na anayejaribu kukuita mwongo lazima ana lake jambo. Tatizo letu wanaJF tunashindwa kuapreciate information na tunajaribu kuficha uozo wetu kwa kukosoa vitu vidogovidogo.

Mimi nitasema na sitachoka kusema kuwa nchi hii inaenda pabaya kwa teuzi hizi za kidini. Siamini na sitaki niamini kuwa Jundu ndiye Jaji Makini na Bora kuliko majaji wengine wote ambao waliteuliwa kabla yake. Na sidhani kuwa ni coincidence tu kwamba Majaji Viongozi wote walioteuliwa katika enzi za Maraisi wa awamu ya pili hadi sasa ni wa madhehebu ya aina moja. Lazima kuna kitu hapa ambacho kinafanyika na ambacho si kizuri kwa mstakabali wa nchi yetu. JK alianzia kwa mabalozi, akaingia majaji na sasa katika kipindi chake ameweka rekodi ya kuteua Majaji Kiongozi wawili ambao wana uzoefu kiduchu katika Mahakama. Hata majaji aliowateua kuingia mahakama kuu na mahakama ya rufani waliacha watu vinywa wazi. Je hii ndiyo tanzania tunayoijenga? Mtu akisema anashambuliwa kuwa kadanganya. Ninajua kuwa baadhi yetu tunamfahamu vilivyo Ndugu Fakihi Jundu na integrity yake pia inajulikana, but hii siyo forum ya kuanza hayo. Mwenye access na Kikwete amwambie kuwa anachofanya katika Taasisi zetu za umma ni kujenga uadui ambao utazalisha matatizo ambayo hatutaweza kuyathibiti in the long run. mwnyw kutukana na aendelee kutukana, but the truth/reality must be said!
 


Jobo kumbuka argument zako kwenye uteuzi wa majaji 2008. Udini!
 
Jobo kumbuka argument zako kwenye uteuzi wa majaji 2008. Udini!

Una kumbukumbu nzuri Mama! Naona bado anaendeleza yale yale na mimi kazi yangu ni kusema hadi pale Watanzania watakapoanza kuthamini uwezo wa mtu siyo dini, kabila au jinsia yake!
 
Last edited:
Wanaotukana mpaka sasa hawajatuletea Jaji Jandu aliteuliwa lini.
Siyo ukweli wote kuwa uzoefu siyo issue katika uteuzi kwa sababu Jaji Kiongozi ni mtawala wa mahakama Kuu. Tusianze mjadala mpya, bali tuletewe aliteuliwa lini?
 
Ndiyo maana Mahakama hutoa hukumu hata saa 8 za usiku iwapo Serikali ina manufaa! Si wakumbuka hukumu ya Mahakama ya KAzi dhidi ya mgomo wa Walimu? Kuna Mwanazuoni mmoja mashuhuri alishangazwa hukumu kutolewa baada ya saa za kazi tena usiku!

Salam Mkuu Ibrah;
Kutokana na Umuhimu wa taasisi hiyo (MAHAKAMA) Inabidi Majaji wa daraja fulani wawe kazini 24/7. Kama vile RAIS anakuwa kazini 24/7. hii ni kwa sababu ya mtukio ya DHARURA yanayohitaji IDHINI maalumu toka kwa Jaji au RAIS ili chombo cha serekali (Dola) kiweze kutekeleza WAJIBU wake kwa MUJIBU WAKATIBA AU SHERIA. pengine mgomo wa Waalimu haukuwa na umuhimu au dharura ya hivyo na ndio maana mwanachuo wetu alishangazwa, au tukio hilo ni geni kwake, kwani kwa nchi zilizobobea kisheria hayo ni matukio na maamuzi ya kawaida.
 
Dotori [* said:
Vile vile tuangalie upande mwingine wa shilingi. Je, inawezekana Raisi akawa anateua majaji "marafiki" ili watoe hukumu "nafuu" kwa "washtakiwa marafiki"?
[/LIST]

Now you are TALKING
Kila ngoma huanza na lele!!!! na hivi ndiyo walianza. Hawa watu ni hatari sana. They know technically how to do it. Now tayari kuna mtu wao amabye ni kinara wa majaji. Unategemea simba atamla simba mwenzake? Haitakuwa hivyo kamwe.
 
Last edited:
Tanzania inahitaji katiba mpya kwaajili ya kukabilana na changamoto za wakati wa sasa.Katiba yetu inampa rais madaraka makubwa kupita kiasi,hakuna sababu za msingi rais kuendelea kuteua majaji.kiundwe chombo huru kitakacho shughulika na ajira za majaji na wasajili wa mahakama kuu ili kuepukana na uteuzi ulio na mashaka unaofanywa na JK na hata rais atakaekuja baadaye.

Uteuzi wa jaji Jundu ni sehemu ndogo sana ya mdudu kulindana na kubebana kwa misingi ya ukabila,udini na urafiki anavyozidi kuliangamiza taifa.Kuna uteuzi wa mkuu wa mkoa nadhani wa Iringa aliteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ndani ya miezi nadhani miwili akapandishwa cheo kuwa mkuu wa Iringa.
 
Una kumbukumbu nzuri Mama! Naona bado anaendeleza yale yale na mimi kazi yangu ni kusema hadi pale Watanzania watakapoanza kuthamini uwezo wa mtu siyo dini, kabila au jinsia yake!


Je Jaji Jundu hana uwezo?
 
Mwanakijiji tunashukuru kwa habari hiyo,kama una zaidi kuhusu hilo turushie.Teuzi nyingi zinazofanywa sasa zina maswali mengi lakini tusubiri muda utatuambia yanayojiri.
 
Baadhi tu ya uzoefu wa Jaji Fakhi Jundu . Ni habari za zamani kidogo lakini haidhuru kuzisoma!


Na nyingine hii ambayo ililipotiwa 13 April 2005


Nadhani kwa sasa tunaweza kusema kwa uhakika, Bw Fakhi Jundu aliteuliwa kuwa Jaji kabla ya tarehe 13 April 2005. Lakini, bado hatujapata jibu lini hasa aliteuliwa kuwa Jaji.
 
Uwezo wake siujui lakini uzoefu hana.


Kwa hiyo unaongelea vitu viwili hapa.

Kwanza uwezo wake na pili uzoefu wake.


Kipi muhimu kati ya uwezo na uzoefu? Unayejali uzoefu kuliko uwezo wa muhusika?
 
SMU.. hiyo kesi ya pili ndiyo sababu ya Jundu kuteuliwa...!!! Ni ujumbe umetumwa!!
 

Jopo wewe akichaguliwa mtu ktk Majina yaliyo ktk Uislam ndio UDINI?...ina maana nyie wakristo mshakuwa na HAKI MILIKI YA KUONGOZA NCHI HII sio? acha ubwege.!!!!...Jadili Utendaji wa mtu kama anapendelea kundi unahaki ya kusema. Huyu Jundu akiingia una khofu gani?....unayo historia ya kuwa ameshawahi kuwa mtendaji Mbaya au Muovu? au Jina kwako Tatizo?

Hivi itakuwaje siku masheikh wakigombea Ubunge kama Wachungaji...? either CCM au chama chochote si itakuwa balaa?

Mwenzako MKJJ alikuja na Gea ya "kama mwaka mmoja" ili wana JF washutumu uteuzi usio na uzoefu...lkn Kashindwa kukubali kuwa alikosea analeta Lahaja zake...!!! Nyie Mnataka uzoefu miaka mingapi?...Kuna Mdau kaweka hapo mnataka mtu mzoefu kama Kijah aliekaa wizara ya Fedha miaka mingi? lkn pia mtadai ni udini?....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…