JK amteua Dr Migiro kuwa Mkuu wa OUT

JK amteua Dr Migiro kuwa Mkuu wa OUT

Mwanasiasa kiongozi wa chama kuwa mkuu wa chuo imekaaje. Hili suala la kurundikiana vyeo kila siku linapígiwa kelele lakini wapi. Huyu jamaa sijui ana chaguaje, kazi kweli kweli.
 
Thanks for correction... I meant kufanya kazi chuoni

NI huu uzaifff wetu wa kuona kila afanyaye kazi hospitali ni daktari na kila afanyaye kazi chuo ni mwalimu

All in all, with her global experience, angeweza kuwa na msaada zaidi bila kujilock on one isntitution ambayo ina taratibu za matumizi ya muda wake, nk

its ok
Acha na hzo issue,inaonyesha hata hjui kaz za mkuu wa chuo? unazidi kuandika ujinga,so kama hjui uliza.kuuliza sio ujinga bali kujielimisha.nna wasiwas na elim yako
 
Mwanasiasa kiongozi wa chama kuwa mkuu wa chuo imekaaje. Hili suala la kurundikiana vyeo kila siku linapígiwa kelele lakini wapi. Huyu jamaa sijui ana chaguaje, kazi kweli kweli.

Sifa anazo,acha wiv wewe
 
Mbona kama kuna watu wanalundikiwa madaraka kibao na wengine wako iddle? Katiba mpya ipige marufuku mambo haya mtu awe na cheo kimoja kwa wakati. Mara nyingi mfumo huu hauna ufanisi na hata ownership
 
Hongera Mh. Rais kwa uteuzi huo kwani umezingatia ni kwa jinsi Msomi huyu atakavyoweza kutosha kwenye nafasi hiyo.

Hongera Dr./Mama Migiro kwa kuteuliwa na mkuu wa nchi kwani amekuamini kuwa unaweza nawe pia hutakiwi kumwangusha.

Endeleza mazuri yaliyopo na lete mapya yenye manufaa kwa elimu masafa hii yenye changamoto nyingi za ndani na nje.
 
Hivi kumbe mtumishi wa umma anaruhusiwa kuwa mwanachama wa chama cha siasa? Au hii inafanya kazi kwa wanachama wa CCM tu? Maana ile kamati kuu dhaifu chini ya Mangula na wengine wamekuwa wakisema kuwa watumishi wa umma lazima wasiwe wanachama wa chama cha siasa.
 
Hivi watakuwa wanamlipa mshahara kiasi gani ukilinganisha na aliokuwa nao UN? Maana kutoka pay cheque ya Naibu Katibu Mkuu wa UN hadi VC wa OUT, mmh, sijui kisaikolojia inakuwaje katika kupokea mshahara wa VC wa OUT kama ulikuwa Naibu Katibu Mkuu UN.
 
Mbona kama kuna watu wanalundikiwa madaraka kibao na wengine wako iddle? Katiba mpya ipige marufuku mambo haya mtu awe na cheo kimoja kwa wakati. Mara nyingi mfumo huu hauna ufanisi na hata ownership
.

mkuu umeongea sahihi sana. Hili ni janga la kitaifa, fursa za kazi ziko chache nchini ipo haja ya kutawanya fursa hii kwa wengi badala ya mtu mmoja.

Naomba nieleweke hili si suala la Migiro tu mifano iko mingi.
 
Hivi kumbe mtumishi wa umma anaruhusiwa kuwa mwanachama wa chama cha siasa? Au hii inafanya kazi kwa wanachama wa CCM tu? Maana ile kamati kuu dhaifu chini ya Mangula na wengine wamekuwa wakisema kuwa watumishi wa umma lazima wasiwe wanachama wa chama cha siasa.
.

Migiro anaangukia vipi kwenye utumishi wa umma? nataka kufahamu kama ukiwa mkuu wa chuo automatically unakuwa mtumishi wa umma au kuna vigezo zaidi? Imekaaje hii????? weka ufafanuzi.
 
Hivi watakuwa wanamlipa mshahara kiasi gani ukilinganisha na aliokuwa nao UN? Maana kutoka pay cheque ya Naibu Katibu Mkuu wa UN hadi VC wa OUT, mmh, sijui kisaikolojia inakuwaje katika kupokea mshahara wa VC wa OUT kama ulikuwa Naibu Katibu Mkuu UN.

Hapo kwenye RED, tafadhali rudi juu kabisa ili uusome huu uzi vizuri, maana naona unachangia vitu ambavyo haviendani kabisa.
 
Mbona OUT ina hadhi sawa na vyuo vingine. Wanaokidharau wafuatilie vigezo vya kusajili wanafunzi huwa ni point ngapi. Tusiongee vitu bila utafiti. Vyuo vingi hapa TZ vilikuwa vinaacha waombaji wenye alama za kutosha sababu ya nafasi kuwa chache.
 
Hongera sana mama, jitahidi kuendeleza na kuimarisha elimu hii kwa njia ya masafa ambayo bado ni ngeni kwetu.
 
Acha na hzo issue,inaonyesha hata hjui kaz za mkuu wa chuo? unazidi kuandika ujinga,so kama hjui uliza.kuuliza sio ujinga bali kujielimisha.nna wasiwas na elim yako

Ni kawaida,

tumefika hapa tulipo kwa kuona wengine wajinga na kuwa na wasiwasi na elimu kwa kuangalia user ID ya JF. If you had take time kuelewa context iliyotumika kuelezea namna tunavyojumuisha bsi ungeelewa lakini its ok

KUhusu elimu yangu, wala usiwe na wasiwasi nayo maana mimi mwenye nayo sina!! na mimi sina wasiwasi na elimu yako maana hiyo ni yako wewe.... Niko very comfortable na elimu yangu ya sasa.

halafu hizo sentensi tatu sijui ndio elimu yako iko juu sana kiasi kwamba sie tuliosoma zamani hatuelewi au vipi maana naona kama unazunguka-zunguka tu na kujikanganya... nieleweshe mkuu, sie wengine wazito sana kuelewa, hata enzi zile tunaanza shule za kata tuliwapa tabu sana walimu wetu
 
Huyu Mama anao ubavu wa kushindana na Dk Slaa come 2015? I doubt...! Naona maandalizi yameanza rasmi...!
 
suzie,
kwanini ashindwe...? huyo kateuliwa kuwa mkuu wa chuo siyo makamu mkuu wa chuo. hashiriki ktk utendaji wowote wa kila siku wa hapo chuoni , yeye ndo anamangia kazi makamu mkuu , na huyo ndo mtendaji mkuuu . migiro anakuwa tu mkuu wa baraza/bodi

Nafagiliaga sana taarifa/post elekezi/fundishi kama hizi
 
Back
Top Bottom