Je, ulishiriki Stories of Change? Tafadhali angalia PM yako

JamiiForums

Official JF Response
Nov 9, 2006
6,200
4,979
Katika mpango mkakati wa JamiiForums (JF) wa miaka 5 (2020-2024), JF ilidhamiria kuendesha shindano lenye kuwawezesha wananchi kushiriki katika kuongeza ubora wa maudhui ya Kiswahili yenye kuchochea mabadiliko. Shindano hili lianza rasmi mwaka 2021 na huendeshwa kila mwaka.

Mwaka 2023 kuanzia Mei Mosi, JF ilianza kupokea maandiko ya Stories of Change kwa siku tisini. Shindano lilifungwa Julai 31, na mchakato wa kuchuja maandiko ulianza muda huo ili kupata maandiko bora yatakayojishindia kitita cha takriban Tsh. milioni 20.

Kwa sasa JamiiForums inaendelea na mchakato wa kuandaa sherehe ya kuwapa tuzo washindi wetu ambao tayari wameshapatikani.

Je, wewe ulishiriki shindano la 'Stories of Change'? Tafadhali ingia PM kuona kama wewe ni mmoja wa washindi wetu ili upate maelekezo zaidi namna ya kushiriki sherehe ya utoaji tuzo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom