Jerusalem: Sababu tatu za kuzuka kwa ghasia kati ya Wapalestina na Wayahudi

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,891
155,893
Ghasia zilizuka nje ya msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa zamani wa Jerusalem

REUTERS: Ghasia zilizuka nje ya msikiti wa Al-Aqsa katika mji wa zamani wa Jerusalem

Jerusalem imekuwa ikigonga vichwa vya habari kufuatia ghasia ambazo zimekuwa zikiripotiwa mjini humo kati ya Wapalestina na vikosi vya usalama vya Israeli ambazo zimewaacha mamia wakijeruhiwa mbali na mshambulizi ya kulipa kisasi kutoka pande zote mbili yakiripotiwa.

Ghasia hizo ziliongezeka siku ya Jumatatu usiku baada wanamgambo wa Kipalestina kurusha roketi kutoka ukanda wa Gaza hadi Jerusalem.

Kundi la wanamgambo la Hamas limetishia kuwashambulia maafisa wa polisi wa Israel baada ya mamia ya Wapalestina kujeruhiwa katika eneo takatifu la Waislamu mjini Jerusalem siku ya Jumatatu.

Likijibu, Jeshi la Israel lilifanya mashambulizi ya angani dhidi ya ngome za wanamgambo katika ukanda wa Gaza.

Maafisa wa afya wa Palestina katika eneo la Gaza wanasema kwamba watu 22 wakiwemo watoto waliuawa katika shambulio hilo.
Jeshi la Israel limesema kwamba takriban wanachama 15 wa kundi la Hamas linalotawala Gaza ni miongoni mwa waliokufa.

Roketi zilirushwa kutoka Gaza hadi Jerusalem siku ya Jumatatu

REUTERS: Roketi zilirushwa kutoka Gaza hadi Jerusalem siku ya Jumatatu

Siku ya Jumanne, Shirika la haki za kibinadamu la Palestina Red Crescent, liliripoti kwamba zaidi ya Wapalestina 700 walijeruhiwa katika ghasia hizo na maafisa wa usalama wa Israel mjini Jerusalem na eneo la West Bank.

Hizi hapa sababu tatu zilizopelekea kuzuka kwa mzozo huo.

1. Siku ya kusherehekea Jerusalem​

Jerusalem imeshuhudia ghasia ambazo hazajiwahi kutokea tangu wikendi ya 2017, zikisababishwa na jaribio la muda mrefu la Wayahudi kujaribu kunyakua nyumba za familia za Kipalestina katika eneo lililonyakuliwa na Israeli la mashariki mwa Jerusalem.
Ghasia hizo za Jumatatu zilizuka nje ya msikiti wa Al Aqsa , katika mji wa zamani wa Jerusalem.

Wapalestina waliwarushia mawe maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia kutoka Israel ambao nao walijibu kwa kuwarushia risasi bandia za mipira na vitoa machozi .

Shirika la haki za kibinadamu la Palestina Red Crescent lilisema siku ya Jumatatu kwamba zaidi ya watu 300 walijeruhiwa.

Vikosi vya polisi vya Israel vilisema kuwa idadi kubwa ya maafisa wa polisi ilijeruhiwa pia.

Zaidi ya Wapalestina 300 walijeruhiwa wakati wa ghasia za siku ya Jumatatu

Zaidi ya Wapalestina 300 walijeruhiwa wakati wa ghasia za siku ya Jumatatu

Msikiti wa Al Aqsa upo katika eneo takatifu linalojulikana na Waislamu kama Haram al Sharif, na Hekalu la Mlimani kwa Wayahudi.
Vikosi vya polisi wa Israel vilisema kwamba maelfu ya Wapalestina waliweka vizuizi katika eneo hilo wakitarajia kutokea kwa ghasia wakati wa maandamano ya Kiyahudi siku ya Jumatatu ili kuadhimisha siku ya Jerusalem.

Maandamano hayo yanaadhimisha hatua ya Israel kunyakuwa eneo la mashariki la Jerusalem 1967 , wakati wa vita vya siku sita ambapo ilifanikiwa kuchukua udhibiti wa mji wote.

Mji huo wa zamani upo mashariki mwa Jerusalem , ikiwa ni nyumbani kwa baadhi ya maeneo matakatifu ya kidini duniani ikiwemo:

Msikiti wa Al-Aqsa, Hekalu la mlimani, Ukuta wa magharibi wa dini ya Wayahudi na kanisa la Wakristo la mtakatifu Sepulcher.

Na eneo hilo linatambulika kuwa mji mtakatifu na Wayahudi, Wakristo na ni mji wa tatu mtakatifu katika Uislamu.

Hatma ya eneo la Jerusalem mashariki ndio kiini cha ghasia kati ya Israeli na Wapalestina na kila upande unapigania haki yake.

Israel inasema kwamba eneo lote la mji huo ni mji wake mkuu , ijapokuwa hilo halitambuliwi na jamii ya kimataifa , na Wapalestina wanadai kwamba eneo hilo ndio mji mkuu wa taifa la Kipalestina litakaloundwa katika siku zijazo.

Wakati wa maandamano hayo ya kuadhimisha siku ya Jerusalem, mamia ya vijana wa Israel walipeperusha bendera na kuelekea katika maeneo hayo ya Waislamu , wakiimba nyimbo za kizalendo.

Wapalestina wengi wanachukulia hatua hiyo kama uchokozi.

Polisi wa Israel walitembelea eneo hilo kuamua kuwapiga marufuku Wayahudi wakati wa maadhimisho ya siku ya Jerusalem.

Maandamano ya kuadhiisha siku ya Jerusalme yanaadhimishwa kufuatia hatua ya Israel kunyakua mji huo

Maandamano ya kuadhiisha siku ya Jerusalme yanaadhimishwa kufuatia hatua ya Israel kunyakua mji huo

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitetea ulinzi uliowekwa.

"Hii ni vita kati ya wavumilivu na wasio na uvumilivu, kati ya wasiofuata sheria na wanaofuata sharia," alisema.

"Wale wanaotaka kuchukua haki zetu mara kwa mara hutulazimisha kusimama kidete, kama maafisa wa polisi wa Israeli wanavyofanya."

Kwa upande wake rais wa Palestina Mahmoud Abbas alishutumu vitendo vya Israel.

"Shambulio la kinyama la vikosi vya Israel dhidi ya waumini waliokuwa katika msikiti mtakatifu wa Al Aqsa na maeneo yake ni changamoto mpya kwa jamii ya kimataifa," alisema msemaji wake Nabil Abu Rudeineh.

2. Uwezekano wa kuzifurusha familia za Wapalestina

Wimbi jipya la ghasia linatokana na juhudi za siku nyingi za Wayahudi kuzifurusha familia kadhaa za Kipalestina kutoika katika makazi yao karibu na wilaya ya Sheikh Jarrah mashariki mwa jerusalem.

Jerusalem ilishuhudia ghasia mbaya zaidi tangu 2017

Jerusalem ilishuhudia ghasia mbaya zaidi tangu 2017
.​

Umauzi wa mahakama mwaka huu uliounga mkono kufurushwa kwao ulizua shutuma kutoka kwa Wapalestina.

Mahakama ya kilele nchini Israel ilikuwa inatarajiwa kusikiliza kesi siku ya Jumatatu lakini kikao hicho kikaahirishwa kutokana na ghasia hizo.

3. Hali ya hofu wakati wa Ramadhan

Wimbi hili la ghasia linajiri katika siku za mwisho za mwezi mtukuafu wa Ramadhan.

Kizuizi cha Ramallah

Hofu ilitanda tangu kuanza kwa mwezi wa Ramadhan katikati ya mwezi Aprili , huku kukiwa na msururu wa matukio ambayo yamesababisha ghasia.

Wakati Ramadhan ilipoanza , ghasia za usiku zilizuka kati ya polisi na Wapalestina wakipinga vizuizi vilivyoweka nje ya lango kuu la Damascus katika mji wa zamani wa Jerusalem ambalo lilikuwa limewazuia kukongamana eneo hilo usiku kucha.

Lakini ghasia hazikutokea Jerusalem pekee kwani sehemu nyengine pia zilirekodiwa katika mji wa Haifa , Kaskazni mwa Israel na mji wa karibu wa Ramallah katika eneo la West Bank.

Wapatanishi wa mashariki ya kati , wakiwemo Marekani, muungano wa Ulaya, Urusi na Umoja wa Mataifa wameonyesha kukerwa na ghasia hizo na kutoa wito kwa pande husika kuvumiliana.

CHANZO: BBC Swahili
 
Ndugu yangu usipotoshe ukweli hivi unajua mmiliki wa huo mji,au unajua mji mkuu wa Israel,na Jerusalem unajua inamilikiwa na inchi gani?punguza chuki,na unajua hao waisreli ni dini gani?
Ukishakujaga mjadala wa kuzungumzia Israel waislam weng hua mnakimbilia kutuambia kua Israel sio wa kristo ni wayahudi, lakini Israel ina dini zote km yalivyo mataifa mengine na wapalestine pale ni wahamiajI.

Ingekua ni mji wao usingeitwa Jerusalem sema akili kichwani hamna nyie, na naomba Israel iwatandike kisawa sawa akili ziwakae saws, mmejaza ujinga kichwani mnawaza vita mda wote.
 
Dunia nzima waislam akili zao ni moja wanawaza fujo mda wote kuua kuandamana kujitoa mhanga,
Kusingekuwepo uislam tungekaa kwa aman sana ila nashukuru mungu aliwapa nguvu Israeli, na wazungu maana wanashughulikiwa kisawa sawa very good
Vipi na Africa ya kati ni waislamu? Vip na bosnia ni waislamu ?? Chechnya pia ni waislamu?
 
Nini chanzo cha haya yote, tangu tukiwa watoto mpaka sasa tu watu wazima tunasikia Israel, Palestina na ukanda wa Gaza, mara wakristo, wayahudi na waislamu, naomba mwenye habari kamili ya hii vita isiyo na mwisho atupe series yake.

Hawa wakristo na wayahudi wanatofautiana wapi wakati wote asili yao ni hapo? Hawa wayahudi wanatofautiana wapi na wapalestina kama wote ndiyo wenye nchi?
 
Dunia nzima waislam akili zao ni moja wanawaza fujo mda wote kuua kuandamana kujitoa mhanga,
Kusingekuwepo uislam tungekaa kwa aman sana ila nashukuru mungu aliwapa nguvu Israeli, na wazungu maana wanashughulikiwa kisawa sawa very good
Ni kweli kabisa ndg maana hao waislam ndo wanaosababisha mnaabudu masanamu,mnaruhusu ndoa jinsia moja.
 
1620796843018.png


Hawa jamaa naona kama kila kitu utata, hata ramani haieleweki,
  • Palestina hapo iko wapi hapa kwenye ramani?
  • Ukanda wa Gaza nao ni upi?
  • Yordani nayo ni kama nchi lakini haina mji mkuu
  • Nani anagombania nini hapo?
 
lakini Israel ina dini zote km yalivyo mataifa mengine na wapalestine pale ni wahamiaj tu
Mkuu natamani sana kuijua hii historia maana huwa sielewi hao wapalestina walitokea wapi mpaka kwenda kuvamia nchi ya watu? Na wao waisrael walikuwa wapi mpaka wapalestina wanajenga mizizi
 
HAO waisrael NI wakimbizi.
Dunia nzima waislam akili zao ni moja wanawaza fujo mda wote kuua kuandamana kujitoa mhanga,
Kusingekuwepo uislam tungekaa kwa aman sana ila nashukuru mungu aliwapa nguvu Israeli, na wazungu maana wanashughulikiwa kisawa sawa very good
 
  • Thanks
Reactions: Lob
Dunia nzima waislam akili zao ni moja wanawaza fujo mda wote kuua kuandamana kujitoa mhanga,
Kusingekuwepo uislam tungekaa kwa aman sana ila nashukuru mungu aliwapa nguvu Israeli, na wazungu maana wanashughulikiwa kisawa sawa very good
Worse is those who believe the oppressor's word over the victim's.
 
Back
Top Bottom