Jeshi la Polisi linachunguza kifo cha mtu mmoja aliyekutwa ameuawa ndani ya gari

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetangaza kuwa linachunguza tukio la kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Felix Josephat Mgeni (47) anayedaiwa kuuawa na mwili wake kukutwa ndani ya gari ukiwa na baadhi ya vitu vingine vya jinsia ya kike.

Akizungumza leo SACP Jumanne Muliro amebainisha kuwa marehemu huyo ambaye ni mkazi wa Kimara Temboni alidaiwa aliuawa maeneo ya Mbezi Luis usiku wa tarehe 14 Julai 2023 majira ya saa 8:15 usiku huku mwili wake ukiwa na jeraha kubwa kichwani kwenye gari namba T.552 DMB Toyota Rav 4.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Mloganzila kwa uchunguzi zaidi na hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa baada ya uchunguzi wa kina.

Chanzo: East Africa Radio

Polisi.png
 
Tulisema mitaa ya mbezi Louis ni jehanamu inayopatikana dar

USSR
 
Jeshi la kanda Maalum ya Dar linachunguza tukio la kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Felix Josephat Mgeni(47) mkazi wa Kimara Temboni anayedaiwa kuuawa Mbezi Luis usiku wa tarehe 14 majira ya saa nane usiku.

Mwili wa marehemu umekutwa kwenye gari aina ya rav 4 huku ukiwa na jeraha kubwa kichwani. Polisi inaendelea na uchunguzi ikiwa ni pamoja na kupeleleza baadhi ya vitu vilivyokutwa eneo la tukio vingine vikiwa vya jinsia ya kike.

Screenshot 2023-07-14 at 14.21.19.png
 
Dah! Naona vifo visivyo na sababu za moja kwa moja vinazidi tu kushamiri nchini.
 
Back
Top Bottom