Bangi inasababisha mshtuko wa Moyo

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Utafiti mpya uliofanyika nchini Marekani umegundua kuwa kuvuta au kula bidhaa zozote zenye bangi husababisha athari kubwa kwenye moyo wa Binadamu kama vile kupata mshtuko wa moyo pamoja na kiharusi na yote haya hutokea hata kama Mtu hakuwa na magonjwa ya moyo na hajawahi kuvuta sigara hapo zamani.

Utafiti huo pia uligundua kuwa hatari ya kupata ugonjwa wa kiharusi kwa wanaotumia bangi kila siku ya maisha yao uliongezeka kwa 42% na hatari ya mtu kupata mshtuko wa moyo pia kwa anaevuta kila siku iliongezeka kwa 25% ambapo liliongezeka kadri idadi ya siku za matumizi ya bangi zilivyoongezeka.

Robert Page II, Profesa wa Chuo Kikuu cha Colorado Skaggs School of Pharmacy na Sayansi ya Madawa huko Aurora, Colorado alisema ongezeko la matumizi ya bangi yamehusishwa na mshtuko wa moyo pamoja na ugonjwa na kiharusi ambapo Vijana wa makamo walio chini ya miaka 55 na Wanawake chini ya umri wa miaka 65 ambao walitumia bangi walikuwa na hatari kubwa ya 36% kupata magonjwa ya moyo, mshtuko wa moyo na kiharusi bila kujali kama walitumia pia bidhaa za kitamaduni za tumbaku kama vile sigara.

Taasisi ya magonjwa ya Moyo nchini Marekani inawashauri Watu kujiepusha na uvutaji wa sigara na bangi au kula vyakula vilivyowekewa bangi ikiwa ni pamoja na bidhaa za bangi kwa sababu ya madhara yanayoweza kutokea kwenye moyo, mapafu na mishipa ya damu.

Credit - MillardAyo
 
Inawezekana, kuna msimu nilikua nikila hiyo mambo nikitoka nje kwenye fresh air nilikua nahisi kukata moto kabisa......
 
Why why these people who want to do so much good for everyone who call themselves government and this and that, why they say you mustn't use the herb 🌿.

Herb is a plant you know if me check reason there's no reason to make it illegally.

-Robert Nesta Marley
 
hii kitu ni kweli kuna kipindi cha nyuma sana nilikua na rafiki yangu jioni tukitoka kujitafuta tunakutana geto kwangu au kwake tunakula mjani wa bob.

basi siku moja jamaa akala vinu ilikua jumapili mchana feni inawaka hewa ipo geto vizuri tu katika moja na mbili jamaa akaamka kwenye kochi akaenda kunywa maji ghafla nilishangaa jamaa anaanguka nikajua utani akawa anahangaika chini kama nusu dakika hivi ndipo akanyanyuka namuuliza vipi mzee ndio nn hio ananijibu aliona kama giza ila alikua ananisikia ninavyomwambia acha utani , niliogopa sana nikaamua kupunguza kula mjani jamaa alikuja kupata tatizo la kuanguka kama kuzimia kwa dakika kadhaa akashauriwa aache na hakulata tatizo tena...

bhange kwa starehe ni kitu nzuri ila isiwe kila muda kila siku ukipiga mara moja moja kwa wiki sioni kama kuna ubaya
 
Back
Top Bottom