Uchaguzi 2020 Jicho la Tatu: Mgombea Urais CHADEMA ni Freeman Mbowe! Tundu Lissu Pacemaker! Nyalandu ni Serious Contender, Msigwa anatania, Dkt. Mayrose Majinge...

Kwanini unahisi Mbowe atashindwa Ubunge?
Nafikiri ni muumini wa hirizi hii
FB_IMG_1582080397242.jpg
 
24/24 unaandika threads za Kusifia sifia tu.. Lissu ndiye Mgombea Chadema na hapo Moto utawaka.. Ikitokea Kuchakachua Dunia Nzima itajua, so wewe na unaowapamba kwanye threads zako omba sana Hasipitiswe otherwise uteuzi unaoupigania utausikia tu kwenye mitandao... Sifia sifia hii ikoje.. Masaa/Muda yote unaandika siasa za Kimrengo wa kusifia wa Kijani...
 
Chadema wasifanye makosa wakamteua mgombea kwa kupip, waweke MTU makini, utabiri wangu kule upande. Wa pili kuna pigo takatifu linaenda kuwasambaratisha kabla ya uchaguzi, hivyo uwezekano wa dola kuchukuliwa na na Chadema no mkubwa
 
Ndugu Pascal, once again tunakushukuru kwa utabiri wako, wa busara na uliofanywa kwa utafiti. Wengi tunapenda sana kukusoma, lakini mabandiko yako ni mengi sana na yanachosha, you are well known and respected for your factual imput and political views, huhitaji maonyesho mengi...
Analysis yako pia nai object kidogo,

Its obvious CHADEMA walishafanya analysis kuwa nani atakua mgombea ila wanapochukua fomu wengi ni kujaribu kuongeza alternative in case lolote likitokea kwa mgombea aliyekusudiwa.

Kuhusu ACT au NCCR ikitokea CHADEMA imeanguka basi jua itakufa na vyote vilvyobaki. ACT ina nguvu visiwani tu coz ya Maalim ila hku bara hawana capital hta ya jimbo moja. CHADEMA at its worst haiwezi kosa walau kura million 2 coz ina capital ya loyalists wake mikoani.

NCCR haina hata kata moja inayoweza kuwa base ila CHADEMA mfano kura za mdee na mnyika pekee hta wakiwa washindi wa pili ni nyingi kuliko majimbo 10 ya zanzibar so kwenye viti maalum ndipo CHADEMA atawazidi kete kma ilivyokua 2015!!.

So hta CHADEMA wakipata majimbo 10 tu ila wakawa runner up majimbo makubwa ya Dar Mbeya Mwanza bado watapata seats extra 15+ enough to offset ACT from KUB.

Hoja hapa ni political capital tu tuache illusions za Mbatia unless awe KUB na wabunge 5 pekee. Ama CCM wampe mgombea urais strong ili apunguze kura za CHADEMA otherwise kwa hoja yako ya KUB sioni wa kuitoa CHADEMA kwa vyama vilivyopo .
 
Wanabodi,

Leo natoa somo linaliutwa Logical Progression kwenye kufanya analysis kwa Kuangalia kitu kwa Jicho la Tatu, ni kuliangalia jambo kwa critical angle kwa kutumia predictions based on logical thinking kwa kutumia critical thinking na kufanya logical progression kwa kupima the motive behind, the causative agents and the underlying factors ya jambo fulani ili kujua kitakacho fuata kabla hakijatokea.

Wakati nikiwa mshauri wa siasa wa ubalozi fulani hapa nchini ile 2010 baada tuu ya uchaguzi mkuu kumalizika, wenzetu Wazungu wanafanya kitu kinachoitwa Stakeholders Mapping ya Who is Who kwenye serikali mpya na hiyo inafanywa na political advisor wao..
Kama ulikosea jambo obvious kabisa kwa Samweli Makinda na Speaker Sitta basi utakuwa unabahatisha tu.

Sita kutupwa nje ya uspika ilikuwa wazi kabisa kwa sababu alikuwa mwiba kwa serikali na ccm at the core.

Ilikuwa lazima atoswe tu hata kama ulikuwa ni utamaduni wa CCM kuongoza mihula miwili.

Back to Tundu Lissu na Mbowe scenario.
Yawezekana uko sahihi sana kwa sababu kuu mbili.
1. Lissu yuko ughaibuni na kurejea Kwake sidhani kama atarejea zaidi ya kuwa pacemaker na kukirudisha chama kwenye masikio ya watu na Mbowe ni an alternative to fill the void pindi Lissu atakaposhindwa kurejea kuendelea na mchakato wa uchaguzi.

2. Wagombea wengine hawana mvuto wa kisiasa hasa Nyarandu, Msigwa na Majinge CHADEMA hakiwezi kusimamisha wagombea kama hao kupambana na Magufuli litakuwa kujichimbia kaburi tu na kujizika chebyewe hivyo Mbowe lazima ajaze hilo Ombwe.

Hoja zako zingine siwezi kujadili kwa sababu they lack merits.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Ndugu Pascal, once again tunakushukuru kwa utabiri wako, wa busara na uliofanywa kwa utafiti. Wengi tunapenda sana kukusoma, lakini mabandiko yako ni mengi sana na yanachosha, you are well known and respected for your factual imput and political views, huhitaji maonyesho mengi.

Kwenye mada: Yote uliyoyatabiri hapa ni facts supported na scenario za ukweli, na kila kitu kiko wazi. Ila ningependa kukuongezea, kama chadema hawatafanya mipango ya umoja (UKAWA) na vyama vingine, basi mgombea mwenza wa Mbowe atakuwa Bi Mayrose...
NCCR haina uwezo wa kupata hata mbunge mmoja hiyo Kambi ya Upinzani wataitoa wapi?

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Mi nakusalimia tu,sina Hoja.
Ni kwamba bila tume huru ya uchaguzi ni kama drama tu.

Tumeshaambiwa bunge litajaa Kijani,na viti vichache vya CUF na Kile chama cha mbatia(CCM B).
 
Umezunguka wee ila lengo ni kuonyesha kuwa Mbowe atashindwa ubunge hivyo anaenda kugombea Urais ili kuficha aibu yake, na pia unataka kuonyesha kuwa alitakalo Mbowe Chadema ndilo linakuwa. Hivi huyu Mbowe mbona anawanyima sana usingizi, yaani ni kama ndiyo oxygen ya wana Lumumba, msipomtaja maisha hayasongi.
Mbona unaongea kitaarabu sana?

Ukweli ni kwamba bila tume huru ya uchaguzi ni kama kucheza mziki tu.
 
Paskal Mayala bado naona unaingia chaka, Unapiga RAMLI CHONGANISHI.

MBOWE Kutangaza nia sio Kichaka cha kuogopa kuukosa ubunge, Bali ni strategic approach.

Free and fair election Mbowe bado anakubalika Hai na atashinda...
Sema wewe ndio unamkubali Mbowe,usituzungumzie hai hatutaki hata kumwona,akija kwenye kampeni tutamzomea kama mwanzo
 
Pascal Mayalla
Mbowe kachukua fomu baada ya kugundua inaweza kua Lissu akashindwa kugombea kwa kushindwa kuja nchini, au akapata misukosuko ya mahakamani.

Hivyo, ili kuzuia genge jingine la wahuni kama akina Nyarando kuja kugombea na kina Msigwa ambao hawawezi zua dafu kwa Magu, badi bora na yeye achukue fom
 
Nakubaliana na wewe Pascal, nilipoona tu mwenye chama ametia nia na jana ikavuja ile clip ya Lena akimsengenya LISSU basi ni indication tosha kuwa LISSU hana chake, ajipange tu kutafuta jimbo la kugombea ubunge.
 
Nimesoma bandiko lako na kupitia rejea mbalimbali kuhusiana na mada husika. Niliposikia habari za Mbowe kuwa naye ameombwa na wazee kutangaza nia na kusudio la kugombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), nilipatwa mshangao kwa kuwa nilitegemea CHADEMA kuepusha aina yoyote ya mchuano kati ya Mwenyekiti Mbowe na Tundu Antipas Lissu, lakini kwa kuwa wanasiasa huwa wana trick na malengo tofauti, hiyo haikunisumbua sana.

Japo bado nikawaza iwapo Tundu Lissu atachuana na kumshinda Mbowe katika kura za wajumbe, hii itakuwa na maana gani hata kama CHADEMA haitashinda kiti cha Uraisi?

Nikiangalia na kurejea kwenye historia ya Wagombea wa Urais kutokea CHADEMA kuanzia mwaka 2005 kwa kuwa Uchaguzi mkuu wa 1995 CHADEMA haikuwa na mgombea wa Urais, halikadhalika pia Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2000 pia hawakuwa na mgombea.

Hii ina maana kuwa tangu kuanza UCHANGUZI MKUU wa vyama vingi mwaka 1995 CHADEMA imeshiriki uchaguzi mkuu kwa nafasi ya Urais mwaka 2005, 2010 na 2015.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 CHADEMA ilimsimamisha Freeman Aikael Mbowe, ambapo alimaliza nafasi ya tatu akiwa na kuwa kura 668,756 asilimia 5.88% ya kura zilizopigwa.

Mwaka 2010 CHADEMA ilimsimamisha Wilbroad Slaa ambapo ilipata kura 2,271,491 sawa na asilimia 27.05% kutoka asilimia 5.88% ilizopata miaka mitano iliyopita.

Tunafahamu mwaka 2015 chini ya mwavuli wa UKAWA CHADEMA ilimsimamisha Edward Lowassa ambapo ilipata kura 6,072,848% sawa na asilimia 39.97% za kura za URAIS.

Kwa nini nimeanza kwa kueleza haya, ni kwa sababu mara nyingi wachambuzi wa siasa hawapendi kuangalia historia. Wachambuzi wengi hasa hawa vijana wenye ushabiki huwa hawaoni mbali zaidi ya ushabiki wao.

Mazingira na pressure za mwaka wa uchaguzi hufanya watu wengi kutokuona uhalisia wa hali ya kisiasa. Waliosoma Takwimu kuna mambo kadhaa ambayo wameyagundua hapo.

Sasa turudi kwenye kupata mgombea kwa mwaka 2020 ndani ya CHADEMA. Mwaka 2015 hali ya nani agombee urais kwa tiketi ya CHADEMA ilibadilika kwa sababu ya ujio wa Lowassa. Hivyo wengi walikubali kuwa Edward Lowassa anafaa, japo kuna yalizungumzwa nyuma ya pazia, kwa sasa hayo hayana umuhimu sana japo yametuachia somo kubwa.

Wote tunakubaliana kuwa Lowassa alikuwa na mvuto, alikuwa anajulikana, alikuwa anauzika, alikuwa anafahamikabna zaidi sana alikuwa na mtaji wa kuutafuta Uraisi.

Hivyo kujiunga kwake CHADEMA ikawa mtaji kwa Chama na hatimaye kwa UKAWA. Lakini kabla ya ujio wa Edward Lowassa ni wazi kuwa mtu aliyekuwa na nafasi kubwa ya kupata uungwaji mkono mkubwa basi alikuwa Dr. Wilbroad Slaa.

Leo tupo hapa mwaka 2020, na inaonekana wengi walidhani kuwa mgombea angekuwa Tundu ANTIPAS Lissu kwa sababu mbalimbali.
Inawezekana Lissu ndiye mjenga hoja mzuri na mzungumzaji mzuri kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya CHADEMA.

Kisiasa wanasiasa wanazidiana katika vipawa na vipaji, wanaweza kuwa wana-itikadi moja, wanaweza kuwa na sera na mipango inayofanana lakini huwa wanakuwa na vipawa tofauti. Rejea Barack Obama na Macron wa Ufaransa.

Kama Mbowe ana nia ya kushindania nafasi ya kugombea Urais kupitia CHADEMA ni wazi kuwa atapata kura za Kamati za Chama na ataweza kupata nafasi hiyo kwa sababu ya historia na nafasi yake ndani ya Chama.

Peter Msigwa na Lazaro Nyalandu, sioni nafasi yao katikati ya Lissu na Mwenyekiti Mbowe. Pia sioni uwezo wao binafsi katika nafasi wanayoitaka. Ni aina ya wagombea wanaotegemea kuuzwa na Chama lakini wao wenyewe wana ushawishi mdogo sana.
Kwa siasa za sasa, unahitaji pia ushawishi binafsi wa mgombea kwenye nafasi ya Urais.

Kwa hali ilivyo na kama Mwenyekiti atagombea hakuna wa kumzuia japokuwa haitawapa mtaji mkubwa sana CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu.

Lakini inawezekana pia ni hesabu za mwenyekiti kwa kuwa haijulikani kama Tundu Antipas Lissu anaweza kuwa na sifa za kukubalika kugombea nafasi hiyo kutokana na mambo kadhaa.
 
Heshima kwenu wanajamvi.

Ningekuwa na mamlaka ndani ya CHADEMA Mh Lissu angepitishwa mapema asubuhi bila kupoteza muda.Nafikiri ni muda muafaka haswa ndani ya CHADEMA kuacha kupoteza muda Mh Lissu anauzika kirahis zaidi ukilinganisha na wagombea wengine hasa katika majira haya yanayo hitaji mtu wa kushindana na Mh Magufuli ambaye katika kipindi cha miaka mitano amehakikisha upinzani haupati nafasi ya kusikika huku yeye binafsi akitumia vyombo vya habari sana.
Mkuu Ngongo, kwanza naunga mkono hoja ya presidential candidature ya Tundu Lissu kwasababu ni presidential material, hata mimi nilishauri
Elections 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Ila baada ya kuanza kufunguka funguka huko Ughaibuni, niliingia mashaka kama atarejea home
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Tundu Lissu akatoa conditions to be met kabla ya kurejea, na mimi nikashauri
Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Na alipoamua kugombea kutokea Ughaibuni nika comment
Elections 2020 - Je, kuna uwezekano kutangaza nia kugombea Urais kupitia CHADEMA kwa baadhi, kunatumika kama kichaka cha kujifichia aibu ya kushindwa ubunge?.

Na mwisho nikawatajia mgombea urais wa Chadema, sio Lissu!.

Elections 2020 - Jicho la Tatu: Mgombea Urais CHADEMA ni Freeman Mbowe! Tundu Lissu Pacemaker! Nyalandu ni Serious Contender, Msigwa anatania, Dkt. Mayrose Majinge...

P
 
Back
Top Bottom