Teamo
JF-Expert Member
- Jan 9, 2009
- 12,271
- 1,065
wanikumbusha mbali,vile wasema marindaKaskazini baridi , ndugu zako tunaganda
hadi mvua zenye radi, Mola ndiye atulinda
tumezipanda saladi, ili njaa kuishinda
tumeiweka ahadi, wala hatutoipinda
kweli tutajitahidi, japo twavaa marinda!
marinda vazi laheshima,kwa watz wa miaka ya nyuma
wazee wetu waliringa,walipovaa marinda
wazee licheka sana walipokunywa mirinda
kaka tuache kucheka,turudi kwenye ile hoja
nina siku thelathini,nabeba ile jumla jumla
kaka naomba ahadi,ili niende na muda
kaka sikusumbui,ila nakukumbusha
leo nimefurahi uliponikumbusha marinda