Jerry Silaa anaweza kupunguza matapeli Ardhi? Wana mtandao, wamejazana wizarani, wana makampuni!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
Kwenye ardhi kuna utapeli wa kila aina ndio mana lukuvi alipokuwa waziri wa ardhi alipiga marufuku baadhi ya makampuni yaliyokuwa yanapima viwanja na kuuza maana walisababisha migogoro mingi sana ya ardhi.

Viwanja vinatangazwa kwenye maspika katika vituo vya daladala kama vile nguo za ndani zinavyotangazwa Kariakoo na Kiboroloni huko Moshi.

Mwaka juzi kuna kampuni ilinunua eneo bulka mateves arusha na likapima viwanja likauzia watu kumbe lile eneo lilikuwa na mgogoro na kesi ilikuwa mahakamani wanunuzi walilipia garama zote wakapata hadi hati na wakaanza ujenzi

Wasijue kilichokuwa kikiendelea yule mtu alieuzia kampuni eneo aliendelea kubuy time mahakamani akikataa rufaa lakini alishindwa

Ndipo mwenye eneo halisi baada ya kushinda kesi akawavamia wanunuzi akitaka waondoke kwenye eneo lake na hapo ndipo paliibuka mgogoro mkubwa sana wakidai wao wana hati na wanamiliki eneo kihalali wakaenda kwenye ofisi ya kampuni iliyowauzia ikawashauri wafungue kesi na wao watasaidia kutoa ushaidi

Wakafungua kesi kupinga kuondolewa kesi ilipoanza kusikilizwa na ushaidi kupelekwa mahakamani ikagundulika wanunuzi japo wana hati miliki ya eneo lakini si wamiliki halali na ununuaji wao ni batili kwa sababu walinunua eneo likiwa na kesi mahakamani tayari mahakama ikaamua hati zao zifutwe na waondoe nyumba walizojenga ili mmiliki halali afanye matumizi kwenye eneo lake wakarudi kwenye ofisi iliyowauzia viwanja wakakuta wamekimbia na simu zimezimwa

Angalizo makampuni haya yanayouza viwanja mengine hayana hata usajili hivyo wewe mnunuzi ukipata matatizo inakuwa ngumu kupata pesa yako

Unaponunua viwanja kwenye majiji makubwa kuwa makini mno utapeli ni mwingi sana na watu wanalia kila siku watu wanauza hadi viwanja vya marehemu wakati mirathi iko mahakamani.

Mwingine mtu na mme wake wanakula njama mume anauza kiwanja na hati ina jina lake kabisa ukilipa pesa tu baada ya mwezi mke wake anaibuka anapeleka pingamizi mahakamani hakushirikishwa kwenye manunuzi wakati mali hiyo walichuma wote

Utapeli ni mwingi sana
 
Kwenye ardhi kuna utapeli wa kila aina ndio mana lukuvi alipokuwa waziri wa ardhi alipiga marufuku baadhi ya makampuni yaliyokuwa yanapima viwanja na kuuza maana walisababisha migogoro mingi sana ya ardhi...
Hivi yule jamaa unaomuona yuko timamu

USSR
 
Back
Top Bottom