Jinsi binti niliekutana nae kwa miezi mitatu alivyotaka kunibambikizia mimba ya miezi 4, Teknolojia ilimuumbua kwa uhuni wake wa kienyeji.

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Habari zenu wana JF, Nikiwa nimejawa maumivu na majonzi ya kisa hivi naandika kwa lengo la kuelimisha tu lakini kiukweli hata navyoandika sasa sina raha kabisa nikikumbuka usaliti huu.

Kipindi hicho kwa muda wa takribani miezi mitatu nilikuwa single, Nikaja kuukwaa kwa binti flani age 26 mimi nikiwa na 29, Mapenzi yalianza kuchipua kama uyoga, yakanoga sana tukaanza kulala pamoja na mifikicho si haba.

Binti akaanza kuniambia ana mimba yangu na kiukweli nami nilianza kuamini ni yangu maana hata elimu ya mimba sina sana nilichojua tu kwavile nimetema ndani navuna nilichopanda, nilifatilia kidogo mambo ya timing nikaona ni kama imewahi mno ila nikapuuzia.

kuna rafiki flani nilikuwa napenda kununua mahitaji ya nyumbani kwake na tukawa tunapiga story akanijuza kwamba huyo mwanamke nayetembea nae si muda mrefu aliachana na mtu aliekuja kufanya kazi katika mkoa huu na kisha kuondoka, Taa iligonga kengele akilini nikaunganisha na ile hali ya kuhisi mimba imewahi, Nikawa assured kabisa kwamba mimba nayoilea sio yangu.

Niliongea na rafiki yangu mwengine kaelimika haya mambo akaniambia tukapime mashine za atra sound tujue mimba ina miezi mingapi ila nimzuge huyo mwanamke kwa uwongo wowote.

Basi siku ikafika, rafiki alishasaidia kuniunganisha na watu wa hospitalini, nilimdanganya mwanamke kwamba tunaenda kucheki afya ya mtoto hivyo nae alikubali.

Majibu yalitoka kwamba mimba ina miezi minne lakini cha ajabu tulianza kusex miezi mitatu iliyopita.

Nilificha hali ya kupanick nilitulia, tulipofika nyumbani ndio nikaanza kumbana sana akiri ujinga alionitendea na wala sikumpiga wala kumgusa, alikuwa anabisaha sana ila nilipomwambia kuhusu huyo mwanaume walieachana muda mfupi kabla ya mahusiano yetu alikiri lakini hakukubali mtoto ni wao

ilibidi nimchanganye kiakili niwe romantic mno kwa siku 2 zijazo kumwambia nipo tayari kulea mtoto hata kama sio wangu maana na mimi nina mtoto wa nje (uongo), basi nae akaingia kingi akasema ni kweli mtoto sio wangu na muda huo namrekodi kwenye simu iwe ulinzi wangu wa mapema hata akija kuzaa mtoto sitaki usumbufu wa mahakamani kupima dna maana inaleta aibu watu wengi kujua kwamba nimechapiwa.

Nataka niseme kwamba alipoingia kingi na huo ndio ukawa mwisho wetu hata wa kuonana,

Nyumbani nilimtimua licha ya yeye kulia machozi lakini ndio hivyo tena alizingua sana kwa alichotaka kunifanyia.

Mimba aliitoa na wala sijui hela aliipata wapi.

Hio ndio story yangu wakuu, Leo hii ningekuwa nalea mtoto ambae si wangu,
 
Habari zenu wana JF, Nikiwa nimejawa maumivu na majonzi ya kisa hivi naandika kwa lengo la kuelimisha tu lakini kiukweli hata navyoandika sasa sina raha kabisa nikikumbuka usaliti huu.

Kipindi hicho kwa muda wa takribani miezi mitatu nilikuwa single, Nikaja kuukwaa kwa binti flani age 26 mimi nikiwa na 29,

Inawezekana pia ilikuwa yako
 
Yani mimba tu mnaipeleka MRI? MRI hii nayoijua? Niliyoionaga pale Rabinnsia Hospital??

Ni MRI mkuu au ultrasound?

# sijui kama MRI inapima na umri wa mimba. Ila ile machine inaogofya 🤔
 
Wanaume,

Mbegu zako za kiume zikishaingia kwenye Mwili wa Mwanamke, zinakuwa ni Mali ya Serikali. Matokeo yatayofuata hapo ni mateso kwako Mwanaume chini ya mkono wa sheria.

Narudia kusisitiza tena, Hakikisha unatumia kinga kila wakati. hadi utapokuwa tayari kupata Mtoto.

Ila kwakuwa mmechagua kujifunza kwa vitendl, acha yawakute.
 
Yani mimba tu mnaipeleka MRI? MRI hii nayoijua? Niliyoionaga pale Rabinnsia Hospital??

Ni MRI mkuu au ultrasound?

# sijui kama MRI inapima na umri wa mimba. Ila ile machine inaogofya 🤔
Umenisahisha vema mkuu, ni atra sound
 
Back
Top Bottom