Jeshi la Polisi lapiga marufuku kuwasha fataki mechi ya fainali Yanga vs Usma uwanja wa Mkapa

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Kuelekea mchezo wa kesho Mei 28, 2023 wa fainali Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga na USM Alger ya Algeria itakayopigwa Uwanja wa Mkapa jijini Dar saa 10:00 jioni, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema tayari limechukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema usalama siku ya mchezo utakuwa wa kiwango cha juu maeneo yote ya kuzunguka uwanja ndani, nje na
barabarani.

"Hairuhisiwa mtu yeyote kwenda uwanjani na silaha ya aina yoyote, isipokuwa baadhi ya vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo," amesema

Amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawatahadharisha baadhi ya mashabiki wenye tabia ya kuwasha fataki au baruti uwanjani, kurusha chupa au kitu chochote.

Ameeleza kuwa hayo ni baadhi ya makosa ya mambo ya kiusalama kwenye viwanja vya soka.

"Jeshi la Polisi halitavumilia tabia hizo na zingine ambazo zimepigwa marufuku na vyama vya soka FIFA, CAF na TFF. Watakao kaidi, watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Jeshi la Polisi linawatakia mashabiki wa soka kushangilia kistaarabu,"amesema.
 
Wametunyima uhuru sisi mashabiki kindakindaki wa timu pendwa na bora kwa sasa Afrika USM ALGER
 
"Jeshi la Polisi halitavumilia tabia hizo na zingine ambazo zimepigwa marufuku na vyama vya soka FIFA, CAF na TFF. Watakao kaidi, watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria"

Soma hiyo paragraph hapo juu,
Polisi wanatimiza tu majukumu yao.
Ehhh, ila polisi bhana
 
Back
Top Bottom