Mahakama yawaachia huru Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Raia Mwema na wenzake wawili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam imeifuta Kesi Namba 407 ya 2022 ya Kimtandao katika Kundi la WhatsApp iliyokuwa ikimkabili Mwandishi wa Habari za Afya na Uchunguzi wa Gazeti la Raia Mwema, Mary Victor na wenzake wawili, Asha Mahita na Rogers Simeo.

Uamuzi huo wa kufuta kesi na kuwaachia huru umefikiwa Desemba 29, 2023 baada ya kuonekana Watuhumiwa hawana kesi ya kujibu kutokana na ushahidi uliotolewa na Jamhuri.

Maria Victor alituhumiwa makosa matatu likiwemo la kutumia Laini ya simu ambayo imesajiliwa kwa jina la mtu mwingine (Asha Mahita), kutuma taarifa ya uongo kuhusu maambukizi ya UVIKO-19 katika Kundi la Waandishi kwenye Mtandao wa WhatsApp.

Upande wa Asha Mahita na Rogers walituhumiwa kwa pamoja kushindwa kutoa taarifa kwa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) juu ya mabadiliko ya umiliki wa laini hiyo ya simu yenye namba 071516621.

Mary na wenzake waliwakilishwa na Wakili kutoka Taasisi ya Sibaba Alex Masaba na Wakili kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania Anti Human Traffic and legal Initiatives, Frank Mposso.

Awali, wakati mchakato unaendelea, Washtakiwa wote walikuwa nje kwa dhamana huku simu za baadhi ya washtakiwa, vitambulisho vyao vikiendelea kushikiliwa katika Kituo cha Polisi Kati (Central).

Pia soma:
= Kesi inayomkabili Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Raia Mwema na wenzake kuendelea kusikilizwa Novemba 29
= Mashahidi 9, vielelezo 10 kutumika katika kesi ya mwandishi wa habari wa Gazeti la Raia Mwema
 
Central Police Station ni Kituo Kikuu cha Polisi katika mji husika. Sio kituo cha kati.
 
Back
Top Bottom