Mbagala Dar - Mwanafunzi wa Miaka 7 auawa, mwili wake wakutwa msitu wa Jeshi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza tukio la kuuwawa kwa mtoto wa miaka 7 mwanafunzi wa shule ya msingi Kibonde maji B, Mbagala na mwili wake kukutwa tarehe 13 Machi, 2024 kwenye msitu wa Jeshi karibu na Shule aliyokuwa anasoma.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Muliro J. Muliro amesema Mtoto huyo aliondoka nyumbani kwao na mtoto mwenzake tarehe 12 Machi 2024 majira ya 11:30 jioni.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Hospitali ya Polisi Kilwa road kwa uchunguzi zaidi. Ufuatiliaji mkali unaendelea kumtafuta mtuhumiwa/ watuhumiwa waliohusika ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
 
Homicide? Je, Wazazi wake wote wawili (baba na mama ) wanaishi pamoja?

Wana maelewano ndani ya ndoa?

Uchunguzi wa kina kabisa unapaswa kufanyika ili kubaini ukweli, na kwa bahati mbaya zaidi Jeshi letu la Polisi halina vifaa vya kutosha vya kisayansi vya kufanyia Uchunguzi.

Ingekuwa katika nchi za wenzetu pengine ingekuwa tayari wameshawabaini watu waliobeba maiti ya mtoto huyu na kwenda kuitupa katika msitu wa Jeshi, hiyo ingekuwa kazi ya muda usiozidi masaa sita hadi kupata majibu ya uchunguzi.
 
Mtu unatoa wapi ujasiri wa kutoa uhai wa mwengine?

Ushauri: katika maisha yako jitahidi sana usimuamini yoyote. Tembea na kuishi kwa machale always walk looking over your shoulders. Jitahidi kutenda mema na kutii na kufuata sheria za nchi. MTANGULIZE MUNGU KWA KILA JAMBO MAISHANI MWAKO.

Nawachukia nakuwaogopa hawa watu watatu. WAONEVU, WASALITI na WADHULUMATI.
 
Back
Top Bottom