Jirani anajenga Msingi wa ukuta katikati ya jiwe la mpaka la manispaa, Sheria ya Ardhi inaruhusu hii?

Huu ukuta ni wa kishari shari ndio maana nauogopa.. maana viwanja vyetu ni vya mtaa wa mwisho. Nyuma yetu kuna majirani waliojenga kienyeji enyeji..

Hao watu wote watategemea mimi ndio niwaachie njia kubwa.. maana walikuja kuomba na tukaongea na jirani wote tuingie ndani mita chache ili wa nyuma wapate njia.

Sasa ghafla jirani kaanza jenga ukuta nyuma ya beacon kabisa
Ramani inaonyesha kuna njia baina yako na jirani?
 
Yes amemsaidia upande mmoja..........Kuna wengine wana bahati anasaidiwa pande tatu zote yeye anabakiza kufunga mbele tu na kuweka geti....Ukinunua viwanja vya kupimwa ndio advantages zake hizo.
Hapana.Kuacha nafasi kati ya nyumba ya kiwanja kimoja na kiwanja kingine ni lazima kisheria za ujenzi.Na kuna vipimo vyake.Kila mmoja ataacha mita moja na nusu kutoka katika jiwe/bikoni yake.Akileta ubishi atabanwa kwa kuombwa yafuatayo kisheria za mipangomiji/halmashauri;-
1-Uhalali wa umiliki eneo(nyaraka halali),
2-kibali cha ujenzi kinachoenenda na muda(expire date)
3-Na kama amehamia/nyumba ipo,ataombwa leseni/kibali/ruhusa ya kisheria ya kuishi hapo,
4-Hana hivyo vitu;a,atapigwa faini kimojakimoja-b,atasimamishwa ujenzi-c,atavunja ukuta kwa muda atakaopewa kwa gharama zake-d,atapewa onyo kali aache ungedere.🙏🙏🙏😂😂😂😂
 
Habari wadau.

Nina kiwanja changu kimepimwa na manispaa ya Ubungo.

Jirani yangu naepakana nae ameamua kujenga msingi wa ukuta wake kati kati ya jiwe linalotutenganisha..

Je yupo sahihi ? Sheria ya Ardhi inaruhusu hili kutokea?

Wataalamu na wazoefu naombeni ushauri

Tazama picha. Kiwanja changu ni upande wa kushoto na cha jirani ni upande wa kulia wa beacon

Beacon iliyowekwa na manispaa ndiyo hiyo pembeni ya mti ( mti ameuweka ndani ya upande wa kiwanja changu) na hayo nyuma ndio matofali ya jiraniView attachment 2371564
Kama anajenga ukuta ni sawa kaeni chini mchangie gharama ukuta uwe wenu wote.

Ila kama anajenga nyumba na ikiwa una nguvu kdg ya kifedha wala usimsemeshe atakapotoa kijiti chake weka chako jenga ukuta mrefu kupita makadirio ya pale atakapofungia lenta. Then kaa relax uone atapauaje?
 
Hapana.Kuacha nafasi kati ya nyumba ya kiwanja kimoja na kiwanja kingine ni lazima kisheria za ujenzi.Na kuna vipimo vyake.Kila mmoja ataacha mita moja na nusu kutoka katika jiwe/bikoni yake.Akileta ubishi atabanwa kwa kuombwa yafuatayo kisheria za mipangomiji/halmashauri;-
1-Uhalali wa umiliki eneo(nyaraka halali),
2-kibali cha ujenzi kinachoenenda na muda(expire date)
3-Na kama amehamia/nyumba ipo,ataombwa leseni/kibali/ruhusa ya kisheria ya kuishi hapo,
4-Hana hivyo vitu;a,atapigwa faini kimojakimoja-b,atasimamishwa ujenzi-c,atavunja ukuta kwa muda atakaopewa kwa gharama zake-d,atapewa onyo kali aache ungedere.🙏🙏🙏😂😂😂😂
Tanzania hii hii ya Samia au
 
Kama anajenga ukuta ni sawa kaeni chini mchangie gharama ukuta uwe wenu wote.

Ila kama anajenga nyumba na ikiwa una nguvu kdg ya kifedha wala usimsemeshe atakapotoa kijiti chako weka chako jenga ukuta mrefu kupita makadirio ya pale atakapofungia lenta. Then kaa relax uone atapauaje?

Ukuta anaoujenga ataupaua. Maana mabanda ya kuku wake na mifugo mingine yanategemea huu ukuta.

Sasa akiupaua si itakuwa balaa
 
Habari wadau,

Nina kiwanja changu kimepimwa na manispaa ya Ubungo.

Jirani yangu naepakana nae ameamua kujenga msingi wa ukuta wake kati kati ya jiwe linalotutenganisha..

Je, yupo sahihi? Sheria ya Ardhi inaruhusu hili kutokea?

Wataalamu na wazoefu naombeni ushauri

Tazama picha. Kiwanja changu ni upande wa kushoto na cha jirani ni upande wa kulia wa beacon

Beacon iliyowekwa na manispaa ndiyo hiyo pembeni ya mti (mti ameuweka ndani ya upande wa kiwanja changu) na hayo nyuma ndio matofali ya jirani

View attachment 2371564

Hiyo si ni fensi mkuu? Kama ni fensi hapo yuko sahihi shukuru Mungu kakusaidia upande mmoja wa fensi.

Sali zaidi watokee na upande wa nyuma na pembeni.

Ila kama si fensi hapo sasa patakuwa na shida.
 
Yes amemsaidia upande mmoja..........Kuna wengine wana bahati anasaidiwa pande tatu zote yeye anabakiza kufunga mbele tu na kuweka geti....Ukinunua viwanja vya kupimwa ndio advantages zake hizo.
Sijawahi kubahatika hili zaidi nimewafaidisha majirani mara mbili sehemu tofauti.
Mimi naumia kujenga ukuta halafu wao wanakuja kuunganisha ukuta tu utafiiiri mimi baba yao
 
Ukuta anaoujenga ataupaua. Maana mabanda ya kuku wake na mifugo mingine yanategemea huu ukuta.

Sasa akiupaua si itakuwa balaa
Kama ni ukuta wa banda na si nyumba ya kuishi mfikishe kwenye uongozi mkubaliane kuwa utakapohitaji kujenga utautumia ukuta wake then unakuja unamalizia alipoishia unazungusha ukuta wako na upande huo unaotesha fensi ya maua ili kuziba madirisha yake asiwe anakupiga chabo ukiwa kwako
 
FRESHMAN Inategemea na muundo wa block yenu. Kama ipo kama hii picha ilivyo kwa maana kwamba viwanja vyenu vipo "mkabala", basi jirani yupo sahihi na kakusaidia kujenga fence.
JPEG_20220929_155231_5069528332621283227.jpg
 
Sijawahi kubahatika hili zaidi nimewafaidisha majirani mara mbili sehemu tofauti.
Mimi naumia kujenga ukuta halafu wao wanakuja kuunganisha ukuta tu
Ikiwa najenga ukuta lazima ni mshirikishe jirani gharama kutegemeana na hali yake ya kimaisha ili tuutumie wote na ikiwa atakuwa mkorofi na ninaona kbs uwezo anao na kiwanja changu ni kikubwa upande wake naotesha fensi then hatua moja kuja kwangu najenga ukuta
 
Back
Top Bottom