DOKEZO Jeshi la Polisi Arusha limchukulie hatua Askari huyu aliyempora Mwandishi kamera akiwa kazini

DOKEZO Jeshi la Polisi Arusha limchukulie hatua Askari huyu aliyempora Mwandishi kamera akiwa kazini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Usiku wa kuamkia leo Septemba 9, 2025 katika maeneo ya Washington karibu na Stand Ndogo Jijini Arusha, kulitokea tukio la kusikitisha ambapo Mwandishi aliyekuwa akitekeleza majukumu yake alivamiwa na askari anayefahamika kwa jina la Inspekta.... (jina linahifadhiwa kwa sasa) kutoka Kitengo cha Mifugo.

Katika video inayoonyesha tukio hilo, Inspekta huyo anaonekana akivuka barabara na kumfuata mwandishi kwa lengo la kumpora kamera.

Tukio hilo lilitokea wakati Wananchi wakishuhudia kibaka aliyekuwa amechomwa moto, ambapo Waandishi walikuwa kazini kama kawaida kurekodi na kuripoti tukio hilo.

Baada ya kushindwa kutekeleza azma yake kufuatia kelele za Wananchi, askari huyo alikimbilia kwenye gari, huku akiwa anaashiria kuwa huenda alikuwa amelewa. Waandishi walijaribu kumjulisha Kamanda wa Polisi kuhusu tukio hilo kwa kumpigia simu, lakini mara tu walipojitambulisha kuwa ni Waandishi, simu ilikatwa ghafla.
‎‎

‎Baada ya tukio hilo, Waandishi walichukua hatua ya kuelekea Kituo cha Polisi cha Central kufungua jalada dhidi ya askari huyo, lakini walizuiwa getini na askari aliyekuwa na silaha pamoja na OCCD.

Walipomweleza kuhusu tukio hilo, OCCD ambaye pia alikuwepo eneo la tukio usiku huo, alidai kuwa hakushuhudia askari huyo akijaribu kupora kamera.

Waandishi walipoomba kufungua jalada, waliambiwa warudi kesho, jambo lililowafanya waulize kama kuna muda maalum wa kufungua jalada Polisi badala ya kupatiwa majibu ya msingi, waliambulia kufukuzwa kituoni kama watu wasio na haki.

Kutokana na hali hiyo, tunaomba kujua hatua gani zitachukuliwa dhidi ya Inspekta huyo, kwani ni jambo la kusikitisha kuona usalama wa waandishi ukivunjwa na wale wanaopaswa kuwalinda.

Ushirikiano kati ya askari na Waandishi ni muhimu, lakini vitendo kama hivi vinavuruga uhusiano huo na kuibua maswali
 
wewe mwenyewe hutaki mtaja jina ila unataka achukuliwe hatua
 
Hao waandishi na jeshi wote akili zao zinafanana siku hizi!
.
Angalia nchi iko kwenye kipindi cha uchaguzi lakin media ziko busy na simba na yanga!
 
Mwandishi wa habari unakuwa muoga kumtaja jina huyo askari
 
Hao wote hawana Faida kwa Watanganyika
 
Kajamaa kenyewe choka mbaya, kaone haka
 

Attachments

  • Screenshot 2025-09-04 111503.png
    Screenshot 2025-09-04 111503.png
    527.7 KB · Views: 20
Rekebisha tarehe mkuu Sept 9 2025 bado hatujafika.
 
Wandishi wa Habari hawana msaada wapigwe tuu, Wamewekwa mfukoni na Wahuni hadi wanashindwa kutetea Utekaji, kufinya demokrasia wamekalia udakuu tuuu. Mbwa kala mbwaa tu hapo
 
Usiku wa kuamkia leo septemba 9,2025 katika maeneo ya Washington karibu na Stand Ndogo Jijini Arusha, kulitokea tukio la kusikitisha ambapo Mwandishi aliyekuwa akitekeleza majukumu yake alivamiwa na askari anayefahamika kwa jina la Inspekta.... (jina linahifadhiwa kwa sasa) kutoka Kitengo cha Mifugo.
Mkuu,kwani wewe unaishi Washington ipi hasa ambayo leo hii ni tarehe hiyo?
 
Back
Top Bottom