Jenerali Ulimwengu na gazeti Jipya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jenerali Ulimwengu na gazeti Jipya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mafuchila, Oct 25, 2007.

 1. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2007
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Gazeti jipya kabisa la Kiswahili linatarajiwa kuingia katika vibanda, maofisi, na mitaa ya Tanzania kuanzia tarehe 31 Oktoba mwaka huu. Jarida hilo la "Raia Mwema" litakuwa na habari mbalimbali zikiwemo za uchunguzi, utafiti, siasa, biashara, maoni n.k Jarida hilo liitwalo "Raia Mwema" limeanzishwa kutokana michango ya hali, mali, na vipaji ambavyo vimekusanywa chini ya Mhariri wake Mtendaji John Bwire

  Kuanzishwa kwa jarida hilo ni alama ya kuvunjika rasmi kwa ndoa ya gazeti lililosifika sana nchini miaka hiyo la "Rai".

  Waandishi waanzilishi wa gazeti la Rai - ukiondoa Dr. Shoo na Salva - na waandishi wengine ndani na nje ya Tanzania wamefikia uamuzi wa kuanzisha gazeti hilo wakizingatia haja ya kupanua uhuru wa maoni, habari na mawazo na kuchangia kwa namna ya pekee kuhamasisha kizazi kipya cha "Raia Wema". Gazeti hilo litakuwa linatolewa kila wiki.

  Gazeti hilo litajumuisha waandishi mbalimbali wakiwemo:

  Jenerali Ulimwengu
  Issa Shivji
  Padre Karugendo
  Prof. Haroub Othman
  Maggid Mjengwa
  Joseph Mihangwa

  na wengine wengi ambao mtapata bahati ya kusoma kazi zao kwenye gazeti hilo ambalo litapatikana pia kwenye mtandao wakati huo.

  Napenda kutoa pongezi kwa ushirikiano wote wa wale ambao wamewezesha gazeti hili kupata mtaji, kibali, na nyenzo za kutendea kazi.. Natarajia kuwa toleo la kwanza litaiweka fani ya uandishi katika ngazi nyingine kabisa nchini.
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,165
  Likes Received: 1,251
  Trophy Points: 280
  Tunalisubiri Kwa Hamu, Maana Kuna Watu Wanajaribu Kunyamazisha Uhuru Wa Kutoa Maoni Ya Watu Kwa Kutumia Fedha Zao.
   
 3. m

  mkama Member

  #3
  Oct 25, 2007
  Joined: Oct 19, 2007
  Messages: 67
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo timu inatisha hasa.Hivi mabo ya uraia wa Jen.Ulimwengu yalishatulia?Tutaona mageuzi makubwa ya uandishi wa habari kwelikweli.

  Nashauri mwanakijiji uombe kazi maaana hata wewe makala zako huwa ni babu kubwa na zinaweza kwenda speed ya hao jamaa
   
 4. S

  Semanao JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2007
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 208
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mbona hizi taarifa zilishawekwa zamani na mwanakijiji? au hii ni kwa msisitizo.
   
 5. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #5
  Oct 25, 2007
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Bila shaka Mzee mwenzetu Mwanakijiji atalisikiliza ombi na kulifanyia kazi. Kinachofurahisha hapo hiyo timu haina bei, hivyo hata kuinunua mhmmm.
   
 6. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #6
  Oct 25, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nawapa tano,ila wa zaidi ni mtengeneza web wao anaonekana kuwa ni mtu makini sana na litapendeza sana ,je?litakuwa ni kila wiki ama ni kila siku?
   
 7. p

  princejafari Member

  #7
  Oct 26, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 44
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii safu ya wachangiaji imetimia. intellectually na 'kiuzalendo pia'. manake issue za manyang'au wetu ni kwamba sio kwamba hawana akili bali wameamua kutumia akili zao kulidhulumu taifa kama kuku nayekula mayai yake mwenyewe. shivji ni mwalimu wangu, hana cha msalie mtume. haroub ni mwalimu wangu pia. these guys are clean and intellecually 'sizzling'
   
 8. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2007
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  http://www.raiamwema.co.tz
  Waugwana haya jamani kimya kingi kina mshindo..kina majjig mjegwa wamo humo...Joseph mihagwa utawapata....kazi kwenye check web site hiyo.
  Regards
   
 9. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #9
  Oct 31, 2007
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nimeona Ni Nzuri Lakini Rangi Zake Zinautata Halafu Wametumia Template Kutengeneza Tovuti Husika , Hawajaweka Majukwaa Huru Ya Watu Kuchangia Na Kuchambua Habari Zinazotolewa Na Gazeti Hilo

  Subiri Kidogo Tutaichambua Zaidi Baada Ya Kukaa Kuiangalia Inavyofanya Kazi
   
 10. M

  Mtu JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2007
  Joined: Feb 10, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndio mwanzo mkuu wape muda kidogo....sema kuhusu maandishi ya mule ndani.
   
 11. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #11
  Oct 31, 2007
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ndio najua ni mwanzo lakini mwanzo wenyewe uwe wa kishindo basi , mfano kama mimi nilivyoangalia page za mwanzo tu nimeshakatishwa tamaa kwa sababu haina mambo mengi ambayo tovuti ya habari inatakiwa iwe nayo , tovuti hii ni sawa tu na ile ya freemedia muonekano wake kasoro vitu kidogo lakini mengi yanaendana na freemedia

  Maandishi ni mazuri kwa sabababu wamekutana na waandishi mashuhuri lakini kaka kuendesha tovuti sio sawa na gazeti , tovuti watu wanataka kuchangia ambao wako nje wanataka kuchangia na hapo hapo waone walichochangia sio wanachangia unahifadhi katika database mambo kama hayo

  Tuko kule kule RAIA MWEMA LAKINI SIO WAZI NA WA HAKI

  NDIO NINI
   
 12. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2007
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Yes Good point Shy.
  Ndio imetolewa juzi juzi tu...kwa hiyo inaonekana toka walipojitoa kwenye Rai...walikuwa wamekaa wanakuna vichwa kuona watoke vipi.Hii inawezekana ukawa ni mwanzo.Na mie nimeangalia sehemu ya kuweka maoni sijaiona zaidi ya ile tuwasiliane.I hope sio mwisho huu.

  Shy kitu kingine hi ni website ya gazeti la hoja..kama ulishwa wahi ona gazeti ya Rai.Kwa hiyo sidhani kama tutegemee vibwagizo vingi.Mie nahitaji makala za uchambuzi na zenye ukweli.Kama lilivyo kuwa Rai.Uku mbali niliko..watakuwa wamenisaidia sana kujua nini kinaendela kwenye Ari mpya..kasi mpya na nguvu zaidi.

  Salaam zao
   
 13. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #13
  Oct 31, 2007
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  nimekupata ulivyosema kuhusu hili ni gazeti la hoja

  kwahiyo basi wangekuwa ndio watu wakwanza kuruhusu watu wenye hoja mbali mbali kushiriki katika kutoa na kujibu hoja hizo yaani mtu awe na account yake aweze kuandika hoja zake na wengine wachangie na kujibu

  mfano wewe uko zako huko ulipo sio lazima utume email kwenda raia mwema unaweza kutengeneza account yako ukaweka hoja yako na ikajibiwa mambo kama hayo

  tafadhali angalia www.antiwar.com hyio ni mfano wa tovuti za hoja watu toka sehemu mbali mbali wanashiriki katika kuleta hoja kutetea hoja zao makala zao na kadhalika

  Jioni njema leo naenda katika send off kwa mara ya kwanza
   
 14. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2007
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nimekupata Shy...
  Nimekuelewa kabisa nasubiri watu wengine wachangie..hiyo web site nimeitembelea..ni kweli iko juu.Hope na hawa watafikia hatu hiyo uko mbeleni.Hope utatujuza kwenye habari mchanganyiko ukitoka kwenye send off.
  Jioni Njema
   
 15. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #15
  Nov 6, 2007
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Bado liko usingizini,natazama labda hili ni toleo la kwanza na hawajajipanga,maana utaliona limejaa lakini habari zote ni zile kwa zile isipokuwa zimeletwa kwa rangi mbali mbali.
   
 16. K

  KGM Senior Member

  #16
  Mar 19, 2009
  Joined: May 21, 2007
  Messages: 188
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kutokana na mwenendo unaoendelea sasa hivi wa ufisadi ulio kubuhu unaosaidiwa kwa kiwango kikubwa na magazeti, nimejiuliza maswali mengi sana kuhusu uungwana wa Jenerali ulimwengu kuunguza magazeti yake kwa mafisadi.

  Kitu gani hasa kilimfanya Jenerali auze magazeti yake kisha baadaye aanzishe gazeti jingine? Alisukumwa na roho gani hasa?. Yeye ndiye aliwafuata wanunuaji au wanunuaji ndio walimfuata.? Hakujua lengo lao? Kwani nini aliyacha haya magazeti ambayo yamegeuka kinyaa machoni pa wananchi.?

  Naamini kama RA angenzisha gazeti jipya isingekuwa rahisi kuchipua. Mimi binafsi ilinichukua mda kujua kama Generali kisha uza magazeti yake, inaonyesha aliuza kimya kimya. Si usaliti mwingine kweli. Gazeti pendwa la RAI leo hii liko chini ya RA, kweli ni sawa?

  Hebu Chukulia leo hii USIKIE CHECHE na KLH News yako mikononi wa Lowasa+RA, tutamwitaje mwanakijiji? Sitakuwa kama bw MDOGO Zito Kabwe
  Mr Down alivyotutia vidole machoni?

  Naombeni tujadfili nini hasa kilimsukuma huyu ulimwengu kufanya aliyoyafanya.

  Nawasilisha.
   
 17. Kandambilimbili

  Kandambilimbili R I P

  #17
  Mar 19, 2009
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 782
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ni msukumo wa kibiashara, halina ubaya na sio usaliti, kapata mshiko kaanzisha gazeti lingine, wakati RAI inashuka la kwake jipya linapanda, ukitaka punda au mlio sawa, cha muhimu ni ujumbe sio lazima tusome Rostam Aziz Intelligency (RAI).

  Hata Umeona GENERAL ON MONDAY inaitwaje sasa hivi?
   
 18. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #18
  Mar 19, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Aligundua kwamba kati ya waandishi wake aliyewaamini tayari walishawekwa mfukoni mwa hao hao mafisadi ama kwakutokujua, kuahidiwa vyeo mahali pengine(ikulu) au kwa njaa zao. Ili asijekuingizwa kwenye huo mkenge nafikiri akaamua yaishe.
   
 19. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #19
  Mar 19, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Partners wake wawili -- Salva Rweyemamu na (Dr?) Gideon Shoo walikuwa wanampiga vita kichinichini -- na inasemekana wao hawa ndiyo walichochea/walimchongea kwa serikali kuhusu utata wa uraia wake na hivyo kunyang'anywa uraia kwa muda fulani.

  Walishinikizwa kufanya hivyo na RA pamoja na fisadi mwenzake EL ili kama Jenerali angefukuzwa nchini kwa sababu ya kutokuwa raia, basi wao wangebaki warithi wa hayo magazeti na yangetumiwa kukamilisha ajenda yao ya kuununua urais.

  Suala la "uraia" liliposhindikana, basi Salva na Shoo wakaanza kuitafuna kampuni polepole, kwanza bila ya Jenerali kujua, kwani aliwaamini sana -- na alipowashitukia, akakuta muflisi. Ikabidi atafutwe mnunuzi wa haraka -- na hivyo RA akapatikana kwani alikuwa tayari anazo pesa za kagoda.

  Naamini kabisa Jenerali alilazimika kuuza kampuni ama sivyo ingekufa kabisa na katika hali ya kawaida asingemuuzia fisadi RA.
   
 20. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #20
  Mar 19, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Pole sana Ulimwengu kwa kilichokupata,kilichompata Ulimwengu ndio kilikuwa kinamnyemelea Mengi wa IPP lakini wakakuta WaTZ wamekwisha wagundua.Rostam Aziz,Lowassa na Chenge ndio vinara wa dili zote za kuiba mali za umma.JK aliingizwa kama ngazi ya EL kupatia Urais,Mkapa naye kajizolea kivike kwa kumtumia Mke wake Mchagga anayejua pesa kwa kuwa mgombea wake alizidiwa kete na mtandao.Sasa wenye magazeti wote chondechonde msiuze kabisa magazeti yenu kwa mafisadi kwa kuwa watawapa wananchi/wasomaji habarimajitaka.Tuwe makini na magazeti na waandishi yanayoshabikia ufisadi na mafisadi ili yasemwe watanzania wayasusie.
   
Loading...