JF Exclusive: CAG Report on IPTL/Tegeta Escrow Account

JF Exclusive: CAG Report on IPTL/Tegeta Escrow Account

Uhalali wa report uliyonayo utapimwa na nini? Naogopa usije ambiwa wewe ndio msambazaji wa report fake.

Manake tulio mtaani tutamwaga ugali.

Naeleweka? Na asipoweka "Invisible" basi "Karumekenge" ataweka. Bahati hatuna zaidi ya siku nyingi kuona Bunge linasemaje.
 
Mimi hofu yangu ni juu ya sintofahamu au mtifuano utakao tokea bungeni...

Sitamani PM ajiuzulu maana itakuwa mzigo kwetu Bali hela iliyozidi irejeshwe....

Mkuu nini kujiuzulu tu, Mimi natamani wafungwe wote waliohujumu na kufisidi Nchi yetu.
Hawa wezi siyo wa kuwachekea kabisa.
 
Hata Mariamu alipokuwa na mimba ya Yesu alituhumiwa hivyo hivyo, si jipya hilo jaribu lingine.

Wewe mama bure kabisa, ni nani aliyekuloga, we na warioba au DR. Salim ni nano anaijua ccm, kwa nn haubadiliki, huyo aliyekuloga nadhani amefariki pole sana
 
What if wakisema kuwa report inayowasilishwa ni ile iliyopelekwa kwa Spika ambayo imenyofolewa hizo kurasa huku wakiwa wameshawabana wale wabunge wao waliopo kwenye Kamati na wale wa upinzani wameshashikishwa ndefu? I'm thinking loud...

Mkuu rejea kauli ya Speaker ndugu Job, aliposema hatuwezi(CCM) kuunda umoja wa wahalifu, maana yake hawawezi kuwa pamoja na wale uliowaita wabunge wa kwenye kamati ambao umefikiri wanaweza kubanwa!! Au kwa lugha rahis watetezi wa ukwapuaji huu!!

Mi nafikiri hilo la kubwana sidhani kama linaweza kutokea kwa sababu CCM wenyewe kwa wenyewe washavurugana,, ndipo inakuja ile dhana ya ukimwaga mboga,,,,,
 
Kijana mbona unakurupuka, na wewe umeingia mkenge kwa uzushi wa mitaani kuwa ripoti eti imenyofolewa kurasa?

Hizo zilizowekwa hapa ni nini?

Na sijaona chochote cha kuonesha wizi wowote kati ya hizi kurasa zilizowekwa hapa.

Nashindwa hata kuwafikiria mkoje, yaani ni zaidi ya misukule.

Mmeamka sasa mnakurupuka tu.
Wenziyo wapo kwenye huu uzi muda mrefu.
Wenziyo wengi walikuwa wamekurupuka hivihivi kama ulivyokuja wewe, baada ya kuelewa kilicholetwa hapa na Invisible sasa hivi hawachangii tena. Najua hata wewe utapotea kwenye uzi huu muda si mrefu. Kwa sasa endelea kutupiatupia tu utujazie space. Chondechonde ku-quote walichoandika wenye akili maana ni kujaza nafasi pasi na sababu.
 
Unafikiri Kama wanaCCM na wazito wasingekuwa na ridhaa juu ya hili Kafulila angefika wapi??

Jiulize swali jepesi tu ... Unakumbuka majibu ya watawala juu ya sakata hili kwenye hatua za mwanzo kabisa lilipoibuliwa na Kafulila?

Je unadhani bila msukumo Wa hao CCM kwenye hili Kafulila angefurukuta? kuna mangapi yanaibuka na kuzimwa bila lolote kutokea?

Je hujiulizi jeuri na kujiamini kwa watawala juu ya majibu waliyotoa awali imepotelea wapi? ni kafulila tu ameweza kuzima jeuri hii? Kama ndiyo mbona mwanzo hakuweza??

Unaamini ni Kafulila pekee anaehangaisha watawala wasilale??

Kama ndivyo fikra zako zilivyo Una safari ndefu Sana kuutambua ulimwengu huu Wa tabu...

Mkuu hapo hujanishawishi kuamini eti ccm wako against hii issue! Nina sababu :
1. Hivi ilikuwa lazima wadhulumiane Kwanza ndipo waamue kuvujisha siri za uharamia huo?

2. Kwanini waanze kuvujisha siri kiuwoga (kupitia mtu asiye Mwana CCM) wakati ccm kama chama tawala kina sekretariati ya maadili, na hili lipo wazi kabisa kuwa limekiuka maadili?

3. Kwanini kama ccm ipo against hii issue sarakasi zimekuwa nyingi, mara vikao vya ajabu ajabu, mara mtishane?

MKUU lusungo ni ngumu sana kuitenganisha CCM na uharamia huu! Mimi ningekuelewa endapo ungesema wana CCM wachache sana wako against huu uharamia!
Ikumbukwe hii saga ipo tangu 2006 imeshatutafuna sana kupitia kodi zetu (overcharges ) kwenda TANESCO, miaka yote tisa ni ccm inatawala, sasa leo ukisema ccm as a chama kipo against huu upuuzi, na watu wakakakuelewa basi me nina safari ndefu ya kuuelewa huu ulimwengu!
Mwisho, jitazame hata wewe humu JF. Miongoni mwa wanaCCM wengi ni wewe unajaribu kupambana na huu uharamia, lakini the least wana msimamo uleule wa kutetea uharamia!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu rejea kauli ya Speaker ndugu Job, aliposema hatuwezi(CCM) kuunda umoja wa wahalifu, maana yake hawawezi kuwa pamoja na wale uliowaita wabunge wa kwenye kamati ambao umefikiri wanaweza kubanwa!! Au kwa lugha rahis watetezi wa ukwapuaji huu!!

Mi nafikiri hilo la kubwana sidhani kama linaweza kutokea kwa sababu CCM wenyewe kwa wenyewe washavurugana,, ndipo inakuja ile dhana ya ukimwaga mboga,,,,,

maccm siyo ya kuamininiwa hata siku moja make lao mara nyingi huwa nikuwaibia wananchi tu, kwani kwa mzalendo wa kweli hawezi kuwa ccm atafukuzwa tu.
 
Sawa sawa kabisa. Unazungumziaje suala la kunyofolewa baadhi ya kurasa ktk ripoti hiyo ya Escrow?

Mkuu,
Suala la Escrow bado linachanganya sana! Je, fedha ni za Serikali au IPTL? Kama ni za Serikali ilikuwaje IPTL ikalipwa? Kama ni za IPTL kwa nini mawaziri, maaskofu, majaji, nk wagawiwe? Na kama hao watu waligawiwa kihalali, mbona wanahaha sana hata kunyofoa kurasa za Ripoti? It is so confusing kwa kweli!!
 
Mmeamka sasa mnakurupuka tu.
Wenziyo wapo kwenye huu uzi muda mrefu.
Wenziyo wengi walikuwa wamekurupuka hivihivi kama ulivyokuja wewe, baada ya kuelewa kilicholetwa hapa na Invisible sasa hivi hawachangii tena. Najua hata wewe utapotea kwenye uzi huu muda si mrefu. Kwa sasa endelea kutupiatupia tu utujazie space. Chondechonde ku-quote walichoandika wenye akili maana ni kujaza nafasi pasi na sababu.

Nimesoma na kusoma na kusoma sijakiona ukisemacho, labda unioneshe wewe, usipinde kilichokuwepo hapo juu lakini.
 
Unafikiri Kama wanaCCM na wazito wasingekuwa na ridhaa juu ya hili Kafulila angefika wapi??

Jiulize swali jepesi tu ... Unakumbuka majibu ya watawala juu ya sakata hili kwenye hatua za mwanzo kabisa lilipoibuliwa na Kafulila?

Je unadhani bila msukumo Wa hao CCM kwenye hili Kafulila angefurukuta? kuna mangapi yanaibuka na kuzimwa bila lolote kutokea?

Je hujiulizi jeuri na kujiamini kwa watawala juu ya majibu waliyotoa awali imepotelea wapi? ni kafulila tu ameweza kuzima jeuri hii? Kama ndiyo mbona mwanzo hakuweza??

Unaamini ni Kafulila pekee anaehangaisha watawala wasilale??

Kama ndivyo fikra zako zilivyo Una safari ndefu Sana kuutambua ulimwengu huu Wa tabu...
Mkuu hii naamini kabisa , kitu ambacho hakina mkono wa baadhi ya wanaccm huwa hakichomozi.
Mfano mzuri ni BMK walishikamana wanachakachua, wakaiba, wakavunja kanuni , marehemu wakavote n.k wapinzani na wananchi wakalia na kusaga meno lakini hawakuambulia chochote.
 
Wewe mama bure kabisa, ni nani aliyekuloga, we na warioba au DR. Salim ni nano anaijua ccm, kwa nn haubadiliki, huyo aliyekuloga nadhani amefariki pole sana

Inahusu nini? Dr. Salim na Warioba, wote kundi moja, bado wana usongo wa kushindwa na Kikwete.
 
JAMANI twende taratibu na pia BUSARA itumike

Nimeiona hiyo report ya CAG, iko numbered Mfano UK 14 kati ya 59, UK 24 kati ya 59 etc.

Sasa kama kweli watanyofoa baadhi ya pages, si itajulikana dhahiri kuwa some pages are missing because the whole document is numbered!

Au hao waliochomoa pages wamepewa pia SOFT COPY hivyo watai number tena upya report?

Kama walionyofoa pages hawatazingatia hayo BASI huu nao utakuwa UCHAKACHUAJI MWINGINE wa KIPUMBAVU kama ule wa marehemu Shida Salum kupiga kura BMK!
 
Mkuu,

Pumzika; lengo si kuvuruga mwenendo wa Bunge bali kuwafanya wanaojaribu kufanya upotoshaji wafahamu kuwa nyaraka nzima ya ripoti ipo tayari kwetu raia na waache michezo yao.

Wawajibishane, kila mtu aubebe mzigo wake. Wanaowajibika na wawajibike; usanii wowote katika hili utachafua hali ya hewa pasi na ulazima wa kufikia huko.

Nadhani tusiendelee, tuliachie Bunge lifanye kazi yake
mkuu kama vp tangaza biashara ili mfuko wa JF uneemeke kidogo, anaetaka mzigo atoe dolari, oooh!
 
Mkuu,
Suala la Escrow bado linachanganya sana! Je, fedha ni za Serikali au IPTL? Kama ni za Serikali ilikuwaje IPTL ikalipwa? Kama ni za IPTL kwa nini mawaziri, maaskofu, majaji, nk wagawiwe? Na kama hao watu waligawiwa kihalali, mbona wanahaha sana hata kunyofoa kurasa za Ripoti? It is so confusing kwa kweli!!

Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa fedha hizo zilizogawanwa zilikwenda kuhifadhiwa Afrika Kusini na Australia. Na kwamba ili fedha zipelekwe huko ni lazima AG aidhinishe. Na hili pia una maoni gani wewe kama wewe pasina kufungamana na upande wowote?

Ukimaliza hapo jumuika na Nguruvi3 hapa chini ili mjadala uendelee:

Mkuu suala hilo halichanganyi kabisa. Intaegemeaunaliangalia kwa jicho gani na upana upi.
1)Kuna fedha za umma za wazi zilizoibiwa(direct or indirect)
2. Kama si fedha za umma, kuna masilahi ya umma yametumikaau kutumiwa kwa jambo lisilo la umma(endapo tutakubaliana si suala la umma)
3)Kuna ukiukwaji mkubwa sana wa maadili. Iweje suala lisilola umma(kama tunakubalina) liwahusishe vingozi wa ngazi za juu, moja kwa mojaau kwa kupitia?
4)Kama umma hauna masilahi, kwanini kuna kujuhudi za kufichasuala hili kwa kutumia ofisi kama za waziri mkuu, mwanasheria mkuu,Ikulu(kupitia katibu kiongozi n.k.)
Kubwa Zaidi jiulize, kama umma hauna masilahi, kwaninitaarifa isiwekwe wazi ili serikali ijisafishe? Kwanini kuna dana dana nyingizisizo na kichwa wala miguu, tena zingine zikihusisha taasisi nyeti kama mahakama?
Sio suala la pesa tu, hili ni corruption. Hebu angaliacorruption ni kitu gani halafu uje utuambie wapi kuna confusion katika sualahili?.
 
Last edited by a moderator:
mkuu Invisible pls kwa hali ilivyo sasa nadhani hujuma kubwa zaidi zinaweza fanyika hata kukata mawasiliano ya mkongo wa taifa wa mawasilino, au hujuma nyingine zozote zitakazokwamisha mawasiliano.

Ni bora umalizie tu mkuu. Hali ishachafuka sana. Kuna uharamia wa miundo mbinu unaweza fanyika tutashanaana hapa mkuu. mi silali naisubiri kwa kweli. hizo page ulizoweka hazisisimui kabisa, wakati bado mnashauriana weka kwanza zile page zenye majina ya Payees.

Umenena vizuri mkuu, naona mkuu Invisible atalifanyia kazi.
 
Last edited by a moderator:
Fuatilia 1st post tu mkuu wangu. It will be updated taratibu
Na wewe unakuwa mtu wa kuingizwa mkenge kirahisi.utajuaje ripoti imechomolewa kabla ya kusomwa?je ikisomwa yote si utajishushia hadhi?ungeacha wanyofoe halafu umwage ndio ungeonekana shujaa
 
Back
Top Bottom