SoC01 Jinsi zawadi za shindano la Stories of Change zinavyoweza kubadili maisha ya washindi

Stories of Change - 2021 Competition

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,822
18,245
Uongozi wa mtandao maarufu wa Jamii Forums (JF) umebuni shindano la Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change) kwa wanachama wake. Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 15, 2021. Zawadi zilizotangazwa kutolewa ni kama zinavyoonekana kwenye kielelezo kifuatacho.

1627855976001.png

Mfano wa zawadi zinazoshindaniwa
Chanzo: Jamii Forums

Nawashukuru sana viongozi wa JF, pamoja na kuwa lengo lao sio kugawa fedha bali kuchochea uandishi wenye kuleta tija, lakini wameona busara kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi watakaoshinda katika mchuano huu. Watu wengi wanakwama kujiendeleza kiuchumi kwa sababu ya kukosa rasilimalifedha za kufanyia shughuli mbalimbali za uzalishaji. Ni imani yangu kwamba washindi watakaoshinda zawadi hizi watazitumia kwa njia chanya zitakazosaidia kuinua uchumi wao kwa namna tofauti tofauti kulingana na ukubwa wa zawadi.

Ikiwa washindi (nikiwemo mimi, iwapo nitafanikiwa kushinda) watazitumia zawadi hizi vizuri, hasa fedha, nina uhakika zitaenda kubadilisha maisha yao kwa kiasi kikubwa sana. Nitatoa mifano michache jinsi ambavyo washindi wanaweza kunufaika na zawadi hizi kwa kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Baadhi ya watu wana mawazo mazuri sana ya kibiashara lakini wanakosa mtaji. Au labda kuna baadhi waliwahi kufanya biashara isiyofaa wakajikuta wanafilisika kwa namna moja au nyingine au huenda walipatwa na majanga mbalimbali kama vile moto, kuibiwa, au biashara zao kutaifishwa, n.k.

Sio siri kuwa rasilimalifedha ndicho kikwazo kikubwa katika masuala mazima ya uzalishaji mali. Hivyo basi, kwa wale watakaoshinda zawadi ya fedha taslimu au vifaa kama zilivyotangazwa kwenye orodha ya zawadi, wanaweza wakanufaika kiuchumi kwa kuzitumia kufanyia shughuli za uzalishaji mali zinazoingiza faida. Kuna aina nyingi ya shughuli kutegemea na mazingira anapokaa mshindi au shughuli alizozoea kufanya lakini naomba nitoe mifano michache na rahisi ya shughuli ambazo mshindi anaweza kuzifanya na zikamzalishia fedha za kutosha. Baadhi ya shughuli hizi ni kama ifuatavyo:

1. Kununua hisa
Ununuzi wa hisa ni biashara inayolipa ijapokuwa watanzania wengi hawaifahamu. Ni watu wachache sana wanaofahamu manufaa ya kununua hisa na jinsi gawio la hisa linavyoweza kuwanufaisha kiuchumi. Kwa kuwa zawadi ya fedha inaanzia Tsh 5,000,000 hadi Tsh 2,000,000, fedha hizi zinawatosha kabisa washindi kununua hisa kwenye makampuni au mabenki na kupata faida kubwa.

Hisa ni sehemu ya umiliki wa kampuni. Hivyo, hisa moja inawakilisha asilimia ndogo ya umiliki katika kampuni. Kama kampuni ina hisa milioni moja na mwekezaji anamiliki hisa 100,000 mwekezaji huyu anamiliki 1% ya kampuni. Mwekezaji anayenunua hisa basi ananunua haki ya kumiliki kampuni. Stahili za mwenye hisa ni pamoja na kushiriki katika kutoa maamuzi ya kampuni katika mkutano mkuu wa wanahisa na kupata gawio litokanalo na faida. Ana haki pia ya kuuza hisa zake kwa faida pale ambapo kuna ongezeko la thamani ya hisa.

Gawio ni malipo yanayofanywa na kampuni kwa wanahisa kutokana na faida ya kampuni. Malipo haya yanapendekezwa na wakurugenzi na kuidhinishwa na mkutano mkuu wa wanahisa. Gawio linaweza kulipwa kutokana na faida ya mwaka husika au malimbikizo ya faida za nyuma. Aidha, gawio linaweza kulipwa kwa fedha taslimu au kwa kuwaongezea hisa wanahisa.

Kwa hiyo, mshindi wa fedha za shindano la Stories of Change anaweza akaamua kununua hisa kwenye kampuni fulani, akawa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo na kujipatia gawio la hisa kila baada ya muda fulani kutokana na faida ya kampuni. Anaweza akachagua kuwekeza fedha zote (million 5, million 3 au milioni 2) au akawekeza tu sehemu ya fedha na kubakisha kiasi kingine kwa ajili ya shughuli nyingine.

2. Fixed depsoit
Ikiwa mshindi ataamua kutowekeza fedha kwenye biashara yoyote, anaweza kuziweka benki kwa muda atakaopenda (miezi, mwaka au miaka, nk) kisha akazichukua pamoja na faida. Mfano wa namna faida inavyopatikana kutokana na fixed deposit ni kama inavyoonekana hapo chini:

1627856381118.png

Mfano wa faida ya kuweka fedha fixed deposit
Chanzo: Mtandao

Kwa mujibu wa kielelezo hapo juu, kwa mfano, mtu atakayeshinda Tsh 2,000,000 kama ataamua kuziweka benki kwa muda wa mwaka mzima atapata faida ya 3% ya fedha zake. Hii maana yake ni nini? Baada ya mwaka mmoja fedha zake zitakuwa zimeongezeka kwa asilimia tatu; sasa atachukua Tsh 2,060,000 na endapo utaamua kuacha zikae benki kwa mwaka mwingine zaidi, zitaongezeka hadi kufika Tsh 2,121,800. Utaona kwamba fedha zake zinazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka. Faida katika fixed deposit ni faida inayozaa ila unatakiwa uziache fedha zikae kwa muda mliokubaliana bila kuzichukua.

3. Biashara
Uwekezaji kwenye biashara ni eneo jingine ambalo mshindi anaweza kuamua kuwekeza. Kuna biashara za aina nyingi, kuanzia kufungua duka au genge hadi biashara za rejareja. Kwa mfano, ikiwa atachagua kufungua genge, basi anaweza ama kukodi fremu au kukodi eneo la wazi na kujenga banda la kawaida kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake. Kiasi chochote cha fedha atakachoshinda – iwe million 5, million 3 au 3 – kinatosha kwa shughuli hii. Kwa mfano, ikiwa ataamua kufungua genge la mama au baba Ntilie, atatenga Tsh 150,000 akodi banda kwa miezi 3; Tsh 150,000 anunue sufuria, majiko, mkaa, mwiko na vifaa vingine vya kazi; na Tsh 300,000 anunue vipikio kama vile unga, mafuta ya kula, mchele, nyama, mboga, nk. Na kiasi kitakachobaki ataweka kama akiba kwa ajili ya dharula zitakazojitokeza. Sijaweka mshahara wa wasaidizi kwa kuwa wasaidizi wanalipwa kwa siku kulingana na makubaliano lakini malipo kwa mfanyakazi mmmoja kwa siku hayapindukii Tsh 4,000.

1627856535792.png

Biashara ya mama Ntilie ni mojawapo ya biashara nyingi ambazo mshindi anaweza kuamua kufanya
Chanzo: Mtandao

Kana kwamba biashara ya mama Ntilie haitoshi, mshindi naweza pia kufungua biashara ya kuuza bidhaa kama vile nguo au akafungua duka la vyakula na mahitaji mengine ya nyumbani. Mtu ukiwa na mtaji huwezi kukwama kubuni biashara yoyote inayolipa ikakuingizia kipato cha uhakika.

4. Kilimo
Kilimo ni biashara kama biashara nyingine kwa sababu kinahusisha matumizi ya fedha na kinalenga kupata faida. Kulingana na eneo la kijiografia analotoka mshindi, anaweza kuamua achague zao moja la nafaka au bustani akalima kitaalamu na kupata faida kubwa.

Kinachowaponza wakulima wengi hata wasifanikiwe katika kilimo ni mtaji. Kwa kuwa sasa mtu atakuwa ameshinda fedha za mtaji, kitakachobaki ni kutafuta shamba na kujikita katika kilimo. Nashauri mtu asije akawekeza fedha kwenye kilimo kwa kufuata mkumbo. Kila mtu atataka kuwa mwalimu wa kukuchagulia zao la kulima. Kuwa makini; usikubali kila ushauri utakaopewa. Ukishapata fedha zako, kaa chini utulize akili na usome vizuri aina ya kilimo unachoweza kufanya kikakuletea faida na tija. Usikurupuke!

1627856660645.png

Kilimo cha mboga
Chanzo: Mtandao

Kwa mfano, ikiwa unaishi kwenye eneo lenye mito na mabonde ya kutosha unaweza ukalima mahindi kwa kumwagilia wakati wa kiangazi halafu ukauza mahindi mabichi ya kuchoma (maarufu kama gobo). Biashara ya mahindi ya kuchoma imeshamiri kila mahali, hasa maeneo ya mjini, hivyo soko lipo. Kinachotakiwa tu ni kuweka ratiba zako za kilimo vizuri kuhakikisha wakati wa mavuno hakutakuwa na mahindi mengi sokoni. Mbinu moja kubwa ni kulima kilimo cha kumwagilia ili uwe na uhakika wa kuuza mahindi wakati wowote bila kujali kama mvua imenyesha au la.

Unaweza kulima kwa kutumia mtaji kidogo na kupata faida. Angalia mchanganuo ufuatao: kukodi shamba ekari moja inagharimu wastani wa Tsh 50,000/=, kulima Tsh 30,000/=, kupalilia Tsh 30,000/=, mbolea mifuko 3, Tsh 150,000/= na madawa Tsh 50,000/=. Jumla kuu ni Tsh 310,000/=.

Kwa ekari moja, ukilima kwa kuzingatia utaalamu una uhakika wa kuvuna kuanzia mahindi 9,800. Hindi moja huuzwa kwa Tsh. 150/= hadi 250/=, kutegemea hali ya soko kwa bei ya jumla. Ukikokotoa utaona kuwa kwa ekari moja unaweza kupata Tsh 1,470,000/= kwa makadirio ya chini na Tsh 2,450,000/= kwa makadirio yaa juu. Ukitoa gharama za uendeshaji (za moja kwa moja) unaweza kukunja faida ya hadi Tsh 2,140,000/= kwa makadirio ya juu. Je, ukilima misimu kadhaa bado utashindwa kujenga nyumba ya maana au kuwa na maisha yenye unafuu? Bila shaka utaweza!

1627856910183.png

Shamba la mahindi yaliyopandwa kitaalamu
Chanzo: Mtandao

Mbali ya kilimo cha mahindi, kilimo cha nyanya nacho kinalipa. Utaratibu wa ulimaji wa zao hili hautofautiani na ule wa kilimo cha mahindi. Mimea ya nyanya haistahimili mvua nyingi kwa kuwa mvua huchochea magonjwa ya ukungu. Mkulima mzuri wa nyanya ni yule anayelazimisha kulima wakati wa msimu wa mvua kwa sababu wakati huo wakulima wengi hushindwa kuhudumia zao la nyanya. Ijapokuwa utatumia gharama kubwa lakini utauza mazao yako kwa bei ya juu itakayokuingizia faida kubwa zaidi. Hivyo, zao mojawapo ambalo mshindi wa zawadi ya fedha kutokana na shindano la Stories of Change anaweza kulima na kumletea faida kubwa ni zao la nyanya.

5. Ufugaji
Kama ilivyo kwenye kilimo, ufugaji nao ni biashara nzuri iwapo utachagua aina ya ufugaji unaoumudu kulingana na eneo lako la kijiografia, kiasi cha mtaji au uwepo wa eneo. Kuna ufugaji wa ina nyingi unaowezekana kufanyika hapa nchini ukiwemo ufugaji wa nyuki, kuku, mbuzi na mifugo mingine. Aina ya mifugo ambao wanafugika kirahisi ni kuku, hasa kuku wa asili, chotara, au nyama. Ufugaji wa kuku ni mzuri zaidi kwa kuwa hauhitaji gharama kubwa na unaweza kufanyika kwa namna nyingi kutegemea rasilimali ulizonazo. Katika maelezo yangu nitajikita zaidi kwenye ufugaji wa kuku wa nyama.

1627857024480.png

Ufugaji wa kuku wa nyama
Chanzo: Mtandao

Ufugaji wa kuku wa nyama ni rahisi kwa kuwa vifaranga wa nyama hufikia umri wa kuuza baada ya mwezi mmoja (siku 30) tu! Kwa kuanzia, unaweza kuanza na kuku wa nyama wapatao 200 ambao utawanunua kwa wastani wa Tsh 1,500 kwa kila kifaranga mmoja. Hivyo, vifaranga 200 watagharimu Tsh 300,000. Gharama za vifaa kama vile vyombo vya kulishia na kunyweshea maji vinaweza kugharimu Tsh 50,000. Gharama za vyakula tangu wakiwa wadogo (chick starter) hadi wanafika umri wa kuingia sokoni (finisher) zinakadiriwa kufika Tsh 600,000. Kama huna banda unaweza kukodi kwa Tsh 50,000. Jumla ya gharama zote ni Tsh 1,000,000. Kama utazingatia kanuni za ufugaji bora, hadi kufika wakati wa mauzo utakuwa na kuku 195 (watano tu watakufa). Kuku mmoja wa nyama huuzwa wastani wa Tsh 8,000. Hivyo jumla ya mauzo itakuwa Tsh 195x8000 = 1,560,000. Jumla ya faida = 1560000 -1,000,000 = 560,000.

Utaona kwamba gharama za kufuga kuku 200 wa nyama zinaangukia ndani ya zawadi zote za ushindi. Ikiwa mshindi yeyote atashindwa kutumia zawadi yake kufugia na kujiongezea kipato, huo utakuwa uzembe wake binafsi. Mshindi yeyote (nikiwemo mimi) akiamua kutumia fedha hizo kwa matanuzi hadi zikaisha, asije akatafuta mchawi kwani mchawi ni yeye (au mimi) mwenyewe.

5. Urahisi na unafuu wa mawasiliano
Tusisahau pia vifaa vya mawasiliano (simu, tablet na laptop) ni sehemu ya zawadi kemkem zitakazotolewa na kampuni ya Jamii Media kwa baadhi ya washindi. Vifaa hivi vitawasaidia washindi kurahisisha na kupata unafuu wa mawasiliano. Kwa mfano, ikiwa mshindi alikuwa akilazimika kwenda kulipia muda kwenye mgahawa wa intaneti, sasa atakuwa anapata mawasiliano kiganjani mwake. Atakachohitaji tu ni kununua modemu ya kuchomeka kwenye laptop na kuijaza bando au kutiririka moja kwa moja kutoka kwenye simu au tablet yake. Hii itamuongezea unafuu na urahisi wa mawasiliano, hivyo kufanya maisha yake kuwa bora zaidi ukilinganisha na zamani. Aidha, urahisi na unafuu huu utamuongezea chachu ya kushiriki na kushinda shindano la awamu ya pili la Stories of Change kutoka hapa hapa JF.

6. Umaarufu
Zawadi ya Ubalozi wa Jamii Forums itamuongezea mshindi umaarufu kwa kuwa atatangazwa katika mitandao yote ya JF na mbele ya vyombo vingine vya habari wakati akitangazwa kuwa balozi. Kitendo hiki kitampa umaarufu mkubwa sana kwani atafahamika kwa watu wengi ndani ya muda mfupi. Umaarufu huu utamsaidia kupata koneksheni na watu wengine maarufu nchini na dunia nzima kwa ujumla, hivyo kumuongezea thamani ya kijamii (social value).

Kwa kumalizia, nawaomba wote mtakaofanikiwa kuusoma huu mnakasha mnipigie kura kwa kubonyeza kitufe hiki hapa chini kinachopatikana upande wa juu, kulia mwa mnakasha wangu. Huenda nikafanikiwa kunyakua hili donge nikalitumia kama nilivyoeleza hapo juu

1627855728832.png

Mbarikiwe sana wapendwa wanaJF mnapojiandaa kunipigia kura zenu za ushindi.

Asanteni.​
 
tpaul Hongera kwa hili bandiko, nimevutiwa na mchanganuo wa matumizi ya fedha hasa kwenye Biashara, Kilimo na Ufugaji,

Nimekuwa wa kwanza ku_Upvote. Kila lakheri ndugu
Ubarikiwe sana mkuu. Ndugu zangu naomba mniunge mkono kwa kunipa kura za kutosha. Mungu awabariki sana mnapojiandaa kunipa kura zenu.
 
Tafadhali ndugu zangu wanaJF naomba mniunge mkono kwa kunipigia kura kwa kugonga hapo nilipoonyesha kwenye screenshot. Mpaka sasa nina kura moja tu; natia huruma sana aisee! Mbarikiwe sana 🙏
1627938000202.png
 
Biashara ya hisa kwa Tanzania ni upotolo mtupu
Biashara hii inategenea kama kampuni uliyowekeza hisa zako inatengeneza faida kiasi gani. Kama kampuni uliyowekeza inatengeneza faida kidogo utapata faida kidogo pia. Ndio maana nimetoa angalizo mtu kuwa makini katika kuchagua kampuni unayowekeza.

Hata hivyo, nimetoa njia zingine ambako unaweza kuwekeza fedha zako za ushindi, ikiwemo kilimo, ufugaji na biashara.

Tafadhali naomba kura yako mkuu Bujibuji 🙏
 
Naomba jina la uzi wako
 
Naomba jina la uzi wako
Uzi ni huu huu mkuu. Na nyingine hizi hapa👇 Naomba support yako ya nguvu kiongozi Bujibuji

Tafadhali wakuuu naomba muendelee kunipigia kura kwa kugonga hapo nilipoonyesha. Ukigonga hapo mara moja tu utaona kura zinaongezeka. Natia huruma sana ndugu zangu kwani hadi sasa nina kura 6 tu! Asanteni kwa kunielewa na kunipigia kura. Mungu awabariki sana 🙏
1628108786996.png
 
Uongozi wa mtandao maarufu wa Jamii Forums (JF) umebuni shindano la Uandishi wa Mtandaoni wenye kuleta tija (Stories of Change) kwa wanachama wake. Awamu ya kwanza ya shindano hili itaanza Julai 14 hadi Septemba 15, 2021. Zawadi zilizotangazwa kutolewa ni kama zinavyoonekana kwenye kielelezo kifuatacho.

View attachment 1876899
Mfano wa zawadi zinazoshindaniwa
Chanzo: Jamii Forums

Nawashukuru sana viongozi wa JF, pamoja na kuwa lengo lao sio kugawa fedha bali kuchochea uandishi wenye kuleta tija, lakini wameona busara kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi watakaoshinda katika mchuano huu. Watu wengi wanakwama kujiendeleza kiuchumi kwa sababu ya kukosa rasilimalifedha za kufanyia shughuli mbalimbali za uzalishaji. Ni imani yangu kwamba washindi watakaoshinda zawadi hizi watazitumia kwa njia chanya zitakazosaidia kuinua uchumi wao kwa namna tofauti tofauti kulingana na ukubwa wa zawadi.

Ikiwa washindi (nikiwemo mimi, iwapo nitafanikiwa kushinda) watazitumia zawadi hizi vizuri, hasa fedha, nina uhakika zitaenda kubadilisha maisha yao kwa kiasi kikubwa sana. Nitatoa mifano michache jinsi ambavyo washindi wanaweza kunufaika na zawadi hizi kwa kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Baadhi ya watu wana mawazo mazuri sana ya kibiashara lakini wanakosa mtaji. Au labda kuna baadhi waliwahi kufanya biashara isiyofaa wakajikuta wanafilisika kwa namna moja au nyingine au huenda walipatwa na majanga mbalimbali kama vile moto, kuibiwa, au biashara zao kutaifishwa, n.k.

Sio siri kuwa rasilimalifedha ndicho kikwazo kikubwa katika masuala mazima ya uzalishaji mali. Hivyo basi, kwa wale watakaoshinda zawadi ya fedha taslimu au vifaa kama zilivyotangazwa kwenye orodha ya zawadi, wanaweza wakanufaika kiuchumi kwa kuzitumia kufanyia shughuli za uzalishaji mali zinazoingiza faida. Kuna aina nyingi ya shughuli kutegemea na mazingira anapokaa mshindi au shughuli alizozoea kufanya lakini naomba nitoe mifano michache na rahisi ya shughuli ambazo mshindi anaweza kuzifanya na zikamzalishia fedha za kutosha. Baadhi ya shughuli hizi ni kama ifuatavyo:

1. Kununua hisa
Ununuzi wa hisa ni biashara inayolipa ijapokuwa watanzania wengi hawaifahamu. Ni watu wachache sana wanaofahamu manufaa ya kununua hisa na jinsi gawio la hisa linavyoweza kuwanufaisha kiuchumi. Kwa kuwa zawadi ya fedha inaanzia Tsh 5,000,000 hadi Tsh 2,000,000, fedha hizi zinawatosha kabisa washindi kununua hisa kwenye makampuni au mabenki na kupata faida kubwa.

Hisa ni sehemu ya umiliki wa kampuni. Hivyo, hisa moja inawakilisha asilimia ndogo ya umiliki katika kampuni. Kama kampuni ina hisa milioni moja na mwekezaji anamiliki hisa 100,000 mwekezaji huyu anamiliki 1% ya kampuni. Mwekezaji anayenunua hisa basi ananunua haki ya kumiliki kampuni. Stahili za mwenye hisa ni pamoja na kushiriki katika kutoa maamuzi ya kampuni katika mkutano mkuu wa wanahisa na kupata gawio litokanalo na faida. Ana haki pia ya kuuza hisa zake kwa faida pale ambapo kuna ongezeko la thamani ya hisa.

Gawio ni malipo yanayofanywa na kampuni kwa wanahisa kutokana na faida ya kampuni. Malipo haya yanapendekezwa na wakurugenzi na kuidhinishwa na mkutano mkuu wa wanahisa. Gawio linaweza kulipwa kutokana na faida ya mwaka husika au malimbikizo ya faida za nyuma. Aidha, gawio linaweza kulipwa kwa fedha taslimu au kwa kuwaongezea hisa wanahisa.

Kwa hiyo, mshindi wa fedha za shindano la Stories of Change anaweza akaamua kununua hisa kwenye kampuni fulani, akawa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo na kujipatia gawio la hisa kila baada ya muda fulani kutokana na faida ya kampuni. Anaweza akachagua kuwekeza fedha zote (million 5, million 3 au milioni 2) au akawekeza tu sehemu ya fedha na kubakisha kiasi kingine kwa ajili ya shughuli nyingine.

2. Fixed depsoit
Ikiwa mshindi ataamua kutowekeza fedha kwenye biashara yoyote, anaweza kuziweka benki kwa muda atakaopenda (miezi, mwaka au miaka, nk) kisha akazichukua pamoja na faida. Mfano wa namna faida inavyopatikana kutokana na fixed deposit ni kama inavyoonekana hapo chini:

View attachment 1876901
Mfano wa faida ya kuweka fedha fixed deposit
Chanzo: Mtandao

Kwa mujibu wa kielelezo hapo juu, kwa mfano, mtu atakayeshinda Tsh 2,000,000 kama ataamua kuziweka benki kwa muda wa mwaka mzima atapata faida ya 3% ya fedha zake. Hii maana yake ni nini? Baada ya mwaka mmoja fedha zake zitakuwa zimeongezeka kwa asilimia tatu; sasa atachukua Tsh 2,060,000 na endapo utaamua kuacha zikae benki kwa mwaka mwingine zaidi, zitaongezeka hadi kufika Tsh 2,121,800. Utaona kwamba fedha zake zinazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka. Faida katika fixed deposit ni faida inayozaa ila unatakiwa uziache fedha zikae kwa muda mliokubaliana bila kuzichukua.

3. Biashara
Uwekezaji kwenye biashara ni eneo jingine ambalo mshindi anaweza kuamua kuwekeza. Kuna biashara za aina nyingi, kuanzia kufungua duka au genge hadi biashara za rejareja. Kwa mfano, ikiwa atachagua kufungua genge, basi anaweza ama kukodi fremu au kukodi eneo la wazi na kujenga banda la kawaida kwa ajili ya kuendeshea shughuli zake. Kiasi chochote cha fedha atakachoshinda – iwe million 5, million 3 au 3 – kinatosha kwa shughuli hii. Kwa mfano, ikiwa ataamua kufungua genge la mama au baba Ntilie, atatenga Tsh 150,000 akodi banda kwa miezi 3; Tsh 150,000 anunue sufuria, majiko, mkaa, mwiko na vifaa vingine vya kazi; na Tsh 300,000 anunue vipikio kama vile unga, mafuta ya kula, mchele, nyama, mboga, nk. Na kiasi kitakachobaki ataweka kama akiba kwa ajili ya dharula zitakazojitokeza. Sijaweka mshahara wa wasaidizi kwa kuwa wasaidizi wanalipwa kwa siku kulingana na makubaliano lakini malipo kwa mfanyakazi mmmoja kwa siku hayapindukii Tsh 4,000.

View attachment 1876902
Biashara ya mama Ntilie ni mojawapo ya biashara nyingi ambazo mshindi anaweza kuamua kufanya
Chanzo: Mtandao

Kana kwamba biashara ya mama Ntilie haitoshi, mshindi naweza pia kufungua biashara ya kuuza bidhaa kama vile nguo au akafungua duka la vyakula na mahitaji mengine ya nyumbani. Mtu ukiwa na mtaji huwezi kukwama kubuni biashara yoyote inayolipa ikakuingizia kipato cha uhakika.

4. Kilimo
Kilimo ni biashara kama biashara nyingine kwa sababu kinahusisha matumizi ya fedha na kinalenga kupata faida. Kulingana na eneo la kijiografia analotoka mshindi, anaweza kuamua achague zao moja la nafaka au bustani akalima kitaalamu na kupata faida kubwa.

Kinachowaponza wakulima wengi hata wasifanikiwe katika kilimo ni mtaji. Kwa kuwa sasa mtu atakuwa ameshinda fedha za mtaji, kitakachobaki ni kutafuta shamba na kujikita katika kilimo. Nashauri mtu asije akawekeza fedha kwenye kilimo kwa kufuata mkumbo. Kila mtu atataka kuwa mwalimu wa kukuchagulia zao la kulima. Kuwa makini; usikubali kila ushauri utakaopewa. Ukishapata fedha zako, kaa chini utulize akili na usome vizuri aina ya kilimo unachoweza kufanya kikakuletea faida na tija. Usikurupuke!

View attachment 1876903
Kilimo cha mboga
Chanzo: Mtandao

Kwa mfano, ikiwa unaishi kwenye eneo lenye mito na mabonde ya kutosha unaweza ukalima mahindi kwa kumwagilia wakati wa kiangazi halafu ukauza mahindi mabichi ya kuchoma (maarufu kama gobo). Biashara ya mahindi ya kuchoma imeshamiri kila mahali, hasa maeneo ya mjini, hivyo soko lipo. Kinachotakiwa tu ni kuweka ratiba zako za kilimo vizuri kuhakikisha wakati wa mavuno hakutakuwa na mahindi mengi sokoni. Mbinu moja kubwa ni kulima kilimo cha kumwagilia ili uwe na uhakika wa kuuza mahindi wakati wowote bila kujali kama mvua imenyesha au la.

Unaweza kulima kwa kutumia mtaji kidogo na kupata faida. Angalia mchanganuo ufuatao: kukodi shamba ekari moja inagharimu wastani wa Tsh 50,000/=, kulima Tsh 30,000/=, kupalilia Tsh 30,000/=, mbolea mifuko 3, Tsh 150,000/= na madawa Tsh 50,000/=. Jumla kuu ni Tsh 310,000/=.

Kwa ekari moja, ukilima kwa kuzingatia utaalamu una uhakika wa kuvuna kuanzia mahindi 9,800. Hindi moja huuzwa kwa Tsh. 150/= hadi 250/=, kutegemea hali ya soko kwa bei ya jumla. Ukikokotoa utaona kuwa kwa ekari moja unaweza kupata Tsh 1,470,000/= kwa makadirio ya chini na Tsh 2,450,000/= kwa makadirio yaa juu. Ukitoa gharama za uendeshaji (za moja kwa moja) unaweza kukunja faida ya hadi Tsh 2,140,000/= kwa makadirio ya juu. Je, ukilima misimu kadhaa bado utashindwa kujenga nyumba ya maana au kuwa na maisha yenye unafuu? Bila shaka utaweza!

View attachment 1876904
Shamba la mahindi yaliyopandwa kitaalamu
Chanzo: Mtandao

Mbali ya kilimo cha mahindi, kilimo cha nyanya nacho kinalipa. Utaratibu wa ulimaji wa zao hili hautofautiani na ule wa kilimo cha mahindi. Mimea ya nyanya haistahimili mvua nyingi kwa kuwa mvua huchochea magonjwa ya ukungu. Mkulima mzuri wa nyanya ni yule anayelazimisha kulima wakati wa msimu wa mvua kwa sababu wakati huo wakulima wengi hushindwa kuhudumia zao la nyanya. Ijapokuwa utatumia gharama kubwa lakini utauza mazao yako kwa bei ya juu itakayokuingizia faida kubwa zaidi. Hivyo, zao mojawapo ambalo mshindi wa zawadi ya fedha kutokana na shindano la Stories of Change anaweza kulima na kumletea faida kubwa ni zao la nyanya.

5. Ufugaji
Kama ilivyo kwenye kilimo, ufugaji nao ni biashara nzuri iwapo utachagua aina ya ufugaji unaoumudu kulingana na eneo lako la kijiografia, kiasi cha mtaji au uwepo wa eneo. Kuna ufugaji wa ina nyingi unaowezekana kufanyika hapa nchini ukiwemo ufugaji wa nyuki, kuku, mbuzi na mifugo mingine. Aina ya mifugo ambao wanafugika kirahisi ni kuku, hasa kuku wa asili, chotara, au nyama. Ufugaji wa kuku ni mzuri zaidi kwa kuwa hauhitaji gharama kubwa na unaweza kufanyika kwa namna nyingi kutegemea rasilimali ulizonazo. Katika maelezo yangu nitajikita zaidi kwenye ufugaji wa kuku wa nyama.

View attachment 1876905
Ufugaji wa kuku wa nyama
Chanzo: Mtandao

Ufugaji wa kuku wa nyama ni rahisi kwa kuwa vifaranga wa nyama hufikia umri wa kuuza baada ya mwezi mmoja (siku 30) tu! Kwa kuanzia, unaweza kuanza na kuku wa nyama wapatao 200 ambao utawanunua kwa wastani wa Tsh 1,500 kwa kila kifaranga mmoja. Hivyo, vifaranga 200 watagharimu Tsh 300,000. Gharama za vifaa kama vile vyombo vya kulishia na kunyweshea maji vinaweza kugharimu Tsh 50,000. Gharama za vyakula tangu wakiwa wadogo (chick starter) hadi wanafika umri wa kuingia sokoni (finisher) zinakadiriwa kufika Tsh 600,000. Kama huna banda unaweza kukodi kwa Tsh 50,000. Jumla ya gharama zote ni Tsh 1,000,000. Kama utazingatia kanuni za ufugaji bora, hadi kufika wakati wa mauzo utakuwa na kuku 195 (watano tu watakufa). Kuku mmoja wa nyama huuzwa wastani wa Tsh 8,000. Hivyo jumla ya mauzo itakuwa Tsh 195x8000 = 1,560,000. Jumla ya faida = 1560000 -1,000,000 = 560,000.

Utaona kwamba gharama za kufuga kuku 200 wa nyama zinaangukia ndani ya zawadi zote za ushindi. Ikiwa mshindi yeyote atashindwa kutumia zawadi yake kufugia na kujiongezea kipato, huo utakuwa uzembe wake binafsi. Mshindi yeyote (nikiwemo mimi) akiamua kutumia fedha hizo kwa matanuzi hadi zikaisha, asije akatafuta mchawi kwani mchawi ni yeye (au mimi) mwenyewe.

5. Urahisi na unafuu wa mawasiliano
Tusisahau pia vifaa vya mawasiliano (simu, tablet na laptop) ni sehemu ya zawadi kemkem zitakazotolewa na kampuni ya Jamii Media kwa baadhi ya washindi. Vifaa hivi vitawasaidia washindi kurahisisha na kupata unafuu wa mawasiliano. Kwa mfano, ikiwa mshindi alikuwa akilazimika kwenda kulipia muda kwenye mgahawa wa intaneti, sasa atakuwa anapata mawasiliano kiganjani mwake. Atakachohitaji tu ni kununua modemu ya kuchomeka kwenye laptop na kuijaza bando au kutiririka moja kwa moja kutoka kwenye simu au tablet yake. Hii itamuongezea unafuu na urahisi wa mawasiliano, hivyo kufanya maisha yake kuwa bora zaidi ukilinganisha na zamani. Aidha, urahisi na unafuu huu utamuongezea chachu ya kushiriki na kushinda shindano la awamu ya pili la Stories of Change kutoka hapa hapa JF.

6. Umaarufu
Zawadi ya Ubalozi wa Jamii Forums itamuongezea mshindi umaarufu kwa kuwa atatangazwa katika mitandao yote ya JF na mbele ya vyombo vingine vya habari wakati akitangazwa kuwa balozi. Kitendo hiki kitampa umaarufu mkubwa sana kwani atafahamika kwa watu wengi ndani ya muda mfupi. Umaarufu huu utamsaidia kupata koneksheni na watu wengine maarufu nchini na dunia nzima kwa ujumla, hivyo kumuongezea thamani ya kijamii (social value).

Kwa kumalizia, nawaomba wote mtakaofanikiwa kuusoma huu mnakasha mnipigie kura kwa kubonyeza kitufe hiki hapa chini kinachopatikana upande wa juu, kulia mwa mnakasha wangu. Huenda nikafanikiwa kunyakua hili donge nikalitumia kama nilivyoeleza hapo juu

View attachment 1876885

Mbarikiwe sana wapendwa wanaJF mnapojiandaa kunipigia kura zenu za ushindi.

Asanteni.​
Zawadi hizi zitakazotolewa si haba ndugu zangu; yeyote atakayeshinda akizitumia vizuri zitamtoa kimaisha.
 
Tafadhali ndugu zangu wanaJF naomba mniunge mkono kwa kunipigia kura kwa kugonga hapo nilipoonyesha kwenye screenshot. Mpaka sasa nina kura moja tu; natia huruma sana aisee! Mbarikiwe sana 🙏
View attachment 1877957
Ndugu wanaJF upigaji kura bado unaendelea. Naomba muendelee kuniunga mkono kwa kura kwenye andiko hili. Bado kura hazitoshi wandugu zangu. Mbarikiwe sana mnapojiandaa kunipigia kura 🙏
 
Back
Top Bottom