Nilijua uko dhaifu kama my wife wa mtu flani
Hii gemu ya watu wazima umeifakamia kichwakichwa
Sasa ngoja uchinjwe kama kuku wa kitoweo
Usije kujilizaliza kama Pinda alivyolia
Ngebe na kelele nyingi sijui unadhani tunacheza ma-ready?
Unaleta pumba kama mpunga sijui ndio kuchanganyikiwa
Sasa kaa chonjo ili ukobolewe kama unga we sembe
Dogo maneno mengi wakati mbata na bong'oa nimekupiga
Mbele yangu huna neno ni bora ujiite Bubu ataka kusema
Unaogopa?
Wanavita Umsolopagaaz Makumazan na Umbopa!
Mashairi unakopa, unga unga bopa bopa?
Umechoka? huna cha kunena unafoka?
Unajiona umetoka kumbe bado umepotoka
Hujui unapokwenda wala kule unapotoka
Spidi ya Gulfstream huipati kwayo Foka
Usilete Mahoka, galasha jokeri joka
Nguvu za Coca, pangusa vyako vimoka
Huliwezi soka, uwanjani toka
Twache makocha tuchane vocha
We ndondocha dondoka mdondo
Ka mnywa gongo mbogo, aliyeshindia kipande cha muhogo
Kama Kublai Khan, ngomeyo naihusuru
Bila msululu wa suluhu kamwe siinusuru
Hii nyukilia, ila siyo kwa asali
Usiposikia utakutana na ajali
Chernobyl au Bhopal, rungu lake Umbopa
We acha kuropoka,
Bila vina wala mizani
Unachina kizani
Wewe dinner dizaini
Wala sina mpinzani
Mzuri ka hina kindani
Mi jogoo la Mikindani
nadhani unabaini, sisemi na shwaini
Tafuta mnazi ukwee, ugeme labda pombe
Kwani kwenye starehe ya vina nachukua kikombe
Hata uombe, uchinje ng'ombe utambike Njombe
Baki na bonge la donge, huku walia chonde chonde
Mswahili mahiri na staili sizoghairi
Mashairi hariri kamili kukudhalili
Napitisha sheria, inayokataza kulia
Nikikupiga panga usiweze kuugulia
Nakupa mitihani ya kughani kwenye fani
Usipofika kani huwezekani kuingia laini
Nakusimamisha kama huna leseni, nenda traffic stesheni
We mtoto tu waoga kwenye beseni