Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,703
- 218,231
Nimeona ni vema jambo hili liwekwe wazi ili kuondoa upotoshaji maana tayari kuna wapotoshaji wameanza kazi yao.
Uongozi na hasa uongozi wa Juu kama Urais, unaendeshwa kwa utaratibu uliowekwa ndani ya Katiba ya nchi, hauendeshwi kwa kutumia jinsia, kigezo hicho hakuna, Suruali au dela la mtu havina mchango wowote kwenye uongozi Mtu yeyote atabebwa na uwezo wake na jinsi anavyoweza kufuata misingi iliyo ndani ya Katiba.
Ikiwa kama wanawake wanao uwezo basi watapewa uongozi kwa uwezo wao waliouonyesha, hawatapewa uongozi kwa sketi zao, na wakishindwa hatutawaonea huruma kwa vile wamevaa hijab, watapigwa chini mchana kweupe bila huruma yoyote ile, hivyo ndivyo tutakavyofanya hata kwa wanaume, uongozi si sawa na kubeba Matofali kwamba ni lazima pande la mtu ndio lituongoze.
Natoa onyo kwa yeyote yule anayetaka kugawa uongozi kwa misingi ya jinsia, kwamba akifanya hivyo tutampinga na atajizolea dharau bila sababu ya msingi, waacheni wenye uwezo wagombee uongozi na tutawatathmini kwa uwezo wao na wala si kwa jinsia zao.
Enzi za kuburuzwa kwa hoja za uongo zimekwisha na hazina nafasi tena