Jiajiri kwenye hii biashara hata kama huna mtaji

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,399
40,295
Najua wengi wana akaunti katika mitandao ya kijamii; sasa ni wakati wa kutumia hiyo mitandao kuingiza pesa.

Anza hivi:-

No. 1
  • Tengeneza 'database' ya mambo yote yanayohusu ujenzi
  • Ingia makubaliano na hawa mafundi:-
i. Fundi wa kupaua
ii. Fundi wa plasta
iii. Fundi wa urembo-decoration
iv. Fundi wa kuskimu
v. Fundi wa ma-grill
vi. Fundi wa aluminium
vii. Wazibuaji wa vyoo
viii. Mafundi bomba
ix. Fundi umeme
x.Fundi wa kujenga
  • Ingia makubaliano na maduka ya vifaa vya ujenzi
  • Ingia makubaliano na kampuni za mabati
  • Ingia makubaliano na wanaokodisha vifaa vya ujenzi
No. 2
  • Ingia kwenye akaunti yako na tengeneza jina, mfano:- Equation x Bingwa wa ujenzi
  • Alika marafiki wa kila namna kadri uwezavyo, na hakikisha kwenye akaunti yako una marafiki hata zaidi ya 10,000
  • Akaunti yako iunge na magrupu mbalimbali
  • Usiruhusu wale ulioingia nao makubaliano kufanya chochote kwenye akaunti yako
  • Tangaza zile kazi zinazofanywa na watu ulioingia nao makubaliano ila tumia njia kuonekana wewe ndio unafanya, na mawasiliano yote yawe ni kwako.
  • Na wale ulioingia nao makubaliano wanatakiwa waonekane wewe ndio umewaajiri, yaani wewe ndio boss wao.
No.3
  • Anza kupokea 'order' na kula mafao
  • Anza kumiliki kampuni kubwa kubwa

NB. Unaweza kutumia hii njia hata kwenye idara zingine si lazima, ujenzi.
 
Ni wazo zuri ila halimfai mtu mvivu.

Kutengeneza hiyo account, kuingia makubaliano na hao watu, kuikuza account mpaka kufikia watu 10,000 siyo kazi ya mwezi au miezi miwili kama unatumia jitiada pasipo matangazo ya kulipia (Ads).

Huu ni uwekezaji wa muda mrefu na unahitaji kujitoa na kujifunza mambo mengi katika sector husika.

Ni wazo zuri kwa aliye tayari kujitoa na kufanya pamoja na kujifunza kwa moyo mmoja.

Kubwa zaidi inahitaji UVUMILIVU mpaka kuanza kupata matokeo.

Ila INAWEZEKANA.
 
Ni kweli lazima mtu awe ni mpambanaji, mfano fb mtu anaweza kuwa na marafiki 5000 ambao hawamuingizii chochote, lakini ukiwatumia wao kama sehemu ya soko, itakuwa na manufaa zaidi.
 
Ni kweli lazima mtu awe ni mpambanaji, mfano fb mtu anaweza kuwa na marafiki 5000 ambao hawamuingizii chochote, lakini ukiwatumia wao kama sehemu ya soko, itakuwa na manufaa zaidi.
Upo sahihi mkuu, lakini ishu huwa inakuja katika kuwachambua kwasababu kuwa na marafiki 5000 au zaidi haina maana wote watakuwa wateja.

Kazi ya kutengeneza, kutafuta marafiki wengi, kutafuta wateja miongoni mwa hao marafiki kisha kutafuta watu wa kununua huduma moja kwa moja.

Wazo lipo Safi kabisa ila ndiyo hivyo lazima mhusika awe Hustler
 
Ukweli kabisa sijaelewa, maana fb nina marafika 4900 na kwenye page kuna watu walio active kama 157 hivi nina miaka kama 5 natangaza kitu ninachokifanya au fani ninayoifanya tena kwa kutupia ujuzi mpya lakini sijawahi pigiwa hata simu ya kazi .sijui shida ipo wapi hapo
 
Mmmh kwel mkuu, kazi IPI hiyo ambayo haina wateja , jaribu na kuweka kwenye status mkuu , pia na kwenye market place
 
Ukurasa wako wa mtandao wa kijamiini ni sawa na mtu aliyefungua duka kariakoo n.k, tofauti iliyopo; kariakoo wateja/wapita njia wapo 'physically' ila kwenye mtandao wateja/wapita njia wapo 'online'. Chakufanya, jitahidi kushawishi ubora wa huduma au bidhaa yako, pia gharama ziwe 'fair'
 
Ukiwa na nyumba za kupangisha, utakuwa na namba ya simu ya mzibua vyoo, fundi umeme, carpenter, plumber na mwanasheria.
Inawezekana,ila kama unataka kuja kumiliki kampuni yenye kufanya shughuli mfano nilizotaja, unaweza kutumia njia pendekezwa.
 
Inawezekana,ila kama unataka kuja kumiliki kampuni yenye kufanya shughuli mfano nilizotaja, unaweza kutumia njia pendekezwa.
Kama una nyumba 10+ zakupangisha ni kheri mzibua vyoo, carpenter, fundi umeme na fundi bomba wakawa kwenye payroll yako kila mwezi.
 
Mmmh kwel mkuu, kazi IPI hiyo ambayo haina wateja , jaribu na kuweka kwenye status mkuu , pia na kwenye market place
Napiga kazi ya skiming na upakaji rangi pia ninaujuzi wa ufungaji umeme na ufungaji mifumo ya maji kwenye nyumba, lakini sioni matokeo yoyote labda sijaweza kujitambua ninakwama wapi
 
Kama una nyumba 10+ zakupangisha ni kheri mzibua vyoo, carpenter, fundi umeme na fundi bomba wakawa kwenye payroll yako kila mwezi.
Ni kweli mara nyingi mnunuzi wa bidhaa anataka huduma kwa bei ya chini, anaweza kutumia pendekezo lako; ila kwa wale wenye mtazamo wa kumiliki kampuni anaweza kutumia mapendekezo pale juu, kwa sababu mwisho wa siku atapata wateja mbalimbali mpaka baadhi ya taasisi.
 
Ukurasa wako wa mtandao wa kijamiini ni sawa na mtu aliyefungua duka kariakoo n.k, tofauti iliyopo; kariakoo wateja/wapita njia wapo 'physically' ila kwenye mtandao wateja/wapita njia wapo 'online'. Chakufanya, jitahidi kushawishi ubora wa huduma au bidhaa yako, pia gharama ziwe 'fair'
Nimekuelewa lakinibulimwengu tuliopo ningumu sana kuweka ushawishi kwa wateja ili hali anajuwa mtaani kwake yupo fundi furani kuliko akutafte wewe asiye kufahamu
 
Back
Top Bottom