04mdete
New Member
- May 6, 2019
- 3
- 1
Iko poa sana.
Habari wakuu ! Natumaini wote ni wazima wa afya , kwa upande wangu niko poa . Sasa twende moja kwa moja kwenye mada yetu .
View attachment 1031445g
Tenses huelezea wakati au muda tendo linafanyika , lilifanyika au litafanyika .
Katika kiingereza kuna tenses ( nyakati ) kuu tatu , ambazo ni :
The present tense ( wakati uliopo)
The past tense ( wakati uliopita )
The future tense ( wakati ujao )
Na kila tense imegawanyika katika sehemu kuu nne ambazo : simple , continous , perfect na continous perfect.
1. PRESENT TENSE ( Wakati uliopo )
I. Simple present tense
II. Present continous tense
III. Present perfect tense
IV. Present perfect continuous tense
2. PAST TENSE ( Wakati uliopita )
I. Simple past tense
II. Past continuous tense
III. Past perfect tense
IV. Past perfect continuous tense
3. FUTURE TENSE ( Wakati ujao )
I. Simple future tense
II. Future continuous tense
III.Future perfect tense
IV. Future perfect continuous tense
Leo tuanze na "simple present tense "
Simple present tense -huu ni wakati ambao unaonyesha vitendo ambavyo vinafanyika kila siku au vya mazoea. Vitenzi ( verbs ) ambavyo vinatumika
katika wakati huu havibadiliki isipokuwa katika nafsi ya tatu umoja .
Zifahamu Nafsi
Nafsi ya kwanza : I ( mimi )
Nafsi ya pili : You ( wewe )
Nafsi ya tatu : He / she / it ( yeye
WINGI
Nafsi ya kwanza : We ( sisi )
Nafsi ya pili : You ( ninyi )
Nafsi ya tatu : They ( wao )
Examples :
I sing songs = > huwa naimba nyimbo
You sing songs = > huwa unaimba
nyimbo
He sings songs = > huwa anaimba nyimbo
She sings songs = > huwa anaimba nyimbo
It sings songs = > huwa anaimba nyimbo
We sing songs = > huwa tunaimba nyimbo
You sing nyimbo = > huwa mnaimba nyimbo
They sing songs = > huwa wanaimba nyimbo
#Kwa nafsi ya tatu umoja , hapa
nazungumzia : ( He , she na it ) ambapo hawa vitenzi vyao vinabadilika vinakuwa vinaongezewa S , ES au IES .
Mfano : take / takes , do / does / fry / fries .
SHERIA YA KUBADILISHA VITENZI ( VERBS ) .
Vitenzi ( verbs ) vingi huwa vinaongezewa " S " tu . Mfano : Seem / seems , look / looks , take / takes .
Kwa vitenzi ambavyo vinaishia na O huwa tunaongezea - ES . Mfano : Go / goes / , do / does , veto / vetoes ) .
Kwa vitenzi ( verbs ) ambavyo vinaishia na - S , - Z , - CH , -SH na - X , hapa huwa tunaongezea " ES " . Mfano : Punch / puches , wash / washes , kiss / kisses , fizz / fizzes , mix / mixes )
Kwa vitenzi ( verbs ) ambavyo vinaishia na sauti ya konsonant alafu mbele zimeishia na - Y huwa tunatoa Y alafu tunaongeza
IES , Mfano : ( Hurry/ hurries , Clarify / clarifies )
Ila kwa vitenzi ambavyo vimeishia sauti ya irabu ( vowel ) huwa tunaongeza " S " tu mbele . Mfano : ( Play / plays , enjoy / enjoys )
KUMBUKA : Kanuni zote za hapo juu zinatumika katika nafsi ya tatu umoja tu ( He , she na It ) .
Kwa nafsi zingine zote vitenzi huwa havibadiliki .
MIUNDO YA SENTENSI KATIKA TENSE HII .
1. Kwa sentensi za kukubali / chanya :
SUBJECT + MAIN VERB
I wake up at 6 AM
( Huwa naamka saa 12 asubuhi )
You wake up at 6 AM
( Huwa unaamka saa 12 asubuhi )
He wakes up at 6 AM
( Huwa anaamka saa 12 asubuhi )
She wakes up at 6 AM
( Huwa anaamka saa 12 asubuhi )
2. Kwa sentensi za kukanusha
SUBJECT + DOESN'T/ DON'T + MAIN VERB
Ufafanuzi :
DOESN'T - inatumika kwa nafsi ya tatu umoja , yani He, she na It .
DON'T - inatumika kwa nafsi
KUMBUKA : Unapotumia DON'T au DOESN'T basi kitenzi kikuu ( main verb ) kinakuwa hakibadiliki ( infinitive ) .
Pia :
Does not = Doesn't
Do not = Don't
KUMBUKA : Unapotumia DON'T au DOES basi kitenzi kikuu ( main verb ) kinakuwa hakibadiliki ( infinitive ) .
Examples :
-I do not wake up at 6 AM
( Huwa siamki saa 12 asubuhi )
-You don't wake up at 6 AM
( Huwa hauamki saa 12 asubuhi )
-He does not wake up at 6 AM
( Huwa haamki saa 12 asubuhi )
-She doesn't wake up at 6 AM
( Huwa haamki saa 12 asubuhi )
- It does not wake up at 6 AM
( Huwa haamki saa 12 asubuhi )
- We do not wake up at 6 AM
( Huwa hatuamki saa 12 asubuhi )
They don't wake up at 6 AM
( Huwa hawaamki saa 12 asubuhi)
3. Sentensi za kuuliza maswali
DO / DOES + SUBJECT + MAIN VERB
Examples :
Do you live here ?
( Je unaishi hapa ? )
Does he like this t-shirt ?
( Je anaipenda fulana hii ? )
Jinsi ya kujibu
-Yes I do .
-Yes he does .
-Yes she does .
Mifano zaidi
She loves her mother
( anampenda mama yake )
He eats banana
( Hula ndizi )
I drive a car
( ninaendesha gari )
You like this movie
( unaipenda muvi hii )
They hate us
( wanatuchikia )
Source : www.englishkona.com
Kwa leo tuishie hapa....tutaendelea .
WhatsApp : 0767329643
NOTE : Huu uzi utakuwa unasasishwa kila mara .
Updates :
II. Present contunuous tense ==> Post namba 235
III. Present perfect tense ==> Post namba 236.
SUBSCRIBE YouTube @ English Kona