JK amteua Dr Migiro kuwa Mkuu wa OUT

JK amteua Dr Migiro kuwa Mkuu wa OUT

Not necessarily prof ana elimu kuliko Dr na inawezekana Dr akawa amesoma kuliko prof....kuwa Dr lazima uwe na PHd lakini prof is NOT!

Waeleze hao watoto. Wanapayuka hovyo hovyo kama wanamuziki kutoka kongo brazavile. Uprofesa is not academic qualification, it is a rank. Uingereza kuna maprofesa kibao wana degree moja tu. Uprofesa unapatikana kutokana na kuandika makala katika majarida ya kimataifa.

 
Huyu mama cheo chake kilikuwa kukubwa mno UN .Nashangaa UN wameshindwa kumpa Kazi Kama Envoy wa nchi fulani au msulihisho Huko Syria ,mali.Kuna kitu alifanya wrong labda kwa sababu uki retire UN kazima wakupe kazi nzuri mno .mwakawago alikuwa balozi na kazi alipewa .kutoka uwaziri mpaka unaibu wa ukatibu UN mpaka kuwa mkuu wa chuo that is weird.ubunge alipoteza?au
ban alimteua kuwa envoy wa masuala ya ukimwi
 
hivi ndo mwanamke wa kwanza kuwa na cheo hicho? au sio wajemeni
 
Kama alishindwa kuongoza Taasisi Kama UN ambayo Ina mpangilio wa hali ya juu na bajeti ya kutosha ndio ataweza kuongoza taasisi Kama OUT ambayo hata bajeti yake ni mgogoro?

Chuki yako itakuletea vidonda vya tumbo buuuuuuuuuuuuure. Kelele za mpangaji,...
 
Wewe kachumbari mbona unadharau vyuo vingine, tunasoma open na tumepandishwa vyeo makazini na kazi tunaiweza zaidi ya hao waliosoma UD. Tena kwenye kampuni kubwa hapa nchini. Nyau wewe.

Una hoja, lakini si vema kufanya majumuisho. Kuna waliosoma UDSM na hawawezi kazi na wapo wanaoweza; vivo hivo na Open University. Inategemea pia na uwezo binafsi wa mtu na siyo chuo alichosoma.
 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

[TABLE="width: 655"]
[TR]
[TD]Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

[/TD]
[TD][/TD]
[TD]PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.

Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM

30 Januari, 2013
Congratulations Madame, Dr. Asha Rose Migiro.

Wish you all the best in your new career development.

Queen Esther
 
Mie naona kachemka kumpa huyo mama coz mnasema tu kuwa yeye sio mtendaji ila makamu wake but wat if mkuu anakuwa na maamuzi mabovu huyo makamu anatenda nini si atatendea kazi maamuzi mabovu vile vile

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
OUT? Mbona wamemdhalilisha hvo mama wa watu? Huyu anastahili apewe chuo chenye hadhi ya kimataifa kv UDISM, Muhimbili,UDOM, TUMAini, SAUTI etc.

Hii OUT hadhi yao akina WASIRA, NCHEMBA na NAPE au CHENGE. Pole sana mama yangu najua huwezi kataa hiki kikombe maana hcho ni kipimo chako cha ukomavu japo najua unaugulia maumivu kwa ndani kimya kimya ukijitahidi kuyavumilia haya ili system iendelee kukufikiria siku za kesho na mtondogoo.


Inabidi ufanye utafiti mdogo tu kisha utoe maoni yasiyoegemea upande wowote. Kufuatana na Tume ya Vyuo Vikuu hapa Tanzania(TCU), UDSM, OUT na Muhimbili 'status' yao ni 'accredited and chartered', SAUT ni 'accredited', UDOM ni 'full registration' na Tumaini - nafikiri una maana ya Dar- 'full registration' lakini katika kundi la vyuo vishiriki. Hapo amua mwenyewe..

Cheo alichopewa ni 'ceremonial' zaidi, si cha utendaji. Kuhusu uwezo wa OUT- angalia kwanza uwezo wa viongozi wake, wametoka wapi, wamefanya nini n.k ( Prof. Mmari, Prof. Mbwette n.k)
 
Ana masilahi na hiyo familia dada yake Mwantumu Malale ni mkuu wa chuo cha Kiislamu cha morogoro na uteuzi alifanya Jakaya na sasa Asha Rose Migiro ahsante baba kwa kuongeza koo zingine za upako toka saba sasa zimekuwa nane
 
Mie naona kachemka kumpa huyo mama coz mnasema tu kuwa yeye sio mtendaji ila makamu wake but wat if mkuu anakuwa na maamuzi mabovu huyo makamu anatenda nini si atatendea kazi maamuzi mabovu vile vile

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Aisee, sasa nimepata picha ya wachangiaji hapa ndani. JF ni dodoki.
 
sawa huyu ni doctor,je profesa tolly mbwete atakuwa kama nani......mkuu wa chuo awe dokta afu msaidizi awe profesa?kweli tz vilaza kibao:target:

hicho cheo ni ceremonial,mkuu wa chuo hana madaraka ya kiutendaji mwenye madaraka hayo ni makamu mkuu wa chuo.mfano Udsm chancelor ni balozi Kazaura Vc wake ni prof mkandara
 
Ana masilahi na hiyo familia dada yake Mwantumu Malale ni mkuu wa chuo cha Kiislamu cha morogoro na uteuzi alifanya Jakaya na sasa Asha Rose Migiro ahsante baba kwa kuongeza koo zingine za upako toka saba sasa zimekuwa nane

Mhhh!!!Nadhani kuna haja ya kuanzisha VAT kwa kila mchango unaotolewa hapa JF. Inaweza kusaidia.
 
Haya mambo ya kuwa na vyeo vya kuteuliwa ni mbaya sana sometimes, maana upendeleo unakuwa ni mkubwa sana! Ukienda Pale UDSM/SUA kuna wanazuoni makini sana wanaoweza kuwa Wakuu wa Vyuo, lakini kwa kuwa hawako kwenye siasa either hawaonekani aud hawapewi nafasi hiyo ilihali wanafaa! Hii mifumo ni wazi sasa inabidi ibadilishwe!
 
sijapendezwa na viongozi wa vyama kuwa wakuu wa vyuo
italeta mgongano wa maslahi kisiasa,
watakepingana nae hapo OUT na wasio wana CCM wako hatarini kufukuzwa vyuo.
 
Back
Top Bottom