SI KWELI Uvutaji sigara husaidia kuondokana na msongo wa mawazo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mara nyingi nikiwa na stress na kupelekea kukosa usingizi, huwa navuta sigara ili kupunguza stress hizo. Hata iwe usiku wa manane nitajitahidi niende kwenye Club zinazokesha nikafuate sigara.

Suala la kuwa inanisaidia au lah, sidhani lakini pale napokuwa navuta huwa nakuwa katika hisia nyingine kabisa. Chanzo cha kutumia sigara kama relief ya stress, ni baada ya kuona kwenye muvi mara kwa mara, na ushauri kutoka kwa marafiki.

Nachotaka kujua kitaalam ni kama kweli sigara inasaidia kupambana na msongo wa mawazo tunaokumbana nao mara kwa mara.

Signs-of-stress.jpg
 
Tunachokijua
Kuvuta sigara ni kitendo cha kuingiza mwilini moshi wa tumbaku uliofungwa katika sigara. Watu hufanya hivyo kwa kuiweka sigara mdomoni na kuiwashia mwisho wake ili kuvuta moshi wa kemikali mbalimbali zilizomo ndani ya tumbaku.

Mashirika ya makubwa ya Afya Ulimwenguni ikiwamo Shirika la Afya Duniani (WHO) na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa Marekani (CDC) wanakubaliana kuwa uvutaji wa sigara una madhara makubwa kiafya ikiwamo kupata magonjwa katika mfumo wa upumuaji, Kupata Kansa ya Mapafu na kuwa katika hatari ya kushambuliwa na magonjwa mbalimbali.

Msongo wa mawazo ni hali ya mtu kuzongwa na mawazo hasi ambayo mara nyingi hupelekea matokeo mabaya Kwa muhusika hasa pale asiposaidiwa au asipojisaidia kutoka kwenye changamoto hiyo.

Kama alivyoeleza Mdau wa JamiiCheck hapo juu, kumekuwapo na hoja za Wadau mbalimbali wakidai kwamba uvutaji wa sigara husaidia kuondoa msongo wa mawazo na kuleta utulivu pindi wanapokukosa utulivu au kuzongwa na mawazo hasi. Aidha, JamiiCheck imefuatilia na kubaini kuwa madai haya ni maarufu duniani na yamewahi kuongelewa na kuchambuliwa na kurasa mbalimbali mtandaoni. soma: (hapa).

Je, kuna ukweli kwamba sigara ina uwezo wa kuondoa msongo wa mawazo?
JamiiCheck imefuatilia vyanzo mbalimbali vya Afya ikiwamo HealthHub.sg, Taasisi ya Afya ya Akili Ulaya na My Health Alberta na kubaini kuwa vyote havikubaliani na hoja ya kuwa Uvutaji wa sigara husaidia kuondoa na msongo wa mawazo kwa mvutaji.

Mathalani, HealthHub.sg wanakanusha hoja ya sigara kusaidia kuondoa msongo wa mawazo kwa kutoa. HealthHub.sg wanaamini uvutaji wa sigara ndiyo chanjo kikuu cha kuongeza msongo wa mawazo na si kupunguza. Katika kufafanua hoja yao HealthHub.sg wanatoa sababu tano za namna ambavyo sigara inachochea kuongezeka kwa msongo wa mawazo kuliko kupunguza. Katika andiko lao wanaeleza:

Sigara ile unayovuta ukijaribu kupunguza mawazo inaweza kukuletea mawazo zaidi na kwa muda mrefu. kuna sababu tano jinsi uvutaji sigara unavyoweza kuongeza badala ya kupunguza mafadhaiko katika maisha yako, 1. Kupunguza mawazo ni suala la kusadikika, 2. Uvutaji wa sigara unagharimu pesa, 3. Uvutaji sigara unahatarisha afya ya mvutaji, 4. Uvutaji wa sigara huaribu mahusiano na watu wako wa karibu, 5. Uvutaji wa sigara una Uraibu.

Kwa upande wao, Taasisi ya Afya ya Akili Ulaya wao wamekuja na utafiti unapinga hoja ya kuwa uvutaji wa sigara huondoa msongo wa mawazo kwa kudai unaongeza mafadhaiko kwa mvutaji. Katika utafiti wao wamebaini kuwa uvutaji wa sigara unaongeza mafadhaiko kwa mvutaji badala ya kupunguza. Sehemu ya andiko lao inaeleza:

Baadhi ya watu huvuta sigara kama 'dawa ya kujitibu' ili kupunguza hisia za mafadhaiko. Hata hivyo, utafiti umedhihirisha kuwa uvutaji sigara unazidisha wasiwasi na mafadhaiko. Nikotini husababisha hisia ya utulivu mara moja, hivyo watu huvuta sigara wakiwa na imani kwamba inapunguza mafadhaiko na wasiwasi. Hata hivyo, hisia hii ni ya muda mfupi na hivi karibuni inachukuliwa na dalili za kuondokana na utegemezi na hamu kubwa ya kuvuta sigara. Uvutaji sigara hupunguza dalili za kuondokana lakini haujapunguza wasiwasi au kutatua sababu ambazo mtu anaweza kuhisi hivyo.

Nao, My Health Alberta wametoa mtazamo wao kwa kueleza kuwa uvutaji wa sigara hausaidii kabisa kupunguza mawazo isipokuwa huwatuliza wavutaji kwa muda baada ya kemikali ya Nikotini kuingia kwenye ubongo na kisha utulivu huo huisha baada ya muda mfupi. Katika andiko lao wanaeleza:

Kuvuta sigara si suluhisho la muda mrefu kwa kutatua mafadhaiko, mvutano, au unyogovu. Utulivu unaoupata kutokana na kuvuta sigara hutokana na kitendo cha kutenga muda wa kuvuta sigara na athari za nikotini kwenye ubongo wako. Ikiwa utarudi kwenye hali ya mafadhaiko baada ya kumaliza kuvuta sigara, haichukui muda mrefu kabla ya mafadhaiko yako kurudi. Na kisha utahitaji sigara nyingine.
Zaidi ya hayo, JamiiCheck imefanya mawasiliano na Mtaalamu wa Afya na mtafiti Dkt. Isaac Maro ambaye pia amepinga madai ya uvutaji wa sigara kusaidia kuondokana na msongo wa mawazo. Akiifafanulia JamiiCheck Dkt. Maro amesema:

Tafiti rasmi zilizofanyika Duniani zinaonesha kuwa Wavutaji wa Sigara wanaamini wanapovuta wanaondolewa msongo wa mawazo, hilo ni suala la hisia tu.
Kila mtu ana kitu ambacho kinampa faraja, mfano sigara ina kitu kinaitwa Nikotini (Nicotine) na ndio inafanya watu wanakuwa ‘addicted’, ni kama ilivyo kwa ‘alosto’, hivyo mvutji akiikosa anahisi kuna kitu hakipo sawa mwilini mwake. Anapokosa ndipo anapoanza kupata ‘stress’ (msongo wa mawazo), hivyo akipata sigara na kuvuta ndipo anahisi stress zake zimeisha lakini kiuhalisia zinazoisha ni zile zilioongezeka wakati amekosa sigara (alosto).
Utafiti unaonesha wavuta sigara wana vichocheo vikubwa vya msongo wa mawazo kuliko wale ambao hawavuti kutokana na wingi wa Nikotini. Mvutaji anahitaji Nikotini ili kupunguza stress, anapofanya hivyo nahisi ameziondoa lakini kiuhalisia sio hivyo, ni suala la hisia tu.

Hivyo, kutokana na vyanzo hivyo pamoja na ufafanuzi kutoka kwa Mtaalamu wa Afya JamiiCheck inaona kuwa hoja inayodai kuwa uvutaji wa sigara husaidia kuondoa msongo wa mawazo haina ukweli.
Mara nyingi nikiwa na stress na kupelekea kukosa usingizi, huwa navuta sigara ili kupunguza stress hizo. Hata iwe usiku wa manane nitajitahidi niende kwenye Club zinazokesha nikafuate sigara.

Suala la kuwa inanisaidia au lah, sidhani lakini pale napokuwa navuta huwa nakuwa katika hisia nyingine kabisa. Chanzo cha kutumia sigara kama relief ya stress, ni baada ya kuona kwenye muvi mara kwa mara, na ushauri kutoka kwa marafiki.

Nachotaka kujua kitaalam ni kama kweli sigara inasaidia kupambana na msongo wa mawazo tunaokumbana nao mara kwa mara.

Ningeomba basi andiko hili pia kuongelea ni namna gani ya kupunguza stress na kuondoa kukosa usingizi ili kumsaidia mletaji bandiko na wasomaji wengine.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom