Jirani anajenga Msingi wa ukuta katikati ya jiwe la mpaka la manispaa, Sheria ya Ardhi inaruhusu hii?

FRESHMAN

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
8,822
33,527
Habari wadau,

Nina kiwanja changu kimepimwa na manispaa ya Ubungo.

Jirani yangu naepakana nae ameamua kujenga msingi wa ukuta wake kati kati ya jiwe linalotutenganisha..

Je, yupo sahihi? Sheria ya Ardhi inaruhusu hili kutokea?

Wataalamu na wazoefu naombeni ushauri

Tazama picha. Kiwanja changu ni upande wa kushoto na cha jirani ni upande wa kulia wa beacon

Beacon iliyowekwa na manispaa ndiyo hiyo pembeni ya mti (mti ameuweka ndani ya upande wa kiwanja changu) na hayo nyuma ndio matofali ya jirani

20220929_142623.jpg
 
Habari wadau.

Nina kiwanja changu kimepimwa na manispaa ya Ubungo.

Jirani yangu naepakana nae ameamua kujenga msingi wa ukuta wake kati kati ya jiwe linalotutenganisha..

Je yupo sahihi ? Sheria ya Ardhi inaruhusu hili kutokea?

Wataalamu na wazoefu naombeni ushauri

Tazama picha. Beacon iliyowekwa na manispaa ndiyo hiyo pembeni ya mti na hayo nyuma ndio matofali ya jiraniView attachment 2371564
Si Ushukuru hata anakuwekea ukuta wew vepee

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Amekengeuka.Kuna umbali maalum/kipimo katika mita alipaswa kuingia kwa upande wake ndiyo ajenge.Hiyo ni ili aache nafasi kati yake na jirani.Pia aache uchochoro/nafasi kwa ajili ya huduma za jamii kama maji,umeme na hata njia ya kupita.Mumuwahi kabla hajaziba kabisa eneo kwa kuwapa taarifa viongozi wa mtaa au Mipangomiji/Ardhi wilayani waje wampe elimu.
 
Si Ushukuru hata anakuwekea ukuta wew vepee

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app

Huu ukuta ni wa kishari shari ndio maana nauogopa.. maana viwanja vyetu ni vya mtaa wa mwisho. Nyuma yetu kuna majirani waliojenga kienyeji enyeji..

Hao watu wote watategemea mimi ndio niwaachie njia kubwa.. maana walikuja kuomba na tukaongea na jirani wote tuingie ndani mita chache ili wa nyuma wapate njia.

Sasa ghafla jirani kaanza jenga ukuta nyuma ya beacon kabisa
 
Huu ukuta ni wa kishari shari ndio maana nauogopa.. maana viwanja vyetu ni vya mtaa wa mwisho. Nyuma yetu kuna majirani waliojenga kienyeji enyeji..

Hao watu wote watategemea mimi ndio niwaachie njia kubwa.. maana walikuja kuomba na tukaongea na jirani wote tuingie ndani mita chache ili
wa nyuma wapate njia.

Sasa ghafla jirani kaanza jenga ukuta nyuma ya beacon kabisa. Hapo watu wa nyuma wote watategemea mimi peke yangu ndie niwape njia
 
Huu ukuta ni wa kishari shari ndio maana nauogopa.. maana viwanja vyetu ni vya mtaa wa mwisho. Nyuma yetu kuna majirani waliojenga kienyeji enyeji..

Hao watu wote watategemea mimi ndio niwaachie njia kubwa.. maana walikuja kuomba na tukaongea na jirani wote tuingie ndani mita chache ili wa nyuma wapate njia.

Sasa ghafla jirani kaanza jenga ukuta nyuma ya beacon kabisa
Siyo kuombwa.Uchochoro kati ya nyumba na nyumba ni lazima uachwe kwa vipimo vyake kitaalamu.Ujenzi holela,ubishiubishi na maroho machafu huwa yanazua balaa.Mkalisheni chini mumueleze huyo mshari.Laa sivyo mbeleni atawasumbua zaidi.Wa wapi huyo jirani yako?
 
Back
Top Bottom