Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,279
Ningependa kuongeza kuwa, katika yale mapambano ya mwili na ubongo katika vita ya kuacha kuvuta sigara, unaweza kupitia hali ya msongo wa mawazo (depression), uwezo wa kufikiri kupungua au kupata shida wakati wa kufiri, akili kutokutulia pia insomnia. Faida zinazoenda sambamba na kuacha kuvuta sigara ni pamoja na kupungua uzito, katika tafit zilizofanywa na Wizara ya Afya ya Uingereza (NHS), zinaeleza kuwa uzito wa kilo 4/5 hupungua katika miezi 12 ya kuacha kuvuta sigara.
Mwili unapokosa nicotine pia humfanya mvutaji mzoefu kusikia kuzunguzungu, dalili za mafua na myalgia. Kama hali ni ngumu sana kuihilimili unaweza kumuona daktari ambae atakupa dawa za antidepressant tablets utakazotumia kwa muda kama bupropian.