Kesi ya Mkurugenzi wa zamani wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi yafikisha siku 660 bila upelelezi kukamilika

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
1686576541565.png

Upelelezi katika kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili, aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Lusubilo Mwakabibi na Mratibu wa Mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam (DMDP) Edward Haule, bado haujakamilika.

Mwakabibi na Haule, wanakabiliwa na mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya madaraka wakiwa watumishi wa Serikali, katika kesi ya Uhujumu Uchumi namba 63/2021.

Mpaka leo Jumatatu Juni 12, 2023 kesi hiyo imefikisha siku 660 ikiwa katika hatua ya kujatwa, huku upelelezi wa shauri hilo ukiwa bado haujakamilika.

Kwa mara ya kwanza, washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Agosti 20, 2021 wakikabiliwa na mashtaka mawili ya matumizi mabaya ya ofisi na madaraka.

Tangu siku hiyo hadi leo kesi hiyo imetimiza siku 660 ambazo ni sawa na mwaka mmoja na miezi tisa na siku 25, bila upelelezi wa shauri hilo kukamilika.

Leo, Wakili Serikali, Monica Ndakidemi aliieleza mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Ndakidemi alitoa maelezo hayo wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Kutokana na maelezo, hakimu Kyaruzi ameharisha kesi hiyo hadi Juni 26, 2023 itakapotajwa na washtakiwa wapo nje kwa dhamana.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, katika shtaka la kwanza ambalo ni matumizi mabaya ya ofisi, washtakiwa wanaodaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Machi 2020 na Machi 2021 katika Manispaa ya Temeke.

Inadaiwa siku hiyo tukio, Mwakabibi akiwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke na Haule akiwa Mratibu wa Mradi wa DMDP na wakiwa waajiriwa wa manispaa hiyo, katika utekelezaji wa ardhi walielekeza ujenzi wa stendi ya mabasi eneo la Buza, kiwanja ambacho kinamilikiwa na Dayosisi ya Kanisa la Anglikana bila kuwa na ruhusa.

Shtaka la pili ni matumizi mabaya ya madaraka, tukio wanaodaiwa kulitenda Machi 2020 na Machi 2021 katika eneo hilo, washtakiwa kwa makusudi wakitumia madaraka yao vibaya na kinyume na kifungu cha 3(1) Cha Sheria ya Ardhi na kifungu cha 3,4,5,7 na 11 Cha Sheria ya Ardhi ya mwaka 2019.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom