Uchaguzi 2020 Jicho la Tatu: Mgombea Urais CHADEMA ni Freeman Mbowe! Tundu Lissu Pacemaker! Nyalandu ni Serious Contender, Msigwa anatania, Dkt. Mayrose Majinge...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi,

Leo natoa somo linaliutwa Logical Progression kwenye kufanya analysis kwa Kuangalia kitu kwa Jicho la Tatu, ni kuliangalia jambo kwa critical angle kwa kutumia predictions based on logical thinking kwa kutumia critical thinking na kufanya logical progression kwa kupima the motive behind, the causative agents and the underlying factors ya jambo fulani ili kujua kitakacho fuata kabla hakijatokea.

Wakati nikiwa mshauri wa siasa wa ubalozi fulani hapa nchini ile 2010 baada tuu ya uchaguzi mkuu kumalizika, wenzetu Wazungu wanafanya kitu kinachoitwa Stakeholders Mapping ya Who is Who kwenye serikali mpya na hiyo inafanywa na political advisor wao.

Nikawafanyia kuanzia juu kwenye viongozi wa mihimili. Samwel Sitta akiwa ndiye alikuwa Spika wa Bunge lililotangulia na amesifika sana kwa kuzitumia zile Initial za jina lake Samwe Sitta -SS kuzigeuza neno Speed & Standards, yaani Spika wa Kasi na Viwango. Hivyo kwenye Stakeholders Mapping yangu nikaonyesha nafasi ya Spika ni Samwel Sitta anaendelea.

Kweli kwenye uspika Samwel Sitta akawa ndio mtu wa kwanza kuchukua fomu na mimi nikajua kwa kazi nzuri ya Spika wa viwango, hata pingwa ndani ya CCM!.

Mara paa!, aliyekuwa deputy wake Anna Makinda, naye kachukua fomu kumchange bosi wake!. Mfano baada ya uchaguzi Job Ndugai achukue fomu kugombea uspika, na Tulia nae achukue fomu kumchallenge Ndugai!.

Kwenye work station yangu nikaona alert ya priority 1 toka kwa balozi anauliza kama Spika ni Sitta ataendelea, what does it mean kwa deputy wake kuchukua fomu kugombea?.

Nikaijibu pale pale tena with confidence without hata thinking, kuwa Spika ni Sitta, nikasema Anne Makinda anajaza fomu kugombea uspika ili kujifurahisha tuu kwa kujionyeshea na yeye ni Speaker material!. Balozi akanijibu "you are wrong Mr.Pascal!" kisha akasuggest a meeting to discuss this.

Kwenye kikao nikaulizwa kwanini bado ninafikiri Sitta ndio ataendelea kuwa Spika? Nikajibu with confidence kuwa huo ndio utaratibu wa CCM kwa nafasi za juu kushikwa angalau kwa vipindi viwili, Sitta amemaliza kipindi kimoja tuu, hivyo ataendelea!.

Balozi akasema hebu think more critically, wewe ni speaker umefanya kazi nzuri, umekaa just one term, umechukua form kuomba kuendelea, halafu mara deputy wako anachukua form kuku challenge!, nikaulizwa doesn't it ring a bell in your head that is a bit awkward?!.

Mimi nikang'ang'ana Anne Makinda amechukua fomu kujifurahisha!. Ndipo mzugu akanipiga somo la logical progression kuwa Sitta anapigwa chini, Anna Makinda kaambiwa achukue fomu, hivyo sasa tusubiri sababu za kumpiga chini Sitta!.

Duh...!, na kweli kwenye CC ya CCM, jina la Sitta likikatwa kwa hoja kuwa tunatoa nafasi ya uspika kwa gender!.

Katika yale mazungumzo yetu na balozi, balozi alionyesha dalili zote kuwa tayari yuko tipped long ago kuwa Sitta atapigwa chini, masikini mimi political advisor wao naulizwa kupimwa tuu!

Hivyo hii ni a quick assessment yangu yangu kwa watia nia 5 wa urais wa JMT kwa tiketi ya Chadema kwa kutumia logical progression.

NB. Hii sio mara yangu ya kwanza kuleta hoja za namna hii, hata kwa mgombea wa CCM uchaguzi Mkuu wa 2015, mimi nilimtaja mwezi August 2014! Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli
Hivyo kama haujui critical thinking, na mambo haya ya logical progression, wewe usinibishie, just sit and watch as time will tell.

Angalizo: Hoja hapa sio ku discuss watu, ni tuna discuss ideas hivyo kama wewe sii miongoni mwa watu wenye uwezo wa kusoma in between the lines na kubaini the motive behind!, nakushauri tuu jipitie zako tuu usipoteze muda wako, na wale wachangiaji simple minds ambao hao kazi yao ni kujadili watu kama kumjadili mtoa mada, karibuni kule MMU etc.

The most serious contender ni Tundu Lissu!. Sababu ni hii
Elections 2020 - Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? Ameonyesha Uwezo Zaidi ya Magufuli!

Lakini kufuatia hoja hii
Kwa mliomsikia Tundu Lissu kwenye Hard Talk, unadhani atarejea nchini? Mimi sina hakika na akirejea, atakuwa ni shujaa kuliko hata Nelson Mandela!

Na hata baada ya kumbembeleza Lissu hapa
Kamanda Lissu, Usisubiri Jibu la IGP Kuhusu Usalama Wako, Aliyekulinda na Shambulio Lile Yupo, Yeye Aweza, na Ataendelea Kukulinda, Welcome Back Home!

Kuna uwezekano ugombea wa Lissu ni just a "Pacemaker" tuu, ndio maana Freeman nae kagombea, hivyo sasa mgombea wa ukweli wa urais wa Chadema could be ni Freeman Mbowe!.

Kitendo cha Lissu ambaye ndie the one and only ndani ya Chadema mwenye guts, ability na capabilities za kumkabili rais Magufuli akapata angalau ka joto joto ka uchaguzi, kitendo Freeman Mbowe kutangaza nia, jicho la tatu linaelekeza Lissu ni Pacemaker tuu!.

Sababu za ugombea wa Freeman Mbowe ni huu niliouzungumza hapa
Elections 2020 - Je, kuna uwezekano kutangaza nia kugombea Urais kupitia CHADEMA kwa baadhi, kunatumika kama kichaka cha kujifichia aibu ya kushindwa ubunge?.

Lazarus Nyalandu ni very serious contender, ila he is too gentlemanly kwa kushindana na Magufuli.
Mchungaji Msigwa anatania tuu!.

Dr. Mayrose Majinge nimemzungumzia hapa
Elections 2020 - Mwanamke ajitokeza kuwania Urais kupitia CHADEMA. Ni Msomi, Mwanamke wa Shoka, Ana uwezo na Jembe Kweli, ila...

NB. Sio lazima kila kitu kwenye critical thinking na logical progression za any predictions kama hii ya Jicho la Tatu ni lazima kitokee au litimie!, hivyo ikitokea other wise msije kunishukia!

Nawatakia mchakato mwema.

Paskali.
 
"Sangara wameongezeka urefu kutoka sentimita 8 hadi sentimita 16" - John Magufuli.

"Inafikirisha pale mmoja wa wagombea anapowahakikishia wagombea wenzake kuwa uchaguzi utakuwa huru na wa haki. Pia Mwenyekiti wa chama kimojawapo kishiriki cha uchaguzi mkuu, anapovionya vyama vingine kuwa hatavumilia matusi na kejeli" Askofu Benson Bagonza.

Mbowe anarushiwa mawe hadi yanalundikana juu ya mwili wake. Waapi buana, Haongei,Hana habari. Watu wanaongea hadi wanajiona wapumbavu.

MwanaSIASA mwingine wa aina hii ni Mzee Lowassa.
 
Umezunguka wee ila lengo ni kuonyesha kuwa Mbowe atashindwa ubunge hivyo anaenda kugombea Urais ili kuficha aibu yake, na pia unataka kuonyesha kuwa alitakalo Mbowe Chadema ndilo linakuwa.

Hivi huyu Mbowe mbona anawanyima sana usingizi, yaani ni kama ndiyo oxygen ya wana Lumumba, msipomtaja maisha hayasongi.
 
Kiukweli mwaka huu sioni nafasi ya Chadema katika uchaguzi huu sema tu Watanzania tumezoea kuishi kwa matumaini fake na kujipa moyo hata pale uharisia unapoonekana wazi.

Kwa vile ni haki ya Chadema kusimamisha mgombea Mimi naona wampe Nyalandu, Tundu Lissu Watanzania wengi wameshampuuza na kumuona ni mpiga porojo tu.
 
Chadema wagombea wanaochuana Ni wawili tu Mbowe na Nyalandu.Lisu na Msigwa ni out of the equation.

Duniani kote huwa Kuna vyama vya maskini na matajiri.

Tanzania Chadema ni chama Cha matajiri toka kuanzishwa kwake Ni capitalist party chenye mlengo wa kibwanyenye. Hivyo nafasi Kama ya mwenyekiti wa chama taifa au mgombea uraisi lazima awe na uwezo kifedha au na uwezo mkubwa wa kuzalisha pesa za ndani au za nje awe money magnet

Nyalandu pesa anazo za ndani na nje na ana connection za pesa za nje na Mbowe pesa anazo na hukaa katikati ya matajiri wa chadema he belongs to Chadema elites wenye pesa.Hawa wawili wanakubalika na wenye pesa ambao ndio injini ya uendeshaji chama kwa pesa na Mali zao na ndio wagharimiaji chaguzi

Lisu na Msigwa Ni maskini wao size Yao Ni ubunge na udiwani sio Uraisi sababu hawana pesa za kuendesha kampeni na bila pesa za kampeni Chadema itashindwa kabla ya uchaguzi.

Mpambano Ni Kati ya wenye nacho Mbowe na Nyalandu.

Lisu ana waunga mkono wengi wa mitandaoni lakini kwanza waunga mkono hao Ni malofa hawana pesa Ni wakereketwa tu wa Iisu mzee wa Facebook na pili hawako kwenye vikao vya maamuzi vya chadema.Ni wapiga yowe mitandaoni tu

Msigwa yeye kajitosa kutania tu
 
Umeandika mafi mafi ..Dr Slaa alikuwa na fedha?
Alikuwa na wafadhili wa nje wa kufa mtu wa kufadhili chadema yeye ndie alikuwa contact person alijuana nao akiwa katibu wa baraza la maaskofu katoliki.kAONDOKA NA WAFADHILI WA NJE WAMEONDOKA
 
Paskal Mayala bado naona unaingia chaka, Unapiga RAMLI CHONGANISHI.

MBOWE Kutangaza nia sio Kichaka cha kuogopa kuukosa ubunge, Bali ni strategic approach.

Free and fair election Mbowe bado anakubalika Hai na atashinda.

Unachofanya hapa ni poor analysis kwa vile umeusoma mchezo kuwa Political situation Mbowe ndio Threat.

By any means lazima awe subjugated.
Atakaposhindwa Ubunge kwa kutotangazwa utarudisha tena Uzi wako huu ili uonekane Umetabiri.

Acha kuplay na mind za watu, people here are not Idiot of that nature.

Njoo na chambuzi za maana bhana.
 
Ndugu Pascal, once again tunakushukuru kwa utabiri wako, wa busara na uliofanywa kwa utafiti. Wengi tunapenda sana kukusoma, lakini mabandiko yako ni mengi sana na yanachosha, you are well known and respected for your factual imput and political views, huhitaji maonyesho mengi.

Kwenye mada: Yote uliyoyatabiri hapa ni facts supported na scenario za ukweli, na kila kitu kiko wazi. Ila ningependa kukuongezea, kama chadema hawatafanya mipango ya umoja (UKAWA) na vyama vingine, basi mgombea mwenza wa Mbowe atakuwa Bi. Mayrose.

Cha kusikitisha ni kuwa leo chadema hakifanyi political calculations, anayestahili kuwa mgombea wao ni Lissu, tukiangalia popularity na chances za kuweza kupata wabunge wengi , Uraisi hapana ni ngumu sana, leo chadema kinapigania kuhakikisha kinabaki kuwa chama kikuu cha upinzani, ambacho kiko hatarini kukipoteza, na kikachukuliwa na ACT au NCCR.

Hii nia ya Mbowe, inatufundisha ubovu wa kuwa na vyama vya watu binafsi kama taasisi za kibiashara ama viduka mamboleo. Always decision inakuwa ni ya mwenye chama na familia yake.

Pia Historia ya siasa Tanzania inaonyesha kuwa Democracy hapa kwetu inapatikana kwa watu wa Pwani, lakini Ikishaenda Bara, siasa zinaingia kwenye mkondo wa Mabavu na Udikteta.
 
Umezunguka wee ila lengo ni kuonyesha kuwa Mbowe atashindwa ubunge hivyo anaenda kugombea Urais ili kuficha aibu yake, na pia unataka kuonyesha kuwa alitakalo Mbowe Chadema ndilo linakuwa. Hivi huyu Mbowe mbona anawanyima sana usingizi, yaani ni kama ndiyo oxygen ya wana Lumumba, msipomtaja maisha hayasongi.
Hapana ndugu hatunyimi usingizi, ukweli ni kuwa Mbowe ni kiongozi wa chama kikuu cha Upinzani, ambacho ndio mshindani mkuu wa chama tawala, lazima tumuangalie kwa jicho la tatu na la nne, tukimpuuza, litatugharimu.

Ni mjinga atakaye mdharau mshindani wake hata awe mfupi, makengeza, kipofu au kiwete.

Huyu Pascal ni mkorofi na mkweli, na hana siri. Na nyie wana chadema mnakosa busara, baada ya kumshukuru, kwani amemifungua macho na kuwaonyesha panapovuja, na mvua kali zinakuja, badala ya kuezeka mnaamua kumshambulia
 
Kiukweli mwaka huu sioni nafasi ya chadema katika uchaguzi huu sema tu watanzania tumezoea kuishi kwa matumaini fake na kujipa moyo hata pale uharisia unapoonekana wazi.

Kwa vile ni haki ya chadema kusimamisha mgombea Mimi naona wampe nyalandu, tundu lissu watanzania wengi wameshampuuza na kumuona ni mpiga porojo tu.
Chadema wasikilize huu ushauri.
 
Hapana ndugu hatunyimi usingizi, ukweli ni kuwa Mbowe ni kiongozi wa chama kikuu cha Upinzani, ambacho ndio mshindani mkuu wa chama tawala, lazima tumuangalie kwa jicho la tatu na la nne, tukimpuuza, litatugharimu.

Ni mjinga atakaye mdharau mshindani wake hata awe mfupi, makengeza, kipofu au kiwete.

Huyu Pascal ni mkorofi na mkweli, na hana siri. Na nyie wana chadema mnakosa busara, baada ya kumshukuru, kwani amemifungua macho na kuwaonyesha panapovuja, na mvua kali zinakuja, badala ya kuezeka mnaamua kumshambulia

Kama wewe hakunyimi usingizi basi wenye chama chao wanamuugua kabisa. Wiki nzima kwenye Bunge la bajeti anazungumziwa yeye, msemaji wa polisi anakubali kulinajisi jeshi kwa uongo wa kitoto kabisa kumchafua Mbowe,huku mitandaoni hasa JF wote mnamshambulia Mbowe. Mwanzoni Pasi alikuwa anatoa miichango fikirishi na elimishi lakini siku hizi ameshaamua kuchua upande na yeye mwenyewe alikiri hivyo hapa wewe unataka kusema nini?
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom