Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

ArIeN

ArIeN

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2017
Messages
8,301
Points
2,000
ArIeN

ArIeN

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2017
8,301 2,000
Binafsi enzi hizo nilikua napiga kwa sequence maalum.
Kwanza nilianza kwa kupiga push ups za kutanua kifua. Ambazo unapanga matofali mawili kushoto na kulia kwako au vipande vya mbao kisha unakua mikono waiweka juu na kupiga push-ups huku kifua kikiingia katikati.
Nilikua napiga push-ups 50 na nilienda mizunguko 6.
Break ya round na round nilikua na piga squats 100.

Zoezi namba 2 nilikua napiga push-ups za kubana kifua huku mikono nikiibana level ya mabega napo idadi ya push-ups ni kama round one na reps ni sita.

Zoezi namba tatu hapa nilikua naikutanisha mikono kisha natengeneza shepu kama ya kopa.
Nilikua napiga push-ups 3 in 1(yani kila push ups tatu nilizihesabu kama moja) huku kila nikishuka chini kifua kina gusa ile kopa.
Zoezi hili lilikua maalum kwa kujenga msuli wa nyuma ya mkono, kujenga kifua cha juu na kuziba yale matundu ya shingoni,kuujenga mgongo na kua na mwonekano wa kupasuka pasuka.
Nilikua napiga push-up 20 na round 5.

Baada ya hapo nilipiga Zoezi la kujenga shoulders ambalo mara nyingi niliipigia kitandani.
Unachuchumaa kitanda kikiwa nyumba yako kisha mikono una irudisha nyuma na kushika ubao wa kitanda.
Zoezi hili unapiga taratibu na unatakiwa upige push ups hizi 60 *5.

Ukimaliza unaenda mlangoni na kupiga pull ups kwa ajili ya kujenga msuli wa mbele ya mkono.
Pia weza ligeuza kujenga msuli wa nyuma ya mkono.

Baada ya kushughulikia sehemu zote nilikua napiga zoezi la kutengeneza six packs.
Hili zoezi ni gumu kulielezea ila unakaa chini.
Kisha unainyanyua miguu yako unakua kama V. Baada ya hapo unaweka mikono yako kifuani na kuanza kupeleka miguu mbele kama unasukuma kitu bila kuishusha. Unapiga mbele 30,kushoto 30,kulia 30 then unageuka na kupiga push-ups 100 za basketball ili kujenga misuli ya mkono wa chini, zile nyama chini ya kiwiko chako.

Then unahamia kwenye mazoezi ya miguu ukimaliza unajikumbushia kata mbili tatu za wingchun then unapiga sparring na swahiba wako kujiweka fiti tu.
bro u a beast!!!
 
Masokwe

Masokwe

Member
Joined
Mar 30, 2019
Messages
70
Points
125
Masokwe

Masokwe

Member
Joined Mar 30, 2019
70 125
hivi unaweza kukata tumbo kwa mazoezi bila kuacha misosi kama wali na ugali ????
 

Forum statistics

Threads 1,336,421
Members 512,614
Posts 32,538,927
Top