MANKA MUSA
JF-Expert Member
- Jul 9, 2014
- 922
- 1,093
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan leo September 19 ameweka Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Kilwa pamoja na kugawa wa Boti 34 kati ya 160 zilizonunuliwa na Serikali kwa Wavuvi na Wakulima wa Mwani.
Hayo yamejiri Wakati wa Ziara ya Kikazi Mkoani Lindi Wilaya ya Kilwa ambapo Rais Samia amesema Ujenzi wa Bandari hiyo utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 260 na itachukuwa muda wa miezi 36 kukamilika.
Kuhusu Boti 34 kati 160 alizogawa kwa Wavuvi, Rais Dkt,Samia amesema boti hizo zinatolewa kwa mkopo nafuu na kuwataka Wavuvi waliokabidhiwa kurejesha mkopo kwa wakati.
Hata hivyo Rais Samia amesema Serikali imekusudia kufufua mji wa Kilwa kiuchumi na kuurudisha kwenye hadhi yake kama zamani.