Kesi inayomkabili Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Raia Mwema na wenzake kuendelea kusikilizwa Novemba 29

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mchakato wa kesi Namba 407 ya 2022 ya Kimtandao katika Kundi la WhatsApp inayokambili Mwandishi wa Habari za afya na uchunguzi wa Gazeti la Raia Mwema, Mary Victor na wenzake wawili, Asha Mahita na Rogers Simeo inatarajiwa kuendelea Novemba 29, 2023.

Usikilizaji wa mashahidi katika kesi hiyo inayosikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilala ulianza Januari 17, 2023.

Maria Victor anatuhumiwa na makosa matatu likiwemo la kutumia Laini ya simu ambayo imesajiliwa kwa jina la mtu mwingine (Asha Mahita), kutuma taarifa ya uongo kuhusu maambukizi ya UVIKO-19 katika Kundi la Waandishi kwenye Mtandao wa WhatsApp.

Naye, Asha Mahita na Rogers wanatuhumiwa kwa pamoja kushindwa kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) juu ya mabadiliko ya umiliki wa laini hiyo ya simu yenye namba 0715166210.

Katika kesi hiyo, Mary na wenzake wanawakilishwa na wakili kutoka Taasisi ya Sibaba Alex Masaba na wakili kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania Anti Human Traffic and legal Initiatives Frank Mposso.

Washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana huku simu za baadhi ya washtakiwa, vitambulisho vyao vikiendelea kushikiliwa katika Kituo cha Polisi Kati (Central).

Hukumu ya Kesi - Mahakama yawaachia huru Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Raia Mwema na wenzake wawili
 
Ugonjwa wenyewe wa uviko19 haupo, kutumia laini ya mtu mwingine nako ni jambo la kawaida sana watu wanapeana laini na maisha yanaendelea. Kesi zingine ni za ajabu sana. Hao mawakilishindwa kupangua kesi hii nyepesi vichwa vitakuwa vimejaa vitu vingine badala ya ubongo wa kawaida wenye akili
 
Back
Top Bottom