Samia tangu arithi Urais 2020's, Jerry Silaa Pekee ndio mtendaji, Wengine wapeni jina!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,047
20,411
Jerry Slaa pamoja na mapungufu yake kisiasa hasa kulaumiwa kwa ubovu wa Barabara za Kivule na Gongo la Mboto kitu ambacho kinahitaji bajeti kubwa na inatoka kwenye wizara na ni nje ya uwezo wake, amejifumua uozo na urasimu uliopo kwa makamishan wa ARdhi Pale Wizarani Dar es salaam na Kibaha mkoani Pwani.

KAZI ALIZOFANYA JERRY TANGU APEWE WIZARA ARDHI
  1. Kutatua mgogoro kituo cham mafuta kilichojengwa makazi ya watu Mikocheni pale Rose garden.
  2. Kurudisha kiwanja kilichokuwa kimeporwa kwa mwananchi huko kunduchi beach mwaka 2006 na kuuziwa tajiri wa mahoteli ya kitalii, Hati ilifutwa na kupewa tajiri, Jerry kaagiza arudishiwe.
  3. Kazui rushwa kubwa inayopenyezwa kwa makamisha wa ardhi pale wizarani.
  4. Anasikiliza kero na kwenda Saiti tofauti na alivyokuwa Anjela Mabula .
MADHAIFU YA JERRY SLAA.
  1. Ameshindwa kugundua kuwa viwanja karibu vyote vya mradi jiji la Dar es salaam huwa watumishi wa ardhi wanajimilikisha kisha kuanza kuviuza kwa bei kubwa. Kijichi, Changanyikeni- mikwambe, Kigamboni na maeneo mengine watumishi huandikisha majina ya ndugu zao kwa siri na kuumia NIDA zao, kisha huviuza tena kwa bei kubwa. Pale Ardhi kuna mfagizi tajiri kuliko mtumishi wa serikali taka seniour. Mfagizi ndio mpiga dili zote za makamishna na hela za Rus*** zinpita kwake.
  2. Mabara ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kutaja machache, lile la Moshi Mjini pale kwa mkuu wa Mkoa kuna wenyevit wamefanya ni mali yao binafsi, wanaendesha watakavyo na limejaa dhulma na rushwa . Baraza la Kinondoni- Mwananyamala kuna mwenyekiti ametokea Moshi amekuja kwa ukali na kutenda haki, alifaa azungushwe kwenye mikoa yote kila bada ya miezi sita, awafundishe matapeli kuwa serikali iop macho . Barazala Ardhi la Ilala kuna mwenyekiti na Mama Fulani ananzia na Bii, huyu ni mkorofi, anadharau wananchi, anatukana mawakili na hata wazee, hafai kuwa kabisa kwenye baraza.
  3. Ameshindwa kuzuia rushwa iliyopo kwenye utoaji wa vibali vya ujenzi, mwananchi akitaka anaambiwa alipie kikao cha madiwani.
  4. Ameshindwa kuzia vituo vya mafuta vinavyojengwa kwenye makazi ya watu, na vingi katika eneo moja la wananchi.
  5. Ameshindwa , baada ya kugundua hati kufutwa na kumilikishwa matajiri, kuenelea kufuatilia wapokeaji wa hizo rushwa na kuchunguza kama mali walizonazo zinaendana na mshahara wa wizara.
  6. Ameshindwa kabisa kuwahamisha makamishna waliojiwekea mizizi ya kufanya kazi za makampuni makubwa na kuacha kazi za watu binafsi kulala , hii ndio inasababisha jam pale wizarani.
  7. Ameshindwa kufunga CCTV CAMERA kwenye kila eneo la wizara, ku monitor utendaji wa watumishi, yaani unaona meza ila hakuna mtu, ukiuliza hupewi jibu na huwa wanatunziana.

URASIMU NA UOZO ULIOPO WIZARANI:
Makamishana wamejigeuza miungu watu, kumuona Waziri Slaa na kukusikiliza ni rais sana kulinganisha na kamishan wa Ardhi. Makamishna, vijana wadogo tu wamegeuza kuwa juu ya serikali- ukiwa na tatizo wanakwambai ni siku 2 tu za wiki na hiyo siku ukiwahi sa 12 asubuhi kumuona ni saa 8 mchana.

Ukipelekana nyaraka kuomba transfer, wanzungusha, chelewesha mpaka ile valuation report ina expire na mtu anaambiwa arudie kufanya valuation.Hizi ni gharama zisizo na maana na wakikwambia urudie wanakwambia kabisa kama unataka iende haraka kuna mtu wao [mtumishi wa wizara anaipga chap], ndani ya wiki valuation inakamilika na transfer inafanyika. Hapa mtumishi wa wizara anaondoka ofisini kufanya kazi binafsi kwa vifaa vya serikali.

DEED POLL AND POWER OF ATTORNEY NA MORTAGE.
hiki kitengo si kuoza tu, kinanuka rushwa, Tenda ya Serikali inatangazwa na wanasema moja ya Sharti lazma kuwe na power of Attorney iliyosajiliwa. Muda wa Tenda ni siku 14 tu tangu kutangazwa. Mtu ananda , anaenda kusajili anaambiwa inatka ndani ya siku 14 za kazi na kiuhalisia ni siku 21 na wakijua ni ya Tenda ndio haitoki. Hapa inabidi wote wanao omba tenda wapitishe 100,000 ili Dokumenti itoke ndani ya sikun moja.

KUJIPANGIA MUDA WA KAZI AMBAO SI WA SERIKALI.
Pale utakuwata wamweka mashtarti yao, mara sijui mwisho saa nane, mara sa sita sijui ndio mwisho wa kitu gani, sasa mtu ametoka mkoani amekuja Dar na anajua mudda wa kazi wa kiserikali mwisho ni saa tisa na nusu, anafika anaambiwa na walinzi hakuna kuingia, huu ni urasimu uliopitiliza, Jerry Slaa naomba uangalie hili.

View: https://www.youtube.com/watch?v=eM17bphvZ0U

View: https://www.youtube.com/watch?v=Ty6dT6-htLwhttps://www.facebook.com/watch/?v=321675367118567


View: https://www.facebook.com/watch/?v=321675367118567https://www.youtube.com/watch?v=Ovm5fnVtJKA


View: https://www.youtube.com/watch?v=Ovm5fnVtJKA



NB: Jerry Slaa kwa kipindi kifupi , akipewa ushirikiano anakuja kuwa kama SOKOINE
 
Back
Top Bottom