Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Jukumu namba moja la Jeshi la Polisi nchini, ni kuwalinda Raia na mali zao.
Katika mahubiri aliyoyatoa katika sikukuu ya Krismas, Askofu Mwingira wa kabisa la Efatha nchini, alitoa tuhuma nzito Sana kwa vyombo vya serikali, kuwa alinusurika kuuawa mara 3 na akaendelea kueleza kuwa hata yule dada ambaye alikuwa "informer" wake, aliuawa Katika mazingira ya kutatanisha, Katika Hoteli ya Rombo Green View, iliyoko Shekilango!
Pamoja na tuhuma hizo akaendelea kuelezea kuwa vyombo vya serikali viliharibu mali zake zilizoko shambani kwake zenye gharama ya mabilioni ya shilingi.
Sasa ni kwanini Jeshi la Polisi, badala ya kufanyia uchunguzi taarifa hizo, ambazo ziko wazi kabisa, badala yake, kamanda maalum wa Jeshi la Polisi, wa Dar, Jumanne Muliro, anampiga "mkwara" mzito Askofu Mwingira, ajitokeze Katika kituo cha Polisi, ndani ya masaa 24 kwa mahojiano na wameeleza kuwa kama madai yake yataonekana kuwa ni ya uongo, Jeshi la Polisi litamchukulia hatua na kumfungulia mashitaka?!
Hivi ni kitu gani alichoongea Askofu Mwingira, ni kigeni nchini mwetu?
Hivi kama kweli Jeshi la Polisi, liko "serious" na usalama wa Raia wake, hebu nijaribu tu kuwauliza, ni kitu gani kinachowafanya wao, waendelee kusuasua, kufanya uchunguzi wa tukio la kushambuliwa kwa risasi, kwa aliyekuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Tundu Lissu,zaidi ya miaka 4 iliyopita na hakuna hata mshukiwa mmoja aliyekamatwa Ili kuhojiwa, kutokana na tukio hilo la kutisha Sana?
Hivi Jeshi letu la Polisi, linaweza likaeleza walipo watu waliopotea zaidi ya miaka 4 iliyopita, kwa mfano Ben Saanane na mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi, Azory Gwanda?
Hivi Jeshi la Polisi linatufanya watanzania wote ni wajinga na linatofautiana Katika utendaji wake hata na Rais wa nchi, Samia Suluhu Hassan, ambaye alitamka wazi kuwa kuna watu wengi Sana walioumizwa, kutokana na vitendo vya kikatili, vilivyofanywa na serikali ya awamu ya 5 chini ya Mwendazake, Hayati John Magufuli?
Ni hayo tu ninayopenda Jeshi letu la Polisi iyatolee ufafanuzi.