JK amteua Dr Migiro kuwa Mkuu wa OUT

JK amteua Dr Migiro kuwa Mkuu wa OUT

Mpita Njia

Platinum Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
6,999
Reaction score
1,189
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

[TABLE="width: 655"]
[TR]
[TD]Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425

[/TD]
[TD][/TD]
[TD]PRESIDENT'S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Asha Rose Migiro kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Taarifa iliyotolewa Dare Es Salaam na kutiwa saini leo, Jumatano, Januari 30, 2013 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Alhamisi ya Januari 17, mwaka huu wa 2013.

Mheshimiwa Asha Rose Migiro ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Katibu wa NEC wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Aidha, Dkt. Migiro amepata kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM

30 Januari, 2013
 
Kabla JK hajamaliza muda wake lazime atam-award tena li-title jingine. Take my word.
 
Huyu mama kwenye level ya decision making naona hawezi wanamchafua bure anafaa kwenye operation yaani anatakiwa aongozwe sio kuongoza kabisa

suzie,
kwanini ashindwe...? huyo kateuliwa kuwa mkuu wa chuo siyo makamu mkuu wa chuo. hashiriki ktk utendaji wowote wa kila siku wa hapo chuoni , yeye ndo anamangia kazi makamu mkuu , na huyo ndo mtendaji mkuuu . migiro anakuwa tu mkuu wa baraza/bodi
 
Kuna mshahara na marupurupu lakini au ni swaga za kukuziana cv kwa ajili ya malengo fulani hapo siku chache zijazo?
 
Wewe. Baraza lina mwenyekiti wake. Mkuu wa Chuo sio mwenyekiti wala mjumbe wa baraza la chuo.
 
Wewe. Baraza lina mwenyekiti wake. Mkuu wa Chuo sio mwenyekiti wala mjumbe wa baraza la chuo.

sawa hata kama baraza lina mkuu wake. lakini mkuu wa chuo siyo mtendaji...samahani mimi sijui utawala wa vyuo. ila ukweli unabaki kuwa mkuu wa chuo siyo mtendaji mkuu ktk chuo
 
Kuna mshahara na marupurupu lakini au ni swaga za kukuziana cv kwa ajili ya malengo fulani hapo siku chache zijazo?
Anawapotezeeni lengo nyie vilaza msahau kuwa anamuandaa kuwa mrithi wake; anajua wadanganyika huwa wanasahau mambo upesi kama walivyokwisahau jinsi wakina Ngeleja na Maige walivyoliibia Taifa na sasa wanakula taratibu bila wasiwasi!!
 
Back
Top Bottom