China yaendelea kuwa nguzo kwenye mafungamano ya uchumi duniani

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,035
VCG41N1008939110.jpg


Katika siku za hivi karibuni mkutano wa Baraza la Uchumi wa Dunia kwa mwaka 2024 ulifanyika huko Davis, Uswisi. Waziri mkuu wa China Li Qiang aliiwakilisha China kwenye mkutano huo, na kutoa hotuba muhimu ambayo sio kama tu iliendelea kutoa imani kwa jumuiya ya wachumi duniani, bali pia ilithibitisha dhamira ya China ya kuwa mdau muhimu kwenye mafungamano ya uchumi duniani.

Mkutano wa baraza la uchumi wa dunia wa Davos, ni moja ya mikutano muhimu duniani ambapo wadau wakubwa wa uchumi wanakutana na kujadili changamoto, fursa na mustakbali wa uchumi wa dunia. Katika muda mrefu uliopita nchi za magharibi ndio zilikuwa wadau wakubwa wa kwenye masuala ya uchumi, lakini katika miaka ya hivi karibuni China imekuwa ni mdau muhimu katika mkutano huo. Kila mwakilishi wa China anapoongea kwenye mkutano huo, kunakuwa na ufuatiliaji mkubwa kutoka kwa wadau wa uchumi duniani.

Kwenye mkutano safari hii wa Davos, Waziri Mkuu Bw. Li Qiang kwenye hotuba yake alitangaza mpango wenye vipengele vitano, ukiwemo uratibu wa sera za uchumi mkuu, utaalamu wa kimataifa wa viwanda na ushirikiano, ushirikiano katika uvumbuzi, ushirikiano katika maendeleo ya kijani, na ushirikiano wa kaskazini-kusini na kusini-kusini. Mambo aliyotaja waziri mkuu Li ni mambo ambayo kimsingi yanapewa msukumo na China, lakini pia yanaonesha kuwa China inaendelea na dhamira yake ya kutoa mchango mkubwa kwenye mafungamano ya uchumi duniani.

Ikumbukwe kuwa katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na sababu mbalimbali, iwe ni za kisiasa, kiusalama, mazingira au maendeleo ya sayansi na teknolojia, kumekuwa na mdororo wa uchumi katika sehemu mbalimbali. Baadhi ya nchi za magharibi ambazo zilikuwa ni wasanifu wa mafungamano ya kiuchumi duniani, zimegeuka na kuwa mstari wa mbele katika kuweka sera za kujilinda kibiashara, na hata kuathiri zaidi uchumi wa dunia. Lakini China imekuwa ikipaza sauti zaidi katika kuhimiza mafungamano, na hata kutoa fursa nyingi za biashara ya uwekezaji kwa nchi hizo za magharibi

Waziri Mkuu Li Qiang alitoa wito wa ushirikiano wa kimataifa katika maeneo mbalimbali ili kujenga upya uaminifu wa kimataifa, akionya kwamba kukosekana kwa uaminifu na mgawanyiko kutahatarisha ukuaji wa uchumi wa dunia na maendeleo. Amekumbusha kuwa kwa mwaka 2023 uchumi wa China ulikuwa kwa asilimia 5.2, na kwamba uchumi unaendelea kuimarika, na kuahidi kuwa China itaendelea kuwa wazi na kutoa soko zaidi kwa biashara za kimataifa, bila kujali jinsi gani hali ya kimataifa inavyobadilika. Kauli hii ya Waziri mkuu ni msisitizo kuwa China itaendelea kutumia maendeleo yake kwa manufaa ya wengine, na kuwa nguzo muhimu ya uchumi katika wakati huu wenye sintofahamu nyingi kiuchumi.

Sio siri kuwa Marekani imekuwa bingwa wa sera za kiliberali za uchumi, na kuna wakati ilikuwa ikijinadi sana kuwa sera hizo zimeleta neema duniani, lakini ajabu ni kuwa ni Marekani hiyo hiyo ambayo sasa inaonekana kuwa kinara wa kuweka sera zinazokwenda tofauti kabisa na ambacho imekuwa inaimba sana. Ni wazi kabisa kuwa dunia ina mabadiliko makubwa, China bila shaka imekuwa ni nguzo muhimu katika uchumi wa dunia, ikiwa na asilimia 18 ya uchumi wa dunia ikifuata Marekani yenye asilimia 25. Kutokana na mafungamano makubwa ya kiuchumi na nchi mbalimbali duniani, uchumi wa China unagusa maisha ya watu wengi wa kawaida duniani kuliko ule wa Marekani. Kama kila nchi inafanya juhudi ya kujiendeleza, kupata maendeleo ndio matokeo ya mwisho, kwa hiyo kujaribu kuweka sera za kuzuia wengine, ni kujiweka mwenyewe vikwazo kwenye mambo ya biashara lakini pia unawaweka hatari kwa wengine, na kufanya uchumi wa dunia kudorora.
 
Back
Top Bottom