Jeshi la Polisi linaendeleza hofu ya utekaji nchini

Jeshi la Polisi linaendeleza hofu ya utekaji nchini

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,908
Reaction score
3,231
4065b565-f6ee-4e62-ba94-7c4820129ae2.jpg
13d0ca5e-6555-4cd6-b085-45626772b982.jpg

Tukio la kukamatwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa Malori Tanzania (TATAMATA), Godlove Materu limerejesha hofu ya utekaji nchini, kutokana na mtindo wa ukamataji unaofanywa na Jeshi la Polisi nchini.

Materu Materu (45), ambaye ni mkazi wa Chapwa, Mji wa Tunduma, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Songwe, alikamatwa na askari Polisi tangu Februari 5, 2026. Lakini polisi hawakusema chochote na viongozi wa TATAMATA walikwenda kuuliza polisi wakaambiwa hakuna taarifa ya kukamatwa kwake.

Lakini Februari 8 baada ya viongozi wa TATAMATA kutishia kuanza mgomo ifikapo Februari 10, polisi wamekuja haraka kukiri kwamba walimkamata, huku wakitoa ufafanuzi.

Hapa ndipo tatizo linapoanzia. Kwa nini polisi wasingetangaza kumkamata Materu siku ile ilikuondoa hofu zisizo za lazima? Ikiwa polisi waliokuja kumkamata walikuwa wamevaa kiraia na hakuna taarifa yoyote ya kukamatwa kwake, kwa nini watu wasiseme kwamba amechukuliwa na watu wasiojulikana?

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe inaeleza kuwa Materu anatuhumiwa kupanga kufanya uhalifu katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Tunduma na viunga vyake, lakini hawataji uhalifu gani au ni kosa gani ili kama linadhaminika adhaminiwe.

Kwa nini polisi wanaficha kukamatwa kwa mtu, wakati angeweza kupata msaada wa kisheria ikiwa pamoja na kudhaminiwa na kupata huduma nyingine muhimu.

Halafu polisi wanataka watu wapuuze taarifa zinazosambaa, wakati wenyewe ndio wanaficha taarifa.

Kwa kuwa Materu ni kiongozi wa chama, huyo ni mtu mkubwa, ni mtu maarufu, kukamatwa kwake hakupaswi kuwa siri.

Utendaji huu wa Jeshi la Polisi ndio umekuwa ukiendeleza hofu za utekwaji. Watu wengi wametekwa na kupotezwa baada ya kukamatwa kwa mtindo huo huo. Watu waakuja wakiwa kiraia, wanakamata mtu na kuondoka naye. Polisi wakiulizwa wanasema hawana taarifa.

Ndio walivyopotea kina Deusdedit Soka na wenzake, kina Mdude Nyagali na wengineo wengi.

Ukamataji huo umekuwa ukiwalenga zaidi wakosoaji wa Serikali.

Ndio maana aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene alizungumzia suala hilo Desemba 8, 2025, alipokuwa akizunguza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Alimwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, Camillus Wambura, kuhakikisha kuwa ukamataji wa watuhumiwa unafanyika kwa kufuata misingi ya sheria na kwa kuzingatia staha.

Alisema aina ya ukamataji unaofanywa na baadhi ya askari ikiwemo kuvaa kininja, kutovaa sare rasmi za polisi na kwenda kuwakamata watuhumiwa majumbani usiku haukubaliki na unapaswa kusitishwa.

Sasa kama mtu anakamatwa na watu wasio na sare, haambiwi kosa lake na hata ndugu zake hawaambiwi, utajuaje kama atatendelewa haki? Mtu huyo akifia mikononi mwa polisi maana yake ndiyo amepotea moja kwa moja.

Ni jambo la hatari, lakini ndio ababu ya watu wengi kupotea wakiwamo kina Ben Saanane, Azory Gwanda, Simon Kangoye na wengineo wengi.

Ni miongoni mwa mambo yanayoondoa Imani ya wananchi kwa Jeshi la Polisi.
 

Attachments

  • 4065b565-f6ee-4e62-ba94-7c4820129ae2.jpg
    4065b565-f6ee-4e62-ba94-7c4820129ae2.jpg
    10.6 KB · Views: 25
Haliendelezi hofu bali limeshindwa kabisa kuacha.. Zaidi linazidi kututhibitishia watekaji ni akina nani

Kweli nimeamini ukianza kula nyama ya mtu huwezi kuacha
 
Shida siyo hao pimbi, shida ni mama yao mbogamboga ndiye anaichafua nchi.
 
Back
Top Bottom