Jinsi ya kuacha kuvuta sigara (A Guide to Quitting Smoking)

Ni kweli mtungi unahamasisha sana kurudia uvutaji kwa mtu aliyeacha. Lakini ukitaka kuacha kabisa tangazia wenzako unaokunywa nao kwamba umeacha sigara halafu uwaonyeshe sigara na kiberiti ulichonacho. Wengi wataku congratulate na hilo litazidi kukupa moral support
 
Ndugu mi naendelea kupuyanga tu we kaa uniambie ngoja sijui nishibe,cjui nifurah au nichukie ila mi Nazid kukimbia tu muda si mrefu natimiza masaa 72 mdogo mdgo nasahau.
Sigara ina tabia moja, kuwa likizo na kurudia, ila 72hrs ni mda ambao hamu ya kuvuta inaisha kabisa, unaweza ukaacha miezi kadhaa siku ukakutana na mtu usiyetarajia kama anavuta, mtu ambae unamheshimu kweli kweli ukashangaa anavuta na wewe ukajikuta una mssuport, sigara kama uchawi sijui! Anyway, hongera kwa kuacha, epuka chama choma mara kwa mara, kaa na kampani ya watu ambao hawapendi kabisa hiyo kitu. Anaza mazoezi mepesi kama kukimbia au kuruka na kamba.
 
Nyie ndio mnaorudisha maendeleo nyuma,
ulifika idadi nzuri sana ya sigara kwa siku, sigara 40.
kwa hesabu za haraka haraka 40*150=6,000 kwa siku.
ukivuta kwa mwezi mmoja yani 6,000*31=186,000 ambacho ni mshahara wa kima cha chini cha mfanyakazi mmoja pale TCC, hasa ulivyoacha unataka jamaa akose mshahara ili afukuzwe kazi..!!!?
tuweni na huruma, at least ungeongeza kutoka 40-50 nngekuona wa maaana, na uchumi wa nchi kumbuka unadidimia.
 
Nina miaka mitano sasa tangu nimeacha sigara na pombe ingawa ilinipunguzia marafiki zangu wale walevi.

Hongera mkuu jiandae tu kisaikolojia kuwa unaweza kuacha wala wasikuvunje moyo hao wanaosema ni ngumu kila jambo likitiliwa nia huwa jepesi sana.

Ila nia yako iendane na vitendo vyako pia.
 
mkuu umenishtua nilivyoona heading..

mimi niliacha tangu tarehe 1 january 2017 baada ya kuvuta kwa miaka 15, ila naibibia kwa wiki mara moja ili niache vzr...

ila embasy wewe, madukani mpka walinitungia jina, et mzee wa embasy
 
Pombe nimeacha toka mwaka 2005,na uzur nmeamua kupunguza aina za marafiki nilionao,sasa sigara nilikua sijaamua ila sasa nmeamua Rasmi,bila pombe,bila sigara,maisha yanasonga bila stress...marafiki wachache wanaojielewa,mke mmoja furaha moja
Hongera sana kwa maamuzi mazuri chief,umechagua maisha mazuri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom